Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,278
- 797
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametimiza ndoto ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kwa kuweka Jiwe la Msingi la Mradi wa ujenzi wa Bwawa la Umwagiliaji Mkomazi. Mradi huo unatarajiwa kuwanufaisha Wananchi zaidi ya 20,000 Wilayani Korogwe. Mradi huo unatarajia kuimarisha shughuli za kilimo na uzalishaji wa mazao. Rais Dkt Samia amefika kwenye Mradi wa Mkomazi leo tarehe 24 Februari, 2025 ikiwa ni muendelezo wa ziara yake mkoani Tanga.