Mhandisi: Reli ya SGR mpya kuchukua miaka 15 kumalizika

Mhandisi: Reli ya SGR mpya kuchukua miaka 15 kumalizika

22 June 2023
Maafisa Habari kutoka Zanzibar Watembelea Mradi wa SGR Reli Mpya




Ikumbukwe kuwa bandari kavu, michepuko (rail network) na njia kuu za reli pia zimo katika mkataba wa bandari za bahari kuu na maziwa makuu, mito ya maji kuboreshwa chini ya mkataba baina ya Dubai na Tanzania kuendesha miundombinu ya kimkakati kupitia DP World.

Bandari na Reli kuunganishwa katika mkataba wa DP World ni kuhakikisha mizigo inayopakuliwa au kupakiwa inafika kunakohusika kwa wakati, hivyo muunganiko huu muhimu wa kimkakati kutiwa ndani ya mkataba wa IGA baina ya Tanzania na Dubai ulipitishwa June 10 2023 na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma.
 
30 September 2022
Abu Dhabi, UAE

Mfuko wa Abu Dhabi kutoa $420 millions sawa na Tshs 1.0 trilioni kugharamia miradi Tanzania ikiwemo mradi wa SGR Reli.

1687775316123.png

Waziri Mwigulu Nchemba ziarani UAE akutana na bw. Mohammed Saif Al Suwaidi mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Abu Dhabi

Mkurugenzi wa the Abu Dhabi Fund amesema Tanzania imewasilisha andiko kwa Fuko hilo la Fedha la Abu Dhabi kwa ajili ya miradi mbalimbali ya kimkakati Tanzania bara na visiwani
 
30 June 2023

PPRA WATEMBELEA MRADI WA SGR RELI MPYA



Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) watembelea maeneo ya mradi wa ujenzi wa reli mpya ya kiwango cha SGR ambao unaendelea

Leo 23 June 2023 tovuti ya Shirika la Reli Tanzania imeonesha limepokea ugeni wa bodi ya wakurugenzi kutoka Mamlaka ya Udhibiti Ununuzi wa Umma - PPRA ambapo wamefanya ziara ya siku mbili kutembelea ujenzi wa mradi wa reli ya kisasa - SGR kutoka Dar es Salama hadi Dodoma hivi karibuni Juni, 2023.

Bodi ya wakurugenzi kutoka PPRA imetembelea mradi wa SGR kwa lengo la kukagua na kujiridhisha juu ya thamani ya fedha iliyotumika kukidhi viwango vinavyotakiwa katika kujenga mradi huo mkubwa wa kimkakati.

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi kutoka PPRA Dkt. Leonada Mwagike ameeleza kuwa ujenzi wa mradi wa SGR umekidhi viwango na ubora utakaowezesha usafirishaji wa abiria na mizigo kwa muda mfupi na treni kufika sehemu kwa wakati.

“Tumeona ubora wa ujenzi uliowekezwa katika mradi huu na nimefurahishwa kwakuwa watanzania wengi wana ujuzi wa kuusimamia mradi huu mkubwa” alisema Dkt. Mwagike.

Naye Mtendaji Mkuu kutoka PPRA Bw. Eliakim Maswi alisema kuwa fedha za umma zinatakiwa zitumike kulingana na maelekezo na Sheria iliyopo hivyo maendeleo ya mradi huo unaenda sambamba na thamani ya fedha iliyowekwa na Serikali.

“PPRA jukumu lake ni kukagua na kuona matumizi yaliyotumika yanalingana na thamani ya fedha iliyowekwa, vitu vilivyofanywa katika mradi huu ni vikubwa sana” alisema Bw. Maswi.

Mkurugenzi Mkuu kutoka TRC Ndugu Masanja Kadogosa ametoa shukurani kwa bodi ya wakurugenzi kutoka PPRA kwa kutembelea mradi wa SGR na kuona maendeleo ya mradi pamoja na kujiridhisha katika maeneo mbalimbali.

