Mhandisi: Reli ya SGR mpya kuchukua miaka 15 kumalizika


Unaweza kutupatia wasifu wa huyo Msomi Mtanzania wa mambo ya reli.
 
18 Apr 2020
Dar es Salaam, Tanzania

March 2020 Progress Video; Tanzania Standard Gauge Railway Line From Dar Es Salaam to Morogoro


About Yapi Merkezi: YM is ranked as 78th in 2017 in the Top International Contractor’s List prepared by monthly magazine Engineering News Record (ENR).

Source: Yapi Merkezi Tanzania
 
April 21, 2020
MDM March 2020 Progress Video : Tanzania Standard Gauge Railway Line From Morogoro to Makutupora, Dodoma.


Source : Yapi Merkezi Tanzania
 
April 21, 2020
Mbeya, Tanzania
Reli urefu kilometa 1860 ya TAZARA iliyojengwa kwa miaka sita
Karakana Pekee nchini ya TAZARA ya Ufufuaji, Uundwaji, Utengenezaji Vichwa vya Treni Nchini


Wafanyakazi wenye uzoefu adimu wa miaka 40 wakiwafundisha wale wapya kwa pamoja wanaonesha ujuzi wao wa kukarabati locomotive (vichwa vya treni), kutengeneza vipuri n.k kwa kutumia vyombo vya kisasa ili treni za TAZARA ziendelee kufanya kazi ktk reli hiyo yenye urefu wa kilometa 1860 iliyojengwa kuanzia mwaka 1970 na kuisha 1976 kufanikiwa kuiunganisha Dsm Tanzania na mji wa katikati ya Zambia wa Kapiri Mposhi ktk ukanda wa migodi ya shaba. .
Source: MbeyaYetuOnline TV
 
April 24, 2020
Mbeya, Tanzania

Reli ya TAZARA urefu wa kilometa 1860 ilichukua miaka sita kukamilika

inayounganisha bandari ya Dar es Salaam na mji wa New Kapiri Mposhi , Zambia. Reli hiyo yenye mahandaki 18, madaraja 18 na kalivati 36 ilichukua miaka 6 kuikamilisha. Daraja ktk mto Mpanga lina kina cha futi 160ft , pia milima mingi kupasuliwa, miinuko mikubwa na miteremko mirefu na sehemu ya Uyole ipo zaidi ya futi 5,000 toka usawa wa bahari na kuonesha changamoto nyingi wakati wa ujenzi wa reli hiyo. Ujenzi ulianza mwaka 1970 na kukamilika mwaka 1976.


Pia TAZARA ilijenga karakana kubwa iliyopo Iyunga mjini Mbeya, Tanzania mwaka 1983 kutokana na kuwa katikati ya reli baina ya Tanzania na Zambia. Karakana ina ukubwa wa square metres 71,000. Locomotive za TAZARA ziliagizwa toka Germany, USA na China.

Locomotive za TAZARA zinauwezo wa 3,000 Horsepower na kichwa kimoja kinaweza kufunga mabehewa 36 na kuyakokota kutegemeana na jiografia ya eneo inapopita mfano Mlimba kwenda Dar es Salaam ni tambarare.

Source : MbeyaYetuOnline TV
 
April 11, 2020
Mbeya , Tanzania

Waziri Isack Kamwelwe: Tanzania 'yasusiwa' reli ya TAZARA, ila tuna matumaini Zambia wataleta mchango wao hivi karibuni.


Source: MbeyaYetuOnlineTV
 
April 11, 2020

Mradi wa JNHPP watumia TAZARA

Vifaa vya Ujenzi wa mradi wa Julius Nyerere Hydropower Project maarufu Stiegler's Gorge vikisafirishwa na TAZARA kwenda Kisaki Morogoro, Tanzania

Source : Tanesco Yetu
 
April 29, 2020
Kilosa, Morogoro

UJENZI WA KIVUKO CHA RELI MPYA YA KATI SGR LOT 2 UNDERPASS,TRENI ITAPITA JUU MAGARI CHINI, HAPA NI KILOSA

Kipande cha Morogoro kuelekea Makutupora ujenzi wa reli mpya SGR, inategemewa treni ya umeme itakuwa inakimbia kilometa 160 kwa saa.
Underpass ( magari yatapita chini na treni inapita juu ) kama inavyoneshwa ktk video ni kuepusha ajali na pia kuwezesha magari na treni kuendelea na mwendo bila kikwazo.

Source : TRC RELI TV
 
Nani kakwambia kuwa hii si Siasa? Don't be miopic brother. This is typically politics. Na ndo maana politicians wakiulizwa kutaja achievements zao hawaachi kutaja SGR!
 
