Mwenyekiti wa zamani wa TAMWA na Mhariri Mkuu wa Clouds media Joyce Shebe amebainisha namna Waandishi wa Habari na Vyombo vya Habari kwa ujumla wake vilivyopata wakati mgumu kufanya kazi Oktoba 29 mwaka huu na siku zilizofuata, kufuatia vurugu zilizotokea siku hiyo ambazo zilisababisha uharibifu wa mali za umma na binafsi, majeruhi na vifo
Akizungumza kwenye mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila na Wahariri wa Vyombo vya Habari Nchini uliofanyika Desemba 5, 2025, Joyce Shebe ametoa swali la tafakuri kwa Wanahabari kujiuliza kama wanaandika kinachosemwa au wanaandika kinachofanywa, au wanaandika vyote au hawaandiki vyote?
Sambamba na hilo, Joyce Shebe pia ametumia jukwaa hilo kueleza nafasi ya tasnia ya habari katika kipindi cha Serikali ya awamu ya sita (6) chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.