Mhe. Mbowe, hongera sana. You are the best; ila acha uongo, uzushi na uchochezi. Kati yako na serikali nani mkweli? Vifo ni 16 tu

Mhe. Mbowe, hongera sana. You are the best; ila acha uongo, uzushi na uchochezi. Kati yako na serikali nani mkweli? Vifo ni 16 tu

Mtaani kila anayesema watu wanakufa kwa wingi na kuzikwa usiku,ukimuuliza mtu umeona?anajibu ameambiwa na mtu wake wa karibu,unamuuliza tena labda umefiwa na ndugu au jirani au rafiki huko mikoani hakuna kitu!!! Sisi waTanzania tuna maneo ya uzushi sana bila ukweli wala uhakika wowote,ugonjwa umewekewa siasa na kutengeneza maneno mitandaoni kuweka taharuki kwa watu bila ukweli wowote,inawezekana watu wengine pia waliokua wakisafiri India au London kupigwa sindano na madawa ya gharama juu magonjwa ya moyo,damu na mengineyo wanakufa kwa sababu hakuna safari hizo tena.

JAH Rastafari Morning Africa.Trust JAH respect nature
Mkuu Mungu akusamehe kama unaamua kubisha kwa hili, hata huku mikoani tuna familia zimeshapata hili tatizo ukiachilia makumi ya picha za mazishi mitandaoni. Hiyo hesabu ya marehemu 16 ukiikubali basi utakuwa na tatizo kubwa sana. Vifo ni vingi zaidi ya hiyo hesabu na ukiniuliza ni vingapi sina idadi ila hali si shwari tena na amka sasa. P anajua vizuri sana.
 
Wanabodi,

Miongoni mwa udhaifu mkubwa kabisa wa mainstream media zetu zote za Tanzania, si TV, Redio, wala Magazeti, hatuna kitu kinachoitwa "News Analysis", yaani uchambuzi wa habari, viongozi wetu wakihutubia, media inaripoti wamesema nini, the story ends there! Hakuna any news analysis ya kuchambua alichokisema kiongozi huyo wala what does it mean, the impact ya kilichozungumzwa, na the consequences. Kazi za media zetu ni kuripoti tu kama kasuku. Angalau sisi JF, ndio angalau tunafanya uchambuzi, alichofanya Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Mbowe, ni a very good piece of news analysis ya hotuba ya Rais Magufuli aliyoitoa Ikulu ya Chato na update ya Corona iliyotolewa na Waziri Mkuu.

Mnyonge, mnyongeni, haki yake mpeni. Tangu kuingia kwa janga hili la Corona, sio tu hakuna kiongozi yoyote amewahi kuizungumzia Corona vizuri na kwa ufasaha kama Mhe. Freeman Mbowe, bali pia tangu nimemfahamu Mbowe na kumsikia, hajawahi kuzungumza vizuri hivi hata mara moja. Freeman, you are the best, hongera sana!

Ila sehemu moja tu ndiyo Mbowe ameharibu, kwenye idadi ya vifo vya Corona. Serikali ilishatoa waraka kuwa wasemaji wa update ya Corona kwa Tanzania ni watu 5 tu. Rais, Makamo, Waziri Mkuu na Waziri wa Afya -- then update ya Corona itatolewa na serikali tu. Sasa kama Waziri Mkuu kasema vifo vya Corona ni 16 tu, then huu ndiyo ukweli. Tanzania watu waliokufa kwa Corona mpaka sasa ninapoandika hapa, ni watu 16 tu na huu ndio ukweli wenyewe.

Kitendo cha kumuita Waziri Mkuu wa JMT kuwa ni muongo na serikali inaficha data za vifo vya Corona, huu ni uongo na uchochezi.

Kati ya Mhe. Mbowe na Waziri Mkuu wa JMT, nani ni mkweli na nani ni muongo? Watanzania wamwamini nani kati ya Waziri Mkuu wa JMT na Waziri Mkuu kivuli?

