Mhe. Nimrod Mkono asaini kumwondoa waziri Mkuu!

Mhe. Nimrod Mkono asaini kumwondoa waziri Mkuu!

Watanzania ni watu wa matukio sana baada ya hapo uwa wanayasahau yote.

Katika orodha ya Slaa aliyoitaja pale Mwembe Yanga Temeke Nimrod Mkono alikuwemo.

Leo baada ya kusaini amekuwa shujaa na kwenye kundi la ufisadi hayumo tena.

Mkuu ritz unajua JF ni tajiri wa kumbukumbu. Tukifukua thread zinazomhusu huyu mzee mtashangaa alivyokuwa akibezwa na kutukanwa kama fisadi wa lile kundi la thenashara lakini leo ni shujaa ambaye halilii bunduki! Watz huwa tunadanganywa kwa khanga, kofia, vitenge, shaba (pilau) na vitu vingine vidogo vidogo. Hii ya Mkono kusaini ni sawa na pilau tu kwa wale waliokuwa wakimuita fisadi ila leo wanamuita shujaa!
 
Last edited by a moderator:
Akitia sign Lowasa hapo,zitto atapewa majina mapya.
"Kanunuliwa ashafishe mafisadi kwa kuwaita wazalendo"

Ubinadamu kazi kweli kweli.
 
Kuishi kwingi ni kuona mengi, lakini pia ukistaajabu ya Musa inakuwaje...
 
Mkono is nothing than a very smart guy. Kwa kutiani saini anajua kuwa jina lake litasafishika. lakini on the other hand anajua kuwa Magamba hawataafiki kupiga kura ya no confidence kwa Mtoto Fake wa Mkulima kwa maana wote ni Wachumia tumbo and they dont know what will be the next course of action.

As you can see, mmeshaanza kumuona Mkono shujaa while in fact ni one of Top Fisadiz. The guy knows mathematics.

Kilichopo hapa ni Kugangamaa na hoja na kama Bi Kiroboto akiizima, the next stage iwe ni Mkakati wa Kumwondoa yeye Bi. Kiroboto kwa kutumia Kanuni.

Nadhani unapoanza vita unakuwa na adui mmoja ili ushinde na Zitto analifahamu hilo. Kwa sasa mission yake ni kukusanya saini hata Pinda akitaka kusaini atampa asaini. Kumbuka hoja ikipita utahitaji kura zao wote ili kumtoa, ukianza kuwabagua sasa hivi utashindwa. Ukisha shinda ndio unaanza kufuatilia na maovu ya nyuma ya wale wale waliokusaidia kushinda.
Mkuu hapo kwenye blue unahitaji kurefresh your memory.
Huitaji kura za wabunge wote ili kumtoa bali 50% ya kura za wabunge wote plus 1
 
Mkuu once a Fisadi always a Fisadi...

Hii ni means to a end kama signature yake itatumika kumuondoa a Bigger Fisadi.., Who Cares...

Brick by Brick..., Brick by Brick my friend, Rome was not built in one day...

Mkuu hivi hunajua kiasi alichokuwa analipwa Mkono na Daudi Balali.

Mkono and Company Advocates walilipwa dola 998,000 (Sh 1.3 bilioni) halafu bado unamuona ni fisadi mdogo kisa kasaini.
 
Ndahani pitia hii thread pal... Then you will atleast get an idea ya why am
curious ni wana CCM wangapi/wepi wana sign hii kitu... Nothing personal - it is politics..

Haaahaa! True nothing personal...ni interest za nchi yetu tu ndo zinatusukuma kujua nani kafanya nini. Well, sutashangaa maana kusema ukweli ni kama watu wamechoka na huu uzembe na kutowajibika. Sishangai kabisa saini za mtu kama huyu....
 
red-arrows-set-down-clip-art.jpg




97988476.JPG
 
Watz huwa tunadanganywa kwa khanga, kofia, vitenge, shaba (pilau) na vitu vingine vidogo vidogo. Hii ya Mkono kusaini ni sawa na pilau tu kwa wale waliokuwa wakimuita fisadi ila leo wanamuita shujaa!

Quote of the day!!!!
 
Kuna ukungu ... sioni vizuri. Ngoja tupumzike kwa masaa 12 tuone kama patapambazuka na kuleta nuru zaidi... Ila Mkono ni mzalendo sana, lakini anajuwa kutengeneza pesa kwa kutumia sheria. Hatua ya yeye kuweka sign yake kwenye mkakati wa kuiwekea shinikizo serikali ni kipimo cha uelewa na uzalendo wake. Ndani ya CCM weeeeengi sana sasa hivi wameasi kimyakimya. Ngojea ukungu upunguwe kwanza ...
 
Wako wapi waliojipachika jina la makamanda wa ufisadi kutoka CCM?Wapi Sitta,Mwakyembe,kilango,sendeka etc?
 
Ujumbe wa Nec ya CCM, utaisha mwaka huu.

Yeye ni mmoja wa wajumbe wa NEC waliochaguliwa kuwawakilisha wabunge wa CCM kwa kipindi cha 2010 -2015. Kwa hiyo amechaguliwa mwaka jana, ujumbe wake unadumu mpaka September 2015 Bunge litakapokuwa vunjwa.
 
Viongozi wa Tanzania wanapenda kung'ang'ania madaraka kana kwamba uhai wao unategemea kubaki kwo kwenye viti walivyo vikalia. Whatever the outcome Pinda kasha aibika sana na kama angekua mtu wa kuona mbali ili kutunza legacy yake angejiuzulu mwenyewe. Tatizo viongozi wa Afrika hawapendi neno "kuwajibika" na wana ng'ang'ania viti to the point mtu ana baki na cheo lakini heshima yote kwisha.
 
vp wamefikia wabunge wangap waliotia sain zao kwenye form?, coz had jana walifikia 73.
 
wabunge wengine 3 waliosaini toka ccm watatangazwa kesho
 
Mkuu ritz unajua JF ni tajiri wa kumbukumbu. Tukifukua thread zinazomhusu huyu mzee mtashangaa alivyokuwa akibezwa na kutukanwa kama fisadi wa lile kundi la thenashara lakini leo ni shujaa ambaye halilii bunduki! Watz huwa tunadanganywa kwa khanga, kofia, vitenge, shaba (pilau) na vitu vingine vidogo vidogo. Hii ya Mkono kusaini ni sawa na pilau tu kwa wale waliokuwa wakimuita fisadi ila leo wanamuita shujaa!
Mkuu Kimbunga nakubaliana kwa kiasi fulani na maoni yako lakini pili natofautiana nawe kidogo,tukiwa tunaelekea mwisho wa enzi ya CCM kuna mambo mengi yatasikika ktk hali ya kawaida wengi hawataamini,lakini ni lazima yatokee! Kutakua na mikataba ya siri ambayo itafanyika kulinda baadhi ya watu,hiyo yote itakua kuiepusha nchi na umwagaji wa damu!
 
Last edited by a moderator:
Hivi kwa nini mnafuta baadhi ya mabandiko yangu nyie watawala?

Kwa nini lakini? Mnashangaza sana nyie watu.

HIVI RAISI YEYE PERFOMANCE YAKE VIPI?

AU YEYE ANAANGUSHWA NA WASAIDIZI WAKE?
 
Back
Top Bottom