Mhe. Mbowe, hongera sana. You are the best; ila acha uongo, uzushi na uchochezi. Kati yako na serikali nani mkweli? Vifo ni 16 tu

Mhe. Mbowe, hongera sana. You are the best; ila acha uongo, uzushi na uchochezi. Kati yako na serikali nani mkweli? Vifo ni 16 tu

Mbowe na wabunge wa CHADEMA wamekimbia vita, na kwenda kujifungia ndani, hawa sio viongozi, badala ya kuongoza vita vya corona, wamekimbia, october tutawapiga chini wote
Bora yao wanepambana hadi dakika karibia za mwisho. Sasa akiyejificha mapema. Alianza kukimbilia dodoma kwenye mawe hali ikawa mbaya akakimbilia chato nako ugonjwa unemfata. Sijui muda si mrefu mtamsikia yupo kwenye maandaki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Paskali imani yangu ni kuwa lengo lako halikuwa kumsifia Mbowe km ulivyozungumza ktk moja ya aya za bandiko lako bali umelenga kumchongea tu kwa mamlaka zenu juu ya ukweli mchungu alioueleza kwa taarifa zinazofichwa..

Tangu awamu hii ishike kijiti umejitahidi kuiwakilisha vyema na kuipambania kwa hali na mali yako sema imekusahau na kutokuthamini mchango wako.

Amini vifo vya Corona ni vingi km alivyosema Hon Mbowe binafsi nimeshashashuhudia vifo 3 ambavyo havimo ktk idadi yenu ya 16 ndani ya wiki hii moja halafu ss naona mmeamua hadi kutumia idara yetu nyeti ya usalama kuendesha hilo zoezi la usiri..

Anyway tunaishukuru Corona kwa kweli maana imekuwa VERY FAIR yaani ingekuwa mchezaji wa mpira ingepewa sifa za CR7 maana inapiga miguu yote sio km Messi anayetumia shoto tu na mbaya zaidi mpaka sasa upande wenu mnapoteza game na mtapoteza zaidi maana mna wagonjwa wengi ktk nyumba yenu ya Kijani basi mdudu akiingia anabonyeza tu kidoooogo kitu waya...

TUTAELEWANA TU SIKU MOJA

Sent using Jamii Forums mobile app
Sure! Tutaelewana very soon.! Na waendelee kuficha ukweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbowe na wabunge wa CHADEMA wamekimbia vita, na kwenda kujifungia ndani, hawa sio viongozi, badala ya kuongoza vita vya corona, wamekimbia, october tutawapiga chini wote
Hebu tuelezeni MATAGA, kwani huko handaki limeshaandaliwa? Maana nasikia mdudu kaingia na huko!
 
Hata kama umekulia na kuyafurahia maisha ya wale akina Mama mashambenga, kuna wakati jitahidi kuwakilisha hoja zako kama a sensible genuine woman.

Kuna wakati yawezekana unakuwa na hoja nzuri lakini kwa kuwa uwakilishaji wako na lugha unayoitumia ni hovyo, kila unachokichangia kinaonekana kuwa cha hovyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unaonaje ukiachana nazo Tu ukasepa.

Ushambega ni jadi yangu. Kumbuka hilo.

Vipi mama'ko kakulia vipi?
 
Wanabodi,

Miongoni mwa udhaifu mkubwa kabisa wa mainstream media zetu zote za Tanzania, si TV, Redio, wala Magazeti, hatuna kitu kinachoitwa "News Analysis", yaani uchambuzi wa habari, viongozi wetu wakihutubia, media inaripoti wamesema nini, the story ends there! Hakuna any news analysis ya kuchambua alichokisema kiongozi huyo wala what does it mean, the impact ya kilichozungumzwa, na the consequences. Kazi za media zetu ni kuripoti tu kama kasuku. Angalau sisi JF, ndio angalau tunafanya uchambuzi, alichofanya Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Mbowe, ni a very good piece of news analysis ya hotuba ya Rais Magufuli aliyoitoa Ikulu ya Chato na update ya Corona iliyotolewa na Waziri Mkuu.




Mnyonge, mnyongeni, haki yake mpeni. Tangu kuingia kwa janga hili la Corona, sio tu hakuna kiongozi yoyote amewahi kuizungumzia Corona vizuri na kwa ufasaha kama Mhe. Freeman Mbowe, bali pia tangu nimemfahamu Mbowe na kumsikia, hajawahi kuzungumza vizuri hivi hata mara moja. Freeman, you are the best, hongera sana!

Ila sehemu moja tu ndiyo Mbowe ameharibu, kwenye idadi ya vifo vya Corona. Serikali ilishatoa waraka kuwa wasemaji wa update ya Corona kwa Tanzania ni watu 5 tu. Rais, Makamo, Waziri Mkuu na Waziri wa Afya -- then update ya Corona itatolewa na serikali tu. Sasa kama Waziri Mkuu kasema vifo vya Corona ni 16 tu, then huu ndiyo ukweli. Tanzania watu waliokufa kwa Corona mpaka sasa ninapoandika hapa, ni watu 16 tu na huu ndio ukweli wenyewe.