Kama serikali imesema vifo ni 16 tu, then vifo ni 16, hata kama umeshuhudia watu 100 wakizikwa na serikali kwa mazishi ya kuhudhuriwa na watu kumi tu. Ukweli wa idadi ya vifo vya Corona ni vifo 16 tu kwasababu sio kila anayekufa amekufa kwa Corona. Hata kama hao wengine wote nao pia walionesha dalili kama za Corona, mamlaka pekee inayojua mgonjwa kafa na nini, ni madaktari tu. Na kwenye case ya Corona, waliokufa kwa Corona ni watu 16 tu, hawa wengine wote wanaokufa kwa matatizo ya kupumua, hayo ni matatizo yao tu, na pia wagonjwa wa magonjwa mengine pia wanaendelea kufa, ili kuzuia mikusanyiko katika misiba, serikali imeamua kuwakinga watu wake kwa kujitolea kuwasaidia Watanzania wengine wote kwa upendo kwa kuwazikia ndugu na wapendwa wao.

Hivyo Mhe. Mbowe, asante kwa kuongea vizuri ila uache uongo na uchochezi kuisingizia serikali yetu inaficha kitu, serikali yetu ni wakweli, hawafichi kitu, waliokufa kwa Corona mpaka sasa ni hao 16 tu, na huo ndio ukweli wetu, tena ni afadhali ya sisi tumetangaza ukweli wa wote waliokufa kwa Corona nchini kwetu ni hao 16 tu; je, ungekuwa unaishi Rwanda na Uganda, kule hakuna hata mmoja aliyekufa, ungesemaje?

Watanzania wenzangu ambao ni wazalendo, naombeni tuendelee kuiaminia serikali yetu kuwa inasema ukweli wote kuhusu Corona, tusiwasikilize, waongo, wazushi, wachochezi na wachonganishi wanaotaka kuichonganisha serikali na wananchi, kwa kuwadanganya kila anayekufa, amekufa kwa Corona, japo ni kweli vifo vya ghafla vimeongezeka, ila siyo vifo vyote ni Corona. Vifo vingine ni magonjwa mengine ukiwemo matatizo ya kupumua.

Tena katika kusisitiza uzalendo, nitawaomba kuanzia saa 1:30 asubuhi nitakuwa live Star TV mgeni wangu akiwa ni Deodatus Balile wa gazeti la Jamhuri, tutasisitiza uzalendo na kuiaminia serikali na sio kuwaaminia wazushi.

Paskali

Umetoa hoja kuntu
 
Kwa nini tumezwe na fallacies paschal Mayala!

Hili bandiko linaendeleza mawazo ya serikali kuwa kauli zao ni ndiyo pekee na mwisho hata kama si sahihi?

Kazi yako ya uchambuzi na wengine inatakiwa iwe ni kutafuta ukweli daima na ndiyo kazi ya mwanahabari, mwanasheria na mzalendo

Kwangu mzalendo ni yule anayetafuta ukweli na kuutetea huku akiendelea kupinga uongo

Serikali inatafuta iaminike licha ya mashaka yaliyopo hivyo nasi wazalendo labda kama alivyo Mbowe tunaeleza hayo mashaka huku tukiishinikiza serikali ama kuondoa hayo mashaka au kueleza ukweli.
Kwa bahati mbaya ninakokaa hatupati waves za startv hivyo nimekosa hayo mazungumzo ya nyongeza.

Kama unakubaliana na mawazo haya, waombe radhi wazalendo wanaeleza mashaka ya maelezo ya serikali na kutaka ukweli.
 
Kitendo cha kumuita Waziri Mkuu wa JMT kuwa ni muongo na serikali inaficha data za vifo vya Corona, huu ni uongo na uchochezi.
Mimi nadhani Mh mbowe amelizungumzia hili Bungeni, na kama Bunge litahisi mbowe kasema uongo litamtaka atowe ushahidi ili kuthibitisha uongo wa serikali.
Lakini ukiona serikali imeufyata,na bunge limeufyata, na hata hakuchukuliwa hatua ya kuambiwa athibitishe maneno yake ama sivyo afute usemi wake,wote wakaufyata,
Hapa inanipa uoni wa pili ya kwa nini atokee mtu nje ya hapo amwite Mbowe Muongo,na aitetee serikali nje ya bunge?
Hii inanipa wasi wasi ya wale jamaa wa Mapambio wa buku 7 usije ukawa na wewe umo muheshimiwa P
 
Wanabodi,

Miongoni mwa udhaifu mkubwa kabisa wa mainstream media zetu zote za Tanzania, si TV, Redio, wala Magazeti, hatuna kitu kinachoitwa "News Analysis", yaani uchambuzi wa habari, viongozi wetu wakihutubia, media inaripoti wamesema nini, the story ends there! Hakuna any news analysis ya kuchambua alichokisema kiongozi huyo wala what does it mean, the impact ya kilichozungumzwa, na the consequences. Kazi za media zetu ni kuripoti tu kama kasuku. Angalau sisi JF, ndio angalau tunafanya uchambuzi, alichofanya Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Mbowe, ni a very good piece of news analysis ya hotuba ya Rais Magufuli aliyoitoa Ikulu ya Chato na update ya Corona iliyotolewa na Waziri Mkuu.

Mnyonge, mnyongeni, haki yake mpeni. Tangu kuingia kwa janga hili la Corona, sio tu hakuna kiongozi yoyote amewahi kuizungumzia Corona vizuri na kwa ufasaha kama Mhe. Freeman Mbowe, bali pia tangu nimemfahamu Mbowe na kumsikia, hajawahi kuzungumza vizuri hivi hata mara moja. Freeman, you are the best, hongera sana!

Ila sehemu moja tu ndiyo Mbowe ameharibu, kwenye idadi ya vifo vya Corona. Serikali ilishatoa waraka kuwa wasemaji wa update ya Corona kwa Tanzania ni watu 5 tu. Rais, Makamo, Waziri Mkuu na Waziri wa Afya -- then update ya Corona itatolewa na serikali tu. Sasa kama Waziri Mkuu kasema vifo vya Corona ni 16 tu, then huu ndiyo ukweli. Tanzania watu waliokufa kwa Corona mpaka sasa ninapoandika hapa, ni watu 16 tu na huu ndio ukweli wenyewe.

Kitendo cha kumuita Waziri Mkuu wa JMT kuwa ni muongo na serikali inaficha data za vifo vya Corona, huu ni uongo na uchochezi.

Kati ya Mhe. Mbowe na Waziri Mkuu wa JMT, nani ni mkweli na nani ni muongo? Watanzania wamwamini nani kati ya Waziri Mkuu wa JMT na Waziri Mkuu kivuli?

Kama serikali imesema vifo ni 16 tu, then vifo ni 16, hata kama umeshuhudia watu 100 wakizikwa na serikali kwa mazishi ya kuhudhuriwa na watu kumi tu. Ukweli wa idadi ya vifo vya Corona ni vifo 16 tu kwasababu sio kila anayekufa amekufa kwa Corona. Hata kama hao wengine wote nao pia walionesha dalili kama za Corona, mamlaka pekee inayojua mgonjwa kafa na nini, ni madaktari tu. Na kwenye case ya Corona, waliokufa kwa Corona ni watu 16 tu, hawa wengine wote wanaokufa kwa matatizo ya kupumua, hayo ni matatizo yao tu, na pia wagonjwa wa magonjwa mengine pia wanaendelea kufa, ili kuzuia mikusanyiko katika misiba, serikali imeamua kuwakinga watu wake kwa kujitolea kuwasaidia Watanzania wengine wote kwa upendo kwa kuwazikia ndugu na wapendwa wao.

Hivyo Mhe. Mbowe, asante kwa kuongea vizuri ila uache uongo na uchochezi kuisingizia serikali yetu inaficha kitu, serikali yetu ni wakweli, hawafichi kitu, waliokufa kwa Corona mpaka sasa ni hao 16 tu, na huo ndio ukweli wetu, tena ni afadhali ya sisi tumetangaza ukweli wa wote waliokufa kwa Corona nchini kwetu ni hao 16 tu; je, ungekuwa unaishi Rwanda na Uganda, kule hakuna hata mmoja aliyekufa, ungesemaje?