“Inatoa picha nzuri kwa kile walichokiona kwenye makaratasi na kuhakiki ujenzi uliofanyika hivi sasa, PPRA kwetu ina umuhimu sana kwa maana ya manunuzi tunafuata Sheria za PPRA“ alisema Ndugu Kadogosa.

Naye Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi kutoka PPRA mhandisi Sylvester Mayunga alisema kuwa reli ya kisasa imejengwa kwa viwango na ubora mkubwa kwa kujenga njia iliyonyooka na kudhibiti sehemu korofi zenye maji kwa kupitisha reli kwenye mahandaki.

“Usimamizi umekuwa mzuri na tumeona vitu vingi vipo imara kuanzia mataruma, kuweka vitu vya kudhibiti wizi na hujuma kwenye njia ya reli “ alisema Mhandisi Mayunga.

Mradi wa SGR kipande cha kwanza kutoka Dar es Salaam - Morogoro kimefikia 98.26% na kipande cha pili kutoka Morogoro - Makutupora 94.19%.

1688204416380.png

Habari na picha kwa hisani ya tovuti ya TRC
The Public Procurement Regulatory Authority (PPRA) is a regulatory body established under the Public Procurement Act,2004 as repealed by the Public Procurement Act,2011.The Authority is charged with regulatory functions and vested with oversight powers and responsibilities on all public procurement activities carried by all public bodies in the mainland Tanzania.

The objectives of PPRA are to ensure the application of fair, competitive, transparent, non-discriminatory and value for money procurement standards and practices; set standards for the public procurement systems in United Republic of Tanzania; monitor compliance of procuring entities;and build ,in collaboration with Public Procurement Policy Division and other relevant professional bodies, procurement capacity in the United Republic.

Our Vision: "A public procurement system with integrity, offering best Value for Money"

Our Mission: "To regulate public procurement system and promote best practices in order to attain best value for money and other desired socio-economic outcomes"
 
06 Agosti 2023

TRC limefanya semina ya siku mbili ya maadili kwa watumishi





Shirika la Reli Tanzania - TRC limefanya semina ya siku mbili ya maadili kwa watumishi wanaosimamia ujenzi wa mradi wa Reli yenye kiwango cha kimataifa - SGR katika ukumbi wa bandari jijini Dar es Salaam, Agosti 2023.

Semina hiyo imehusisha watumishi wa reli wanaosimamia ujenzi wa mradi wa reli yenye kiwango cha kimataifa kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza kwa awamu ya kwanza wakiwemo mameneja na wasaidizi wao, maafisa jamii, maafisa mazingira na maafisa ardhi kutoka TRC.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Bi. Amina Lumuli amesema lengo la mafunzo ni kutoa uelewa na kufuata Sheria na taratibu za maadili za Utumishi wa Umma kwa wasimamizi wa miradi na watumishi wa kada mbalimbali zinazohusika na ujenzi na mradi wa reli yenye kiwango cha kimataifa - SGR katika awamu ya kwanza ambayo ni Dar es Salaam hadi Mwanza na awamu ya pili Tabora - Kigoma.

Watoa mada katika semina walikua maafisa kutoka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, TAKUKURU na Idara ya Usalama wa Taifa.

"Tunajua kwamba mradi huu unajengwa kwa gharama kubwa kwahiyo wasimamizi wa mradi leo wamepata elimu kutoka TAKUKURU dhidi ya Rushwa wawapo maeneo ya kazi sababu wanaweza kushawishika kwa namna moja au nyingine" ameongeza Bi. Amina Lumuli.

Afisa Masuala ya Jamii Bi. Tumaini Rikanga amesema kupitia semina hii amejifunza namna mtumishi wa Serikali anavyopaswa kufuata Sheria na kanuni za kazi katika utendaji kazi na kuhudumia jamii kwenye eneo lake la kazi.

TRC imeaminiwa na Serikali katika kusimamia ujenzi wa reli ya kiwango cha kimataifa - SGR katika awamu ya kwanza Dar es Salaam - Mwanza na ujenzi wa awamu ya pili Tabora hadi Kigoma ambao umeanza katika hatua za awali.
Source : tovuti ya TRC Reli

N.B
. Ikumbukwe reli na barabara zinategemewa kuinua ufanishi wa bandari
 
Ukarabati wa TAZARA ni muhimu ili bandari ya Dar es Salaam ifikiwe kwa uharaka kupokea na kupakua mizigo mingi ya Zambia

 
11 May 2023
Beira, Mozambique

Rais wa Zambia atembelea bandari ya Beira Mozambique



Ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kwanza ya kiserikali, Rais wa Jamhuri ya Zambia, mheshimiwa Hakainde Hichilema, alitembelea Bandari ya Beira tarehe 6 Aprili 2023.

Alitembelea gati za namba 3, 4 na 5 mahsusi kwa ajili ya makontena na gati za mizigo mchanganyiko (general cargo) , na alifurahishwa sana na vifaa vya ikiwemo kreni kubwa za kisasa Ship-to-Shore ktk Bandari ya Beira na haswa na teknolojia ya hali ya juu inayotumiwa na Cornelder de Moçambique katika shughuli zake.
 
Beira, Mozambique

Kreni kubwa za kisasa za Ship-to-Shore muonekano wake bandari ya Beira, nchini Mozambique

 
Mozambique

UWEZEKAJI KATIKA MAPACHA WALIOUNGANIKA YAANI RELI NA BANDARI

Miundo-mbinu ya reli (the cape gauge 1067mm) inayofanya bandari za Beira na Nacala nchini Mozambique kuwa na ufanisi wa kuondoa mizigo na kuifikisha kwa uharaka bandarini

 
Maputo, Mozambique

UFANISI NDIYO UTAMBULISHO WA BANDARI YA MAPUTO, RELI NA BANDARI ZACHANGIA PAKUBWA



Bandari ya Maputo kwa sasa ndiyo yenye ufanisi zaidi katika eneo hili la Afrika kwa suala la muda wa meli kusubiri kufikia gati.

Pia ni katika Bandari ya Maputo ambako malori ya mizigo huchukua muda mfupi kupakua.
Sababu hizi, pamoja na hali ya nzuri ya miundo-mbinu ya usambazaji / ugavi kuifikia bandari , huifanya iwe bora zaidi kwa nchi za jirani .

Utendaji wa Bandari ya Maputo umeimarika sana: muda ambao meli husubiri kufika kwenye gati ni saa 24 tu, dhidi ya siku saba ambazo ni wastani wa muda wa kusubiri bandarini katika eneo hili la Afrika.

Malori nayo huchukua chini ya dakika tisini, kutoka kwenye eneo la Bandari ya Maputo hadi kupakua mizigo.
Mambo haya muhimu na nyeti kwani husaidia mawakala wa meli kuamua ni bandari gani ya kutumia kwa ajili ya kusafirisha na kuagiza bidhaa.

Bandari ya Maputo imefanya mapinduzi ya kiutendaji kazi kwa uwazi. Inachukua nafasi ya rekodi zilizotengenezwa kwa karatasi na fomu ambao ni wa kizamani na sasa kuanza kutumia mifumo ya kidijitali katika shughuli zote za bandari.

Uwekezaji unaofanywa katika teknolojia ya tehama unawaruhusu wateja na wale wote wanaohusika katika mnyororo mzima wa usafirishaji kufuata mizigo / makontena , mara tu zinapofika bandarini.

Taratibu hizi za uwazi wa tehama zimepunguza upotevu wa mizigo na kuinua kiwango cha uaminifu kati ya wasimamizi na watumiaji wa Bandari ya Maputo.

MPDC, mwendeshaji wa Bandari ya Maputo, sasa anakadiria ukuaji marudufu wa mizigo inayopita Bandari ya Maputo kwa miaka kumi ijayo
 
BARABARA YA TANZAM MLIMA KITONGA INAVYOONESHA MIZIGO YA ZAMBIA, MALAWI, CONGO DR, ZIMBABWE INAHITAJI RELI YENYE UFANISI BANDARI YA DAR ES SALAAM IWE KIMBILIO LA WATEJA ZAIDI

 
25 August 2023

MABEHEWA CHAKAVU 673 KUFANYIWA UKARABATI MKUBWA ILI KURUDI KUFANYA KAZI KTK RELI MGR YA MKOLONI


View: https://m.youtube.com/watch?v=ZOYYz9QUvi0

Mradi mkubwa wa kukarabati mabehewa chakavu na yaliyopata ajali ulioanza January 2023 unaendelea na utachukua miaka miwili kukamilika ili kuongeza ufanisi wa kusafirisha mizigo na abiria ktk mtandao wa reli ya mkoloni maarufu MGR.

Mabehewa hayo yanayofanyiwa karabati kutokana na overdue date of repair ni 600 ya mizigo na 37 ya abiria. Jumla ya vibarua 200 waliomaliza vyuo vya ufundi na chuo cha reli wameajiriwa kukamilisha kazi hiyo muhimu ya kusafirisha mizigo
Source : TRC Reli TV
 
Nimeisikiliza zaidi ya mara moja.
Ni kweli SGR itakamilika kati ya miaka 10-15. Mhandisi amejiongeza namna ya kulisema hili.

Ameongelea namna MGR itakavyowasaidia wananchi temporarly hadi hapo mtandao wa SGR utakapokamilika. Ukisikiliza haraka huku unamfikiria bashite 😀 huwezi kuielewa implication ya anachokisema.
Kipande gani?
 
Strategic Infrastructure Development in Tanzania: Presenter: Eng. CHEDI MASAMBAJI

STANDARD GAUGE RAILWAY (SGR) INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT

View: https://m.youtube.com/watch?v=NukHe4FL7d4

  1. Introduction of Strategic Projects
  2. Tanzania Railway Network
  3. Types of Railways in Tanzania
  4. SGR Railway Network Development Phases
  5. SGR Phase I Development
  6. SGR Phase II Development
  7. Other Phases Development
  8. SGR Phase I Implementation
  9. Photo from Site
  10. Contract Types Used
Source : African Intellectuals
 
11 September 2023

Bw. Ally Amani Karavina mwenyekiti mpya wa Bodi ya Shirika La Reli Tanzania atoa ahadi nzito


View: https://m.youtube.com/watch?v=m1HuVy7k-0c


news title here

12 SEPTEMBER 2023

Shirika la Reli Tanzania - TRC imefanya hafla fupi ya uzinduzi wa Bodi mpya ya wakurugenzi iliyo ongozwa na mgeni rasmi Waziri wa Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa iliyofanyika katika jengo la stesheni ya SGR lililopo jijini Dar es Salam Septemba 11, 2023.

Bodi mpya iliyozinduliwa ni pamoja na Mwenyekiti wa Bodi Bw. Ally Karavina akiwa na wajumbe wa Bodi ambao ni Dtk. Shaaban Ramadhani Mwijaka, Bw. Narcis Aloyce Lumumba, Bw. Masanja Kungu Kadogosa, Bw. Shaaban Ahmed Kabunga, Bw. Plasduce Mkeli Mbossa na Bw. Redemtus Peter Bugomola.

Prof. Mbarawa ameipongeza Bodi mpya ya wakurugenzi ya TRC kwa kuaminiwa na Serikali na kuteuliwa kusimamia Shirika la Reli Tanzania ambalo linatoa huduma ya usafiri wa abiria na mizigo kwa njia ya reli.

