Mhashamu Almachius Rweyongeza apigilia msumari zaidi kwenye waraka wa TEC

Mhashamu Almachius Rweyongeza apigilia msumari zaidi kwenye waraka wa TEC

Kingsmann

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2018
Posts
4,805
Reaction score
17,850
Mhashamu Almachius Vicent Rweyongeza, Askofu wa jimbo katoliki la Kayanga, Karagwe, Kagera amesema "Chaguzi zilizopita zilikua zinakasoro wengi mlipokea Rushwa na mkasimamia hovyohovyo, Bunge likajaa hao wabunge ambao wameanza kubadili sheria ili ziwalinde"

Msikilize kwa dakika 8 akitema madini ikiwemo kukemea vyumbo vya habari vikubwa kutokuripoti kabisa au juujuu waraka wa TEC.

Wahashamu shikilia hapohapo
 
Attachments

  • Screenshot_20230821_112100_WhatsAppBusiness.jpg
    Screenshot_20230821_112100_WhatsAppBusiness.jpg
    39.4 KB · Views: 3
Na pia tusisahau hoja zilizo kiini cha haya yote...

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Siku hizi Tanganyika hakuna tena magazeti, hata yale niliyokuwa nikiyaamini sasa nimegundua hayana maana kabisa.

Ajabu ile kauli ya jana ya kijinga ya JK imeripotiwa na magazeti yote, hapo ndipo utaona hawa wahariri wa siku hizi ni wapuuzi watupu.

Sioni sababu tena ya mtu anayejitambua kununua magazeti nchi hii, vyema waachwe wahariri wayasome na wafanyakazi wao.
 
nyie simnasema roma nikila kitu kumbe hata magazeti yameshindwa kutoa ujumbe wenu.
 
Mhashamu Almachius Vicent Rweyongeza, Askofu wa jimbo katoliki la Kayanga, Karagwe, Kagera amesema "Chaguzi zilizopita zilikua zinakasoro wengi mlipokea Rushwa na mkasimamia hovyohovyo, Bunge likajaa hao wabunge ambao wameanza kubadili sheria ili ziwalinde"

Msikilize kwa dakika 8 akitema madini ikiwemo kukemea vyumbo vya habari vikubwa kutokuripoti kabisa au juujuu waraka wa TEC.

View attachment 2723765

Kwenye hiko kipande kaeleza ukweli. Look at bunge tulilo nalo? So dissapointing
 
Ajabu ni kwamba Mrundi anatetea rasilimali zetu lakini baadhi yetu sisi wenye nchi tukiongozwa na wewe tumekuwa wapumbavu waandamizi.

“Wapumbavu waandamizi” naomba nilichukue hili neno hahahah
 
Mhashamu Almachius Vicent Rweyongeza, Askofu wa jimbo katoliki la Kayanga, Karagwe, Kagera amesema "Chaguzi zilizopita zilikua zinakasoro wengi mlipokea Rushwa na mkasimamia hovyohovyo, Bunge likajaa hao wabunge ambao wameanza kubadili sheria ili ziwalinde"

Msikilize kwa dakika 8 akitema madini ikiwemo kukemea vyumbo vya habari vikubwa kutokuripoti kabisa au juujuu waraka wa TEC.

View attachment 2723765
Alisema hizo kofia zao no Nyekundu kwa sababu wao wamejitoa hadi Kufa ktk kuulinda Ukweli na Haki.

Uhainiiiiiiiii
 
Mhashamu Almachius Vicent Rweyongeza, Askofu wa jimbo katoliki la Kayanga, Karagwe, Kagera amesema "Chaguzi zilizopita zilikua zinakasoro wengi mlipokea Rushwa na mkasimamia hovyohovyo, Bunge likajaa hao wabunge ambao wameanza kubadili sheria ili ziwalinde"

Msikilize kwa dakika 8 akitema madini ikiwemo kukemea vyumbo vya habari vikubwa kutokuripoti kabisa au juujuu waraka wa TEC.

View attachment 2723765
Nchi ina vituko hii sasa huyu Muhutu naye anasema nini.
 
Back
Top Bottom