Watanzania wenzangu ambao ni wazalendo, naombeni tuendelee kuiaminia serikali yetu kuwa inasema ukweli wote kuhusu Corona, tusiwasikilize, waongo, wazushi, wachochezi na wachonganishi wanaotaka kuichonganisha serikali na wananchi, kwa kuwadanganya kila anayekufa, amekufa kwa Corona, japo ni kweli vifo vya ghafla vimeongezeka, ila siyo vifo vyote ni Corona. Vifo vingine ni magonjwa mengine ukiwemo matatizo ya kupumua.

Tena katika kusisitiza uzalendo, nitawaomba kuanzia saa 1:30 asubuhi nitakuwa live Star TV mgeni wangu akiwa ni Deodatus Balile wa gazeti la Jamhuri, tutasisitiza uzalendo na kuiaminia serikali na sio kuwaaminia wazushi.

Paskali
Mnafiki mayala katika ubora wake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pasco nimekuelewa unachomaanisha na umekuwa na aina hii ya uandishi wa tafsida kwa muda mrefu sasa.
Nikushauri jambo,kuna mazingira ambayo si busara wala hekima kutumia tafsida kama hizi.
Tuna janga ambalo kila mtu anapaswa straight forward kuonyesha anapambana nalo.
Wewe ni nguli humu,ni Mwandishi maarufu,ni public figure.
Kwa situation tuliyofikia,unapaswa kuweka tafsida zote kando and be straight kile unachosimamia ukielezee kwa uwazi na lugha iliyonyooka.
Imagine kwa status yako kwenye jamii,ukiamua kufuata ushauri huu ukakemea kwa nguvu na kunyoosha lugha kama lile swali ulilouliza siku ile pale Ikulu,impact gani utaleta kwenye jamii?Bila shaka ni kubwa mno.Usiogope vikao vya kuitwa kule naniliu.Watakuita mwisho watachoka.
Na hata kama watakufanya chochote kibaya,basi lile watalokufanyia kitakuwa ni ulimi uzungumzao a thousand times kuliko hata maneno yako.Utakuwa ufa unaobomoa nyumba yao wenyewe watakaokufanyia ubaya.
Be straight Pasco.
Watu wanakufa Pasco.
Hapa tumuambie serikali kwa uwazi tuu bila kuogopa ili atikisike na kuona watanzania wamekunja sura,wanaumia,asipostuka asitulaumu baadae.

Athlete,

Watu wanakufa wapi? Na kwa nini usiandike wewe unataka Pasko aandike?

Hii ni kutafutiana lawama mkuu na ni tabia mbaya sana kutaka kuonekana mzuri na kutaka Fulani mbaya

Maisha yanaendelea
 
Nimesoma comment za wanaufipa nimecheka sana kweli Pasco ni muandishi Bora wale wale waliokuwa wanamuita kila aina ya majina yote mabaya Mara anataka uteuzi Mara njaa sijui anatetea tumbo lake leo wamesahau wanamsifu na kumpamba, tatizo Sasa je wamelielewa bandiko? Au badae watarudi Tena na kufuta comments zao hizi na kuanza kumuita Tena mtaka uteuzi?
 
Athlete,

Watu wanakufa wapi? Na kwa nini usiandike wewe unataka Pasko aandike?

Hii ni kutafutiana lawama mkuu na ni tabia mbaya sana kutaka kuonekana mzuri na kutaka Fulani mbaya

Maisha yanaendelea
Hawa ndio walikuwa wakishabikia upuuzi wa akina Sugu wakutaka raisi atoke azurure mitaani. Leo hao wapiga kelele ndio wamekimbia na kujifungia wakiogopa kufa!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
With due respect Pascal huyu mtu hastahili kusifiwa kwa lo lote. Ni kweli hata saa iliyokufa itaonesha majira sahihi mara mbili ndani ya saa 24. Hii haimaanishi kwamba saa hiyo ni nzima.
 
Pole sana Kwa Kukubali Kupakwa mafuta kwa Mgongo Wa chupa.

Haujamuelewa Pascal.

