Mhe. Nimrod Mkono asaini kumwondoa waziri Mkuu!

Mhe. Nimrod Mkono asaini kumwondoa waziri Mkuu!

Mjumbe wa NEC CCM na mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Ndugu Nimrodi Mkono muda huu amesaini waraka ambao utapelekwa Bungeni kesho kuhusu kura ya kutokuwa na Imani na Waziri Mkuu.

Huyu amekuwa Mbunge mwingine miongoni mwa wabunge wa CCM ambao wameamua kuusaini waraka huo kabla ya kuwasilishwa Bungeni kesho siku ya jumatatu.

Huyu ni mjumbe wa NEC ya CCM , tafsiri ya jambo hili nini maana yake .....

UPDATE:

Amesema kuwa yeye ni mbunge wa NEC (ya CCM) wa kuchaguliwa na wabunge na wabunge ndio wanalalamika hivyo hawezi kukaa kimya nchi ikiwa inapotea!

Sawali:

Kama wabunge wanaendelea na movement hii wananchi tunafanya nini, upepo hautakiwi uvume tu, kimbunga je
 
Mkuu hivi hunajua kiasi alichokuwa analipwa Mkono na Daudi Balali.

Mkono and Company Advocates walilipwa dola 998,000 (Sh 1.3 bilioni) halafu bado unamuona ni fisadi mdogo kisa kasaini.
Mkuu sijasema ni fisadi mdogo (nimesema kama signature itasaidia kupata bigger fisadis) maana yake ni kwamba either wakubwa kuliko yeye au genge kubwa zaidi...

Kumbuka kusaini kwake hakumfutii kesho kutupwa lupango, kumbuka hapa Zitto hatafuti signature za watu wasafi bali signature za wabunge 70 ili kuondoa uozo, (yaani nina uhakika hata signature ya Pinda is welcomed)...
ritz kumbuka mimi sioni ushujaa wowote wa mtu yoyote kusign (sababu moja inaweza ikawa motive ya kujisafisha hata kama hawana motive they are just doing their jobs after taking our (tax) Poshos for so long..., this is the least these Prima Donas can do...

Na hata baada ya hizo signatures watakuwa bado hawajashinda any battle let alone the war... (Vita vitashindika siku CCM ikiwa buried and all those lunatics are in Jail)
 
Last edited by a moderator:
Hongera Mhe Nimrod Mkono kwa kusahini Chadema wamekusafisha rasmi na wamekutoa kwenye orodha yao ya List of shime.
Jamani jamani Jamani, ni heri uandike kimatumbi ulichozowea kuliko kuivamia Lugha ya Malkia.
 
Yes,kuna kazi.Hata mafisadi sasa wanageukana.Kama yuko upande wetu ni ndugu yetu.Karibu Mkono ila usitugeuke tena.Maana ulituibia kweli Bank kuu.
Mjumbe wa NEC CCM na mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Ndugu Nimrodi Mkono muda huu amesaini waraka ambao utapelekwa Bungeni kesho kuhusu kura ya kutokuwa na Imani na Waziri Mkuu.

Huyu amekuwa Mbunge mwingine miongoni mwa wabunge wa CCM ambao wameamua kuusaini waraka huo kabla ya kuwasilishwa Bungeni kesho siku ya jumatatu.

Huyu ni mjumbe wa NEC ya CCM , tafsiri ya jambo hili nini maana yake .....

UPDATE:

Amesema kuwa yeye ni mbunge wa NEC (ya CCM) wa kuchaguliwa na wabunge na wabunge ndio wanalalamika hivyo hawezi kukaa kimya nchi ikiwa inapotea!
 
Zittokabwe #Mkono ameamua kuwa upande sahihi wa historia na atawatoa woga wabunge wengi sana. Picha na sababu zake mtapata kesho
 
Last edited by a moderator:
Ingawa Mkono si msafi, nampongeza kwa kuweka politics on the side na kuweka maslahi ya taifa mbele. Naon amesoma alama za nyakati.

On my opinion naona hili swala lina mkono wa JK, kwani ameona hakubaliki na sasa akaona ni bora akimaliza kipindi chake amalize na CCM yake(meaning iondoke madarakani).

Ukiangaliz teuzi alizofanya resently, za kina Lubuva, Sefue nk utaona ameamua kubadilika. In this move ni yeye somehow kaparticipate, kafanya hii akijua kabisa atakuwa nje ya nchi. Sefue wiki nzima alikuwa Dodoma akiongea na wabunge na kufacilitate then amerudi nchini na takayosema ni kwamba wananchi wamechoka na wabunge wamechoka ngoja tuwape what they want; having that said I'm pretty sure kesho mambo yanabadilika.

Change is coming.
 
Who is Mkono anyway? Does he even talk?

I can swear I don't remember when I last heard him talk in parliament let alone sponsor any kind of significant piece of legislation.
Mbunge gani unaemjua wewe amewahi ku "sponsor any piece of legislation" in modern history?

Mnatumia vi concept vya kigeni ambavyo havipo kwenye bunge la Tanzania!