Huu mradi mbwembwe nyingi mara underpass, overpass, tunnels, stesheni za kisasa, e-ticketing, viaducts , kutengeneza matuta ya mamia ya kilometa ambayo hata reli za Canada au USA hayapo. Sishangai mhandisi aliyesema itachukua miaka 15 kumaliza mtandao mzima wa reli mpya ya SGR inaonekana yupo sahihi kabisa.

Meter gauge railway MGR reli ya kati ya mkoloni haikuwa na mbwembwe zote hizo na ina sehemu chache korofi ambazo serikali ingezitatua bila kujiingiza ktk ujenzi wa SGR railway unaoigharimu serikali pesa nyingi.
 
May 3, 2020
Pwani, Tanzania

TRENI YA MGR MKOLONI YAINGIZA SHEHENA YA MAKONTENA NDANI YA BANDARI KAVU YA KWALA.
Bandari kavu ya Kwala iliyopo mkoani Pwani nchini Tanzania umbali wa kilometa 90 New Dry Port to Change Face of Ruvu, Bringing More Power Hungry Business toka bandari kuu ya Dar es Salaam leo imeweza kupokea treni ya MGR ya mkoloni ikiwa imesheheni makontena yaliyopakiwa ktk mabogi ya wazi.

Na bandari hiyo kavu ya Kwala kuweza kuisaidia bandari kuu ya Dar es Salaam kupunguza msongamano wa mizigo, magari ya usafirishaji, taratibu za forodha sawia na kuongeza ufanisi wa kupakua na kupakia mizigo ktk bandari ya Dar es Salaam.
Source : TRC RELI TV
 
May 4, 2020
Dar-Es-Salaam, Tanzania

RELI MATUKIO - UKARABATI RELI METER GAUGE (MGR) MKOLONI, UJENZI SGR DAR-MORO SASA NI ZAIDI YA 77%. UJENZI STESHENI YA DAR WAZIDI KUNOGA !

Mkurugenzi wa miundo-mbinu wa TRC mhandisi Faustine Kataraia anazungumzia changamoto na maendeleo ya ujenzi wa mitandao ya reli ya mkoloni ya kati MGR na ile reli mpya ya SGR . Kufurika kwa Mto Ugalla na kuathiri reli ya kule Mpanda Kaliua Tabora pia mafuriko huko Korogwe katika reli ya Tanga.....Train Control Room kwa ajili ya kuratibu mawasiliano na ishara / signals ktk mtandao mzima wa reli nchi nzima. SGR Kilosa Gulwe mahandaki na daraja.


Source : TRC Reli TV
 
May 7, 2020
Ugalla, Tabora
Tanzania

KAZI YA KUREJESHA RELI YA TABORA MPANDA INAENDELEA

Kazi ya kukarabati njia ya reli iliyosombwa na maji mengi ya mto Ugalla kwenda Mpanda inaendelea usiku na mchana kwa wahandisi wa reli TRC kutupa mawe ktk mto Ugalla wenye kina cha mpaka mita 4 ili kurudisha mawasiliano ya treni ktk reli hiyo ya mkoloni MGR.

Source : TRC Reli TV
 
Kazi kweli kweli, hata tukiwauliza reli hii itapomalizika miaka 15 ijayo, itaosaidia nchi hii ya Tanzania kivipi hakuna maelezo yaliyo nyooka.

Ni full ' mazingaombwe' ili kutumia kupata kura lakini ndiyo hivyo wakati mwingine ukiwa na mambo mengi lazima mengine yakwame.

SGR reli, MGR reli, TAZARA reli, Ndege ATCL, Stiegler's Gorge, Madaraja yote miradi mikubwa ya gharama kubwa kwa nchi masikini kama Tanzania.
 
May 8, 2020
Igala Tabora
Tanzania

Kazi ya Kukatiza mto mkubwa wa maji

Wahandisi waelezea mbinu wanayotumia kuvusha reli ya mkoloni MGR kukatiza mto Ugalla unaotenganisha mikoa ya Tabora na Katavi


Source : TRC Reli TV
 
Mfano wa ujenzi wa Gabion unaotumiwa na Shirika la Reli Tanzania TRC kujenga daraja la gabion kuvuka mto Ugalla ktk mpaka wa mikoa ya Tabora na Katavi. Wahandisi wa TRC wanasema pia kutakuwepo kuta za gabion kadhaa kupunguza kasi ya maji ya mto Ugalla .
 
May 8, 2020
Tabora, Tanzania

Reli ya mkoloni MGR Tabora Kaliua Mpanda
Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi na kamati ya ulinzi na usalama wafika kwa boti, watembelea eneo la mto Ugalla ambapo daraja la aina ya gabion (mawe yaliyofungwa ndani ya makasha yaliyosukwa kwa nyaya) yanatengeneza kivuko.


Source : TRC Reli TV
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…