Mhe. Mbowe, hongera sana. You are the best; ila acha uongo, uzushi na uchochezi. Kati yako na serikali nani mkweli? Vifo ni 16 tu

Mkuu Mungu akusamehe kama unaamua kubisha kwa hili, hata huku mikoani tuna familia zimeshapata hili tatizo ukiachilia makumi ya picha za mazishi mitandaoni. Hiyo hesabu ya marehemu 16 ukiikubali basi utakuwa na tatizo kubwa sana. Vifo ni vingi zaidi ya hiyo hesabu na ukiniuliza ni vingapi sina idadi ila hali si shwari tena na amka sasa. P anajua vizuri sana.
 
Umetoa hoja kuntu
 
Kwa nini tumezwe na fallacies paschal Mayala!

Hili bandiko linaendeleza mawazo ya serikali kuwa kauli zao ni ndiyo pekee na mwisho hata kama si sahihi?

Kazi yako ya uchambuzi na wengine inatakiwa iwe ni kutafuta ukweli daima na ndiyo kazi ya mwanahabari, mwanasheria na mzalendo

Kwangu mzalendo ni yule anayetafuta ukweli na kuutetea huku akiendelea kupinga uongo

Serikali inatafuta iaminike licha ya mashaka yaliyopo hivyo nasi wazalendo labda kama alivyo Mbowe tunaeleza hayo mashaka huku tukiishinikiza serikali ama kuondoa hayo mashaka au kueleza ukweli.
Kwa bahati mbaya ninakokaa hatupati waves za startv hivyo nimekosa hayo mazungumzo ya nyongeza.

Kama unakubaliana na mawazo haya, waombe radhi wazalendo wanaeleza mashaka ya maelezo ya serikali na kutaka ukweli.
 
Kitendo cha kumuita Waziri Mkuu wa JMT kuwa ni muongo na serikali inaficha data za vifo vya Corona, huu ni uongo na uchochezi.
Mimi nadhani Mh mbowe amelizungumzia hili Bungeni, na kama Bunge litahisi mbowe kasema uongo litamtaka atowe ushahidi ili kuthibitisha uongo wa serikali.
Lakini ukiona serikali imeufyata,na bunge limeufyata, na hata hakuchukuliwa hatua ya kuambiwa athibitishe maneno yake ama sivyo afute usemi wake,wote wakaufyata,
Hapa inanipa uoni wa pili ya kwa nini atokee mtu nje ya hapo amwite Mbowe Muongo,na aitetee serikali nje ya bunge?
Hii inanipa wasi wasi ya wale jamaa wa Mapambio wa buku 7 usije ukawa na wewe umo muheshimiwa P
 
Mnafiki mayala katika ubora wake

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Athlete,

Watu wanakufa wapi? Na kwa nini usiandike wewe unataka Pasko aandike?

Hii ni kutafutiana lawama mkuu na ni tabia mbaya sana kutaka kuonekana mzuri na kutaka Fulani mbaya

Maisha yanaendelea
 
Nimesoma comment za wanaufipa nimecheka sana kweli Pasco ni muandishi Bora wale wale waliokuwa wanamuita kila aina ya majina yote mabaya Mara anataka uteuzi Mara njaa sijui anatetea tumbo lake leo wamesahau wanamsifu na kumpamba, tatizo Sasa je wamelielewa bandiko? Au badae watarudi Tena na kufuta comments zao hizi na kuanza kumuita Tena mtaka uteuzi?
 
Athlete,

Watu wanakufa wapi? Na kwa nini usiandike wewe unataka Pasko aandike?

Hii ni kutafutiana lawama mkuu na ni tabia mbaya sana kutaka kuonekana mzuri na kutaka Fulani mbaya

Maisha yanaendelea
Hawa ndio walikuwa wakishabikia upuuzi wa akina Sugu wakutaka raisi atoke azurure mitaani. Leo hao wapiga kelele ndio wamekimbia na kujifungia wakiogopa kufa!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
With due respect Pascal huyu mtu hastahili kusifiwa kwa lo lote. Ni kweli hata saa iliyokufa itaonesha majira sahihi mara mbili ndani ya saa 24. Hii haimaanishi kwamba saa hiyo ni nzima.
 
Pole sana Kwa Kukubali Kupakwa mafuta kwa Mgongo Wa chupa.

Haujamuelewa Pascal.

Sent using Jamii Forums mobile app
Bila shaka kwa wasiomfahamu Paskali (sio Pascal!) ni vigumu kumuelewa. Nikijikumbusha niliyoyasikia ya Uingereza wakati wanatangaza idadi ya vifo vilivyotokana na covid-19, walisisitiza (qaulified) takwimu zile ni za wale wagonjwa/waathirika waliofia katika hospitali ambazo ziko kwenye mtandao wa serikali, na walidokeza, idadi ikawa kubwa zaidi kwani wale ambao watakuwa wamefia kwenye vituo vya kulea wazee na hospitali zisizo katika mfumo wa serikali hawakujumlishwa (yaani idadi yao haikuwa inajulikana. Vivyo hivyo kwa Tanzania! Taarifa ya vifo sio ya uongo- sawa kabisa - shida serikali haiweki angalizo jinsi ilivyopata taarifa zake- inafumbia macho nafasi zingine ambazo vifo vitokanavyo na codiv 19 zinaweza kuwepo kwenye jamii, lakini jinsi ya kuhakiki taarifa hizo ni vigumu.
Mbowe anaposema ni zaidi ya vifo 16, hajakosea - mosi yeye hawajibiki kufanya utafiti wa kisayansi kutoa ushuhuda ni 16 au 16+ au hata 16-! Yeye anapata taarifa kupitia jamii kama mwanasiasa, na hata kama angelazimishwa atoe ushahidi, anaweza kufanya hivyo kwa kuegemea taarifa anazopata, labda abanwe, kama ana hati za vifo za watu hao, ambapo ni vigumu.
Lakini kwa nini yote hayo!
Ni nini tunachojali sasa- what is our focus? Sio kuwaelewesha watanzania ukweli wa makali ya corona ili waongeze jitihada na tahadhari? Tuache kubabiisha kwenye jambo nyeti kama hili!
 
Unaweza ukajifanya umeelewa kumbe wewe ndio kiazi kwelikweli

Navyomsikiliza pasco star TV namaanisha navyosema

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu wewe jiongeze pale kwenye Tv ulifikiri mkuu P angefunguka huru Kama humu JF Kama wakina mwakyembe,polepole kabudi wanayakana machapisho yao sembuse mkuu P,wee fata alichopost humu sio. Kwenye Radio Ccm hio
 
Mbowe na wabunge wa CHADEMA wamekimbia vita, na kwenda kujifungia ndani, hawa sio viongozi, badala ya kuongoza vita vya corona, wamekimbia, october tutawapiga chini wote

[emoji23][emoji23][emoji23] kweli wewe hamna kitu, Meko je yuko wapi?? Kama hii ni vita amiri jeshi mkuu yuko wapi??


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Athlete,

Watu wanakufa wapi? Na kwa nini usiandike wewe unataka Pasko aandike?

Hii ni kutafutiana lawama mkuu na ni tabia mbaya sana kutaka kuonekana mzuri na kutaka Fulani mbaya

Maisha yanaendelea
Mie sina nafasi wala platform aliyo nayo Paskali.
Hatufanani hata kidogo.Nimeandika mengi humu na kwingineko kama ningekuwa na status ya Paskali ningeshasikilizwa na kuisaidia sana nchi.
Kuna tofauti hapo.
Paskali akubali tuu yeye ni tycoon wa media na sasa ni wakati wa kulitumikia taifa kwa mvua kwa jua.Usimtetee akimbie kivuli chake.Paskali taifa linakuhitaji at your best right now,yaani yule Paskali mwwnyewe o.g,msukuma honest na mbishi kukubali kupelekeshwa.Sio kwamba nakuingiza chaka,la hasha,nakupa u..uu.jasiri😂😂 Pascal Mayalla
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…