Mkono kwa kutia sahihi list hii ametuonyesha kwamba hii movement inakubalika na wabunge wa upinzani na wa CCM,wenye uzoefu na connections tofauti.
Mkono sio CCM wa kwanza ku saini huu waraka! Na CCM ambao wameshasaini wana "uzoefu na connections tofauti" vile vile. Sasa kwa nini yeye akisaini ndio iwe nongwa ya "hii ametuonyesha kwamba hii movement inakubalika" ?? Usimweke Mkono kwenye pedestal bila sababu.
 
Mbunge gani unaemjua wewe amewahi ku "sponsor any piece of legislation" in modern history?

Mnatumia vi concept vya kigeni ambavyo havipo kwenye bunge la Tanzania!


Mkono sio CCM wa kwanza ku saini huu waraka! Na CCM ambao wameshasaini wana "uzoefu na connections tofauti" vile vile. Sasa kwa nini yeye akisaini ndio iwe nongwa ya "hii ametuonyesha kwamba hii movement inakubalika" ?? Usimweke Mkono kwenye pedestal bila sababu.

CCM wengine waliosaini kabla ya Mkono wenye gravita na powerbrokering swashbuckle of a Mkono ni kina nani?
 
Hii nchi bwana inanipa raha sana..yaaani kesho bunge litawaka moto!! Pinda kama ana akili ni kuondoka tu ukapalilie mahindi yako huko katavi maana unapenda sana kulima..
 
Mkuu ritz unajua JF ni tajiri wa kumbukumbu. Tukifukua thread zinazomhusu huyu mzee mtashangaa alivyokuwa akibezwa na kutukanwa kama fisadi wa lile kundi la thenashara lakini leo ni shujaa ambaye halilii bunduki! Watz huwa tunadanganywa kwa khanga, kofia, vitenge, shaba (pilau) na vitu vingine vidogo vidogo. Hii ya Mkono kusaini ni sawa na pilau tu kwa wale waliokuwa wakimuita fisadi ila leo wanamuita shujaa!

Si kweli na wala si sahihi kwamba Mkono kuweka mkono wake kwenye orodha ya wabunge wanaotaka Waziri Mkuu akimbizwe kunamuondolea cheo cha ufisadi. Wanachothamini wachangiaji, ni dhamira yake ya kushughulikia tatizo lililopo sasa. Waswahili wanasema "Kafiri akufaaye si islam asiyekufaa." Tena wakaongeza kuwa "Baniani m-baya kiatu chake dawa" Hivyo hata kama wako watakatifu miongoni mwa CCM na vyama vingine (UDP) ambao hawawezi kuangusha saini zao kwenye waraka hao ni islam wasiotufaa katika hili na kafiri Mkono ni heri kuliko wao. Japo kiatu chake ni dawa baniani huyu hageuki kuwa mzuri bado anaitwa baniani m-baya (aka fisadi).
Ni dhahiri kuwa islam yeyote atashangaa sana kusaidiwa na kafiri wakati islam mwenzake (mwenye uwezo wa kufanya hivyo)akimkodolea macho. Si ajabu basi ukamwona islam huyu akimsifu kafiri kwa kumfaa siku ya dhiki yake. Hilo ndilo linalotokea; wako wapi islam wa CCM katika hili. Kwa vile hawakufaa heri kafiri anayefaa (na ukafiri wake) yaani Mkono.
 
CCM wengine waliosaini kabla ya Mkono wenye gravita na powerbrokering swashbuckle of a Mkono ni kina nani?
Mkono hana "gravitas" wala "power brokering swashbuckle" yeyote!

Amewahi kum power broker nani????

Wewe mwenyewe umesema Mkono ana madhambi "yasiyokomboleka"! Kwenye jamii mtu mwenye madhambi yasiyokomboleka hana "gravitas"! Unajua maana ya gravitas we mja wa Kilwa Pande wewe? Ni mtu aliye na utukuka, heshima kwenye jamii, umakini, umuhimu, taadhima, sio mtu mtu tu almuradi tajiri na mali zake! Mfano, Salim Ahmed Salim, Ally Hassan Mwinyi, Waziri Mwandosya n.k. Mkono yuko kwenye buku jeusi la Mwembeyanga Kumi na Moja, hana gravitas!

Mwana CCM hapa mwenye bellwether influence and deserving of applause ni aliyeanzisha noma lote hili, Deo Filikunjombe. Bila Filikunjombe Zitto asingepata wherewithal wala inclination ya kukusanya saini!
 
Unajua mapaka sasa watu hawajaifahamu zaidi CDM. Wanaikurupukia tu. Tuna mikakati ya kuanika all about CDM. Stay tunned!

....Kwamba CDM ni chama cha wachaga na wakristo (ukabila na udini)....Dr Slaa kachukua mke wa mtu, Dr Slaa kampa mimba mke wa mtu, Dr Slaa upadri ulimshinda kwa kuwa alikuwa mzinzi na pia alifanya ufisadi wa kuondoka na bulungutu kubwa, Dr Slaa anataka kuanzisha umwagaji damu nchini.....Blah blah zenu Watanzania tumeshazistukia na ndio sababu kubwa Dr Slaa anachanja mbuga na kusababisha wimbi kubwa la wanachama wa magamba kurudisha kadi ili kujiunga na CDM. People's................

Alutta Continua

 
Back
Top Bottom