Sent using Jamii Forums mobile app
Bila shaka kwa wasiomfahamu Paskali (sio Pascal!) ni vigumu kumuelewa. Nikijikumbusha niliyoyasikia ya Uingereza wakati wanatangaza idadi ya vifo vilivyotokana na covid-19, walisisitiza (qaulified) takwimu zile ni za wale wagonjwa/waathirika waliofia katika hospitali ambazo ziko kwenye mtandao wa serikali, na walidokeza, idadi ikawa kubwa zaidi kwani wale ambao watakuwa wamefia kwenye vituo vya kulea wazee na hospitali zisizo katika mfumo wa serikali hawakujumlishwa (yaani idadi yao haikuwa inajulikana. Vivyo hivyo kwa Tanzania! Taarifa ya vifo sio ya uongo- sawa kabisa - shida serikali haiweki angalizo jinsi ilivyopata taarifa zake- inafumbia macho nafasi zingine ambazo vifo vitokanavyo na codiv 19 zinaweza kuwepo kwenye jamii, lakini jinsi ya kuhakiki taarifa hizo ni vigumu.
Mbowe anaposema ni zaidi ya vifo 16, hajakosea - mosi yeye hawajibiki kufanya utafiti wa kisayansi kutoa ushuhuda ni 16 au 16+ au hata 16-! Yeye anapata taarifa kupitia jamii kama mwanasiasa, na hata kama angelazimishwa atoe ushahidi, anaweza kufanya hivyo kwa kuegemea taarifa anazopata, labda abanwe, kama ana hati za vifo za watu hao, ambapo ni vigumu.
Lakini kwa nini yote hayo!
Ni nini tunachojali sasa- what is our focus? Sio kuwaelewesha watanzania ukweli wa makali ya corona ili waongeze jitihada na tahadhari? Tuache kubabiisha kwenye jambo nyeti kama hili!
 
Unaweza ukajifanya umeelewa kumbe wewe ndio kiazi kwelikweli

Navyomsikiliza pasco star TV namaanisha navyosema

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu wewe jiongeze pale kwenye Tv ulifikiri mkuu P angefunguka huru Kama humu JF Kama wakina mwakyembe,polepole kabudi wanayakana machapisho yao sembuse mkuu P,wee fata alichopost humu sio. Kwenye Radio Ccm hio
 
Hawa ndio walikuwa wakishabikia upuuzi wa akina Sugu wakutaka raisi atoke azurure mitaani. Leo hao wapiga kelele ndio wamekimbia na kujifungia wakiogopa kufa!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Stupid people ndio kina chadema
FB_IMG_15881898225185601.jpg
 
Mbowe na wabunge wa CHADEMA wamekimbia vita, na kwenda kujifungia ndani, hawa sio viongozi, badala ya kuongoza vita vya corona, wamekimbia, october tutawapiga chini wote

[emoji23][emoji23][emoji23] kweli wewe hamna kitu, Meko je yuko wapi?? Kama hii ni vita amiri jeshi mkuu yuko wapi??

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Athlete,

Watu wanakufa wapi? Na kwa nini usiandike wewe unataka Pasko aandike?

Hii ni kutafutiana lawama mkuu na ni tabia mbaya sana kutaka kuonekana mzuri na kutaka Fulani mbaya

Maisha yanaendelea
Mie sina nafasi wala platform aliyo nayo Paskali.
Hatufanani hata kidogo.Nimeandika mengi humu na kwingineko kama ningekuwa na status ya Paskali ningeshasikilizwa na kuisaidia sana nchi.
Kuna tofauti hapo.
Paskali akubali tuu yeye ni tycoon wa media na sasa ni wakati wa kulitumikia taifa kwa mvua kwa jua.Usimtetee akimbie kivuli chake.Paskali taifa linakuhitaji at your best right now,yaani yule Paskali mwwnyewe o.g,msukuma honest na mbishi kukubali kupelekeshwa.Sio kwamba nakuingiza chaka,la hasha,nakupa u..uu.jasiri😂😂 Pascal Mayalla
 
Back
Top Bottom