“Niipongeze pia Bodi iliyomaliza muda wake kwa kazi nzuri waliyoifanya ya usimamizi wa huduma za Shirika pamoja na miradi ya kimkakati ukiwemo wa SGR na mradi wa kukarabati reli ya kati kipande cha Dar es Salaam - Isaka” alisema Mhe. Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa alieleza kuwa Serikali inaendelea kuweka fedha katika mradi wa ujenzi wa SGR ambao unaendelea vyema katika vipande vitano vya awamu ya kwanza ambapo kipande cha kwanza Dar es Slaam - Morogoro kina urefu wa kilometa 300, kipande cha pili Morogoro - Makutupora chenye urefu wa kilometa 422, kipande cha tatu Makutupora - Tabora chenye urefu wa kilometa 368, kipande cha nne Tabora - Isaka chenye urefu wa kilometa 165 na kipande cha tano Isaka - Mwanza chenye urefu wa kilometa 341 na kipande cha sita Tabora - Kigoma chenye urefu wa kilometa 506.

Hata hivyo Prof. Mbarawa alisema kuwa TRC inaendelea na ukarabati wa reli ya kati kwa kipande cha Kaliua - Mpanda, ujenzi wa daraja kipande cha Kilosa - Gulwe pamoja na ukarabati wa maeneo mbalimbali kati ya Dar es Salaam na Isaka kupitia mradi wa TIRP 2.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TRC ambaye pia ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala Bi. Amina Lumuli amefafanua kuwa bodi ya wakurugenzi ya TRC inaundwa kwa mujibu wa kifungu cha 12, kifungu kidogo cha 1 (a) cha Sheria ya Shirika la Reli Na. 10 ya mwaka 2017 ambayo inakua na Mwenyekiti pamoja na wajumbe saba ambao wanatoka katika ofisi mbalimbali za Serikali.

“Kwa mujibu wa kifungu hicho wajumbe wa Bodi wanatakiwa kuwa na taaluma ya Uhandisi, Rasilimali Watu, Utawala na Biashara, Sheria, Uchumi, Fedha na Usafirishaji” alizungumza Bi. Amina.

Bi. Amina alieleza kuwa TRC ina jumla ya wafanyakazi 2974 kati yao 2688 ni wa ajira ya kudumu na 286 ni wa ajira ya mkataba.

TRC imekuwa na mchango mkubwa katika kutoa huduma za usafirishaji wa njia ya reli kwa jamii ambapo pasi na uendeshaji wa treni za abiria na mizigo kwa masafa marefu na treni za mijini pia TRC inaendelea na miradi ya ujenzi ukiwemo mradi mkubwa wa kimkakati wa SGR, mradi wa ukarabati wa reli ya kati kwa vipande mbalimbali pamoja na ukarabati wa vichwa vya treni na mabahewa.

Sources : TRC Reli TV / https://www.trc.co.tz/news/mbarawa-azindua-bodi-mpya-ya-wakurugenzi-trc
 
12 September 2023
Dar es Salaam, Tanzania

Eneo Vingunguti Dar es Salaam kipande cha reli SGR MPYA


View: https://m.youtube.com/watch?v=SXPQnXeiGwA

Maendeleoa ya ujenzi wa vivuko vitatu vya eneo muhimu la Vingunguti na barabara ya Julius Nyerere Road iendayo Airport na viwandani jijini Dar es Salaam ... wahandisi wanatupa maendeleo ya kazi katika eneo hilo lenye shughuli nyingi sana za kiuchumi ....
 
21 September 2023

Dola za Marekani bilioni 3.24 zahitajika kumalizia ujenzi wa SGR, Serikali ya Spain kupiga jeki pia


View: https://m.youtube.com/watch?v=pFvYoZSP40A
Zaidi ya Dola za Marekani bilioni 3.24 zinahitajika kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kwa kipande cha tatu, kipande cha nne na kipande cha tano kinachoanzia Makutopora hadi Mwanza na kipande cha Tabora hadi Kigoma.

View: https://m.youtube.com/watch?v=yu6zq9cU0EY
Ms Xiana Margarida Méndez Bértolo waziri wa nchi masuala ya biashara toka Hispania katika mazungumzo na mheshimiwa Mwigulu Nchemba

Pia mbali ya Hispania kufadhili ulipaji bima kwa mradi huo wa SGR reli mpya, kampuni ya kiHispania ya TYPSA inawafanya kazi za usanifu wa kina wa Sehemu ya Lot 4, Kipande cha Tabora hadi Isaka kina jumla ya kilomita 165 ambapo kilomita 130 ni njia kuu na kilomita 35 ni njia za kupishania. ikijumuisha kazi za civil engineering, majengo, stesheni, mifumo ya umeme, ishara na mawasiliano ya reli SGR mpya.
 
Zaidi ya Dola za Marekani bilioni 3.24 zinahitajika kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR)

Miradi mikubwa ya kimkakati kwa mkupuo mmoja yaani ujenzi wa SGR reli mpya, JNHPP Rufiji Stiegler's gorge, Ndege ATCL n.k zinaipa changamoto kubwa Tanzania
 
21 September 2023

Dola za Marekani bilioni 3.24 zahitajika kumalizia ujenzi wa SGR, Serikali ya Spain kupiga jeki pia


View: https://m.youtube.com/watch?v=pFvYoZSP40A
Zaidi ya Dola za Marekani bilioni 3.24 zinahitajika kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kwa kipande cha tatu, kipande cha nne na kipande cha tano kinachoanzia Makutopora hadi Mwanza na kipande cha Tabora hadi Kigoma.

View: https://m.youtube.com/watch?v=yu6zq9cU0EY

Pia Ms Xiana Mendez waziri wa nchi masuala ya biashara toka Spain mbali ya Hispania kufadhili ulipaji bima kwa mradi huo wa SGR reli mpya, kampuni ya kiHispania ya TYPSA inawafanya kazi za usanifu wa kina wa Sehemu ya Lot 4, Kipande cha Tabora hadi Isaka kina jumla ya kilomita 165 ambapo kilomita 130 ni njia kuu na kilomita 35 ni njia za kupishania. ikijumuisha kazi za civil engineering, majengo, stesheni, mifumo ya umeme, ishara na mawasiliano ya reli SGR mpya.


Secretary of State Ms. Xiana Margarida Méndez Bértolo in Tanzania, held talks with minister Mwigulu Nchemba

View: https://m.youtube.com/watch?v=yu6zq9cU0EY
Ms Xiana Margarida Méndez Bértolo spain's Secretary of State in talks with Tanzanian minister for finance Mr Mwigulu Nchemba


Madrid — SPAIN, Madrid : SPAIN, through its Export Credit +Agency (ECA), has expressed an interest in financing the Standard Gauge Railway (SGR) construction project by providing loans, loan guarantees and insurance to the country's companies that will build the railway from Makutupora to Mwanza and from Tabora - Morogoro to Malagarasi.

The country's decision comes due to the importance of the project to the development of the country.

The pledge was made in Madrid, Spain, by Secretary of State in-Charge of Commerce Ms Xiana Mendez, when she held talks with the Finance Minister Dr Mwigulu Nchemba, where, among other things, they discussed how to strengthen the bilateral cooperation between the two countries, including the construction of the massive SGR project.

"The participation of the Spanish Insurance Agency (Export Credit Agency-ECA) in implementing the strategic project is essential for the country's development and the long-term cooperation between Spain and Tanzania and the development of its people at large," Dr Nchemba said.

He said to strengthen relations and preparations for implementing the SGR funding, the contractor has sought 12 Spanish companies to supply the equipment used to build the railway and asked the Secretary of State Ms Xiana Margarida Méndez Bértolo and her Government, in general, to persuade more companies from the country to come forward to participate in the construction of the project.

Dr Nchemba said the SGR project is vital for Tanzania, because it is a trade gateway to seven land-linked African and Great Lakes countries that do not border the waters. He further argued that when completed, the project will stimulate trade, transport and freight operations and ultimately increase GDP
 

BODI YA WAKURUGENZI TRC YAMALIZA ZIARA KUKAGUA MRADI WA SGR​


SEPTEMBER 2023

news title here


Bodi ya Wakurugenzi Shirika la Reli Tanzania – TRC yamaliza ziara kukagua mradi wa ujenzi wa reli yenye kiwango cha kimataifa SGR kuanzia Dar es Salaam hadi Mwanza iliyofanyika kuanzia Septemba 15 hadi 19, 2023.

Bodi ya wakurugenzi TRC imefanya ziara kukagua mradi kwa lengo la kuona maendeleo ya mradi, kujifunza pamoja na kutambua changamoto za mradi kwa ajili ya kutoa muongozo na maelekezo ya kuhakikisha changamoto zinatatuliwa na mradi unakamilika kwa wakati.

“Tuko kwenye ziara na bodi mpya ya wakurugenzi, tumeanzia kipande cha kwanza na leo tunamalizia kipande cha tano lengo ni kupata uelewa wa kinachoendelea ili waweze kujua wapi wataanzia pale ilipoishia bodi iliyomaliza muda wake” alieleza Kaimu Mkurugenzi Mkuu Bi. Amina Lumuli

Mwenyekiti na wajumbe wa bodi ya wakurugenzi TRC waliambatana na menejimenti ya Shirika la Reli pamoja na wahandisi mbalimbali kwa ajili ya kupata taarifa za maendeleo ya mradi ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya reli, mifumo ya mawasiliano, ishara na umeme pamoja na maandalizi ya vifaa kwa ajili ya shughuli za uendeshaji ambavyo ni mabehewa na vichwa vya treni.

Mwenyekiti wa Bodi Bw. Ally Karavina amesema kazi za mradi zinaendelea vizuri ziko ndani ya muda na amewaahidi watanzania mradi kukamilika kwa wakati.

Mwenyekiti alieleza kuwa Miradi ya kimkakati ni miradi itakayobadilisha uchumi wa nchi kwenda kwenye uchumi wa juu ikiwemo mradi wa SGR.

Mradi wa SGR awamu ya kwanza Dar es Salaam – Mwanza wenye vipande vitano unaendelea sambamba na uagizwaji wa mabehewa na vichwa kwa ajili ya kuanza shughuli za uendeshaji pindi mradi utakapokamilika.

“Utengenezaji wa mabehewa unaendelea vizuri, tumeshapokea mabehewa 14 mapya lakini leo tuna mabehewa mengine mapya 15 yameanza kushushwa, pia tumepokea mabehewa 6 ya ghorofa.

Kwahiyo kwa upande wa mabehewa hakuna shida, kichwa cha kwanza cha treni tunatarajia kukipokea mwanzoni mwa mwezi Novemba 2023 ili tuanze majaribio” alisema Bi. Amina Lumuli kaimu mkurugenzi mkuu wa TRC.
1695768840780.png

Picha: kichwa cha treni (locomotive)

Bi. Amina Lumuli alisisitiza kuwa watanzania wategemeea huduma nzuri, Shirika limejipanga kwa wataalamu wanaopata mafunzo ndani na nje ya nchi pia maandalizi yanaendelea kuhakikisha wananchi wanapata huduma nzuri zenye ubora unaostahili.

Sambamba na ziara Bodi imeanza mafunzo ya siku mbili jijini Mwanza kwa ajili ya kuwajengea uwezo kuhusu namna ya kusimamia Shirika, Sheria pamoja na taratibu za kiutendaji katika shughuli za Bodi na Shirika kwa ujumla.
Source : trc.co.tz/news
 
SGR inahujumiwa na wenye MALORI ambao pia wapo viongozi na wanasiasa kwenye biashara hiyo.
 
Back
Top Bottom