Kitendo cha kumuita Waziri Mkuu wa JMT kuwa ni muongo na serikali inaficha data za vifo vya Corona, huu ni uongo na uchochezi.

Kati ya Mhe. Mbowe na Waziri Mkuu wa JMT, nani ni mkweli na nani ni muongo? Watanzania wamwamini nani kati ya Waziri Mkuu wa JMT na Waziri Mkuu kivuli?

Kama serikali imesema vifo ni 16 tu, then vifo ni 16, hata kama umeshuhudia watu 100 wakizikwa na serikali kwa mazishi ya kuhudhuriwa na watu kumi tu. Ukweli wa idadi ya vifo vya Corona ni vifo 16 tu kwasababu sio kila anayekufa amekufa kwa Corona. Hata kama hao wengine wote nao pia walionesha dalili kama za Corona, mamlaka pekee inayojua mgonjwa kafa na nini, ni madaktari tu. Na kwenye case ya Corona, waliokufa kwa Corona ni watu 16 tu, hawa wengine wote wanaokufa kwa matatizo ya kupumua, hayo ni matatizo yao tu, na pia wagonjwa wa magonjwa mengine pia wanaendelea kufa, ili kuzuia mikusanyiko katika misiba, serikali imeamua kuwakinga watu wake kwa kujitolea kuwasaidia Watanzania wengine wote kwa upendo kwa kuwazikia ndugu na wapendwa wao.

Hivyo Mhe. Mbowe, asante kwa kuongea vizuri ila uache uongo na uchochezi kuisingizia serikali yetu inaficha kitu, serikali yetu ni wakweli, hawafichi kitu, waliokufa kwa Corona mpaka sasa ni hao 16 tu, na huo ndio ukweli wetu, tena ni afadhali ya sisi tumetangaza ukweli wa wote waliokufa kwa Corona nchini kwetu ni hao 16 tu; je, ungekuwa unaishi Rwanda na Uganda, kule hakuna hata mmoja aliyekufa, ungesemaje?

Watanzania wenzangu ambao ni wazalendo, naombeni tuendelee kuiaminia serikali yetu kuwa inasema ukweli wote kuhusu Corona, tusiwasikilize, waongo, wazushi, wachochezi na wachonganishi wanaotaka kuichonganisha serikali na wananchi, kwa kuwadanganya kila anayekufa, amekufa kwa Corona, japo ni kweli vifo vya ghafla vimeongezeka, ila siyo vifo vyote ni Corona. Vifo vingine ni magonjwa mengine ukiwemo matatizo ya kupumua.

Tena katika kusisitiza uzalendo, nitawaomba kuanzia saa 1:30 asubuhi nitakuwa live Star TV mgeni wangu akiwa ni Deodatus Balile wa gazeti la Jamhuri, tutasisitiza uzalendo na kuiaminia serikali na sio kuwaaminia wazushi.

Paskali
Wewe mpaka uzike ndugu yako au likupate mwenyewe ndio utajua hujui. Endelea kutetea tumbo lako.
 
Huyu mayalla mjinga sana,Siku hizi amepewa timu Lumumba kabla hajatoa post wako mkao Wa kumsapoti punde anapo post,hivi mayalla pamoja na uandishi wako uchwara unaamini hizo talwimu za pm na wizara ya afya,subirini soon mtaumbuka..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, i was told you are a lawyer, some one with necessary skills to comprehend, analyse and defend issues ,but i am so disappointed. Uzi wako ni reflection of what you are, a boot licker, unainajisi legal profession na kuwa mfano wa watu waliosoma wakashindwa kuelimika.

Wewe haufanani na mtu anaye jenga hoja kwamba serikali ndiyo ya kuaminiwa zaidi na kwamba matamko ya viongozi ndiyo ukweli? Mkuu, hapa unainyanyua serikali na kuipa nguvu za ki-Mungu, kwamba watu wasihoji ukweli na usahihi wa taarifa zake, kweli? Hivi ndivyo vijana wetu wamefundishwa namna ya kutafakari?

Serikali inaweza ikawa sahihi au isiwe sahihi lakini kama inafanya jambo kwa maslahi ya umma wananchi baada ya kuelimishwa wataielewa. Katika jambo hili la corona viongozi wa upinzani hawaoni serikali ikijipambanua na kuchukua hatua ambazo jamii inatarajia. Ni haki yao ya kikatiba kuhoji na kupata majibu.

Ikumbukwe kwamba serikali imewekwa na wananchi na inatumia pesa za wananchi kuendesha shughuli zake, hivyo ni haki ya wananchi kuhoji na huu ni moja ya msingi wa utawala bora.

Namalizia kwa nasihi zifuatazo:

1. Kwenye ukweli uongo hujitenga; na
2. Ukweli utakuweka huru.
Is he really a lawyer? What an insult to his profession!!!? Siamini kama 'lawyer' ndo kaandika hivi. Hata wanaoabudu wanapewa muda wa kutafakari. Huyu jamaa anawaabudu viongozi bila hata kutafakari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom