Mhe. Nimrod Mkono asaini kumwondoa waziri Mkuu!

Mhe. Nimrod Mkono asaini kumwondoa waziri Mkuu!

Unajua mapaka sasa watu hawajaifahamu zaidi CDM. Wanaikurupukia tu. Tuna mikakati ya kuanika all about CDM. Stay tunned!

Don't you think it is a bit too late. The ship has left the shore and whatever you guys throw at CDM will do no harm.
 
Mkono hana "gravitas" wala "power brokering swashbuckle" yeyote!

Amewahi kum power broker nani????

Wewe mwenyewe umesema Mkono ana madhambi "yasiyokomboleka"! Kwenye jamii mtu mwenye madhambi yasiyokomboleka hana "gravitas"! Unajua maana ya gravitas we mja wa Kilwa Pande wewe? Ni mtu aliye na utukuka, heshima kwenye jamii, umakini, umuhimu, taadhima, sio mtu mtu tu almuradi tajiri na mali zake! Mfano, Salim Ahmed Salim, Ally Hassan Mwinyi, Waziri Mwandosya n.k. Mkono yuko kwenye buku jeusi la Mwembeyanga Kumi na Moja, hana gravitas!

Mwana CCM hapa mwenye bellwether influence and deserving of applause ni aliyeanzisha noma lote hili, Deo Filikunjombe. Bila Filikunjombe Zitto asingepata wherewithal wala inclination ya kukusanya saini!

Gravita ni umuhimu, hata character ya shetani ina gravita, as in umuhimu. Kwa kuwa inawavuta watu kwenye mabaya. Gravita = gravity, sasa usitake ku limit gravita kwa definition ya kwanza tu ya integrity.

Katika chama kilichojaa ufisadi, fisadi mkubwa kabisa ndiye mwenye gravita kuliko hao kina Filikunjombe, Salim na Mwandosya ambao nao si mali kitu. Wamejaa rushwa na woga wote tu.

Ukijua kusoma utaona sijatoa applause popote, nimestate.
 
lengo la kikwete ni kumuondoa pinda hapo kitini..

I aggree with you, na ndio maana anawaacha wale 8fish ili Hasira ya wananchi na wabunge isipoe! I wish tungemgeuzia kibao YEYE!
 
Kama Nimrodi naye kaungana na hii movement, basi nadhani huenda kuna ajenda ya siri inayotaka kupitishwa kwa kutumia kivuli cha skendo hii. Nimrodi hawezi kuwa na uchungu sana na nchi hii ilhali yeye ndiye aliyekuwa mmoja wa vinara walioidhulumu sana nchi hii kwa njia mbalimbali, na alikuwa grupu moja na Lowasa, Chenge, na Rostam wakisistiza kuwa CCM kiwe ni chama cha wakulima, wafanyakazi na wafanyabiashara wakubwa.
 
lengo la kikwete ni kumuondoa pinda hapo kitini..

Ni kweli, inaonekana wazi kuwa Kikwete hamtaki Pinda katika nafasi ile, ila kwa vile yeye mwenyewe hana confidence ya kumtoa hapo kitini, ndiyo maana ya masuguano huo. Ningekuwa Pinda, ningejiondoa kimya kimya tu. Kuibuka kwa Nimrodi kusaini hoja ya Zito ni wazi kuwa Lowasa naye anafurahia sakata hilo na angependa zipatikane sahihi nyingi tu. Swali kubwa lisilojulikana ni iwapo Kikwete anataka kumrudisha Lowasa katika nafasi ile kwa ajili ya kumwandaa kwa 2015.
 
M4C Huyu ahesabiwe kuwa ni shujaaa wa mabadiliko. Apewe heshima na wananchi kama shujaa. Wengine wote wanasubiri kuzomewa wakirudi majimboni.
 
Mkuu Kimbunga nakubaliana kwa kiasi fulani na maoni yako lakini pili natofautiana nawe kidogo,tukiwa tunaelekea mwisho wa enzi ya CCM kuna mambo mengi yatasikika ktk hali ya kawaida wengi hawataamini,lakini ni lazima yatokee! Kutakua na mikataba ya siri ambayo itafanyika kulinda baadhi ya watu,hiyo yote itakua kuiepusha nchi na umwagaji wa damu!

Mkuu timbilimu mikataba ya siri ya kulindana tena? Nchi itamwagaji damu wakati wa kushughulikia mafisadi?
 
Last edited by a moderator:
Si kweli na wala si sahihi kwamba Mkono kuweka mkono wake kwenye orodha ya wabunge wanaotaka Waziri Mkuu akimbizwe kunamuondolea cheo cha ufisadi. Wanachothamini wachangiaji, ni dhamira yake ya kushughulikia tatizo lililopo sasa. Waswahili wanasema "Kafiri akufaaye si islam asiyekufaa." Tena wakaongeza kuwa "Baniani m-baya kiatu chake dawa" Hivyo hata kama wako watakatifu miongoni mwa CCM na vyama vingine (UDP) ambao hawawezi kuangusha saini zao kwenye waraka hao ni islam wasiotufaa katika hili na kafiri Mkono ni heri kuliko wao. Japo kiatu chake ni dawa baniani huyu hageuki kuwa mzuri bado anaitwa baniani m-baya (aka fisadi).
Ni dhahiri kuwa islam yeyote atashangaa sana kusaidiwa na kafiri wakati islam mwenzake (mwenye uwezo wa kufanya hivyo)akimkodolea macho. Si ajabu basi ukamwona islam huyu akimsifu kafiri kwa kumfaa siku ya dhiki yake. Hilo ndilo linalotokea; wako wapi islam wa CCM katika hili. Kwa vile hawakufaa heri kafiri anayefaa (na ukafiri wake) yaani Mkono.
Mkuu Dawa ya Mjinga tatizo ni yeye kuonekana shujaa kwa kuwapa pilau waliokuwa wakimuita fisadi. Fisadi ni fisadi tu hata kama atapiga kura ya wazi ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu acha kusaini peke yake.
 
Last edited by a moderator:
Huyu mbuge sianawakilisha jimbo la marehemu baba wa taifa? Kama ndivyo basi kuna jambo.
 
Pinda alitakiwa hadi leo awe ameandika barua ya kumwaga manyanga. pinda unangoja nn.
 
Kumbe Ole Sendeka na Anna Kilango-Malecela wanaunga mkono ufisadi. Siwaamini tena!
 
Unajua mapaka sasa watu hawajaifahamu zaidi CDM. Wanaikurupukia tu. Tuna mikakati ya kuanika all about CDM. Stay tunned!

Kwa bahati mbaya kila mki ibuka na Kombora la kuipiga CDM linawageukia nyie wenyewe! Chanzo cha matatizo ya CCM sii CDM. Mchawi wenu yumo humo humo kwenu! Ushauri wa bure: Clean your house first before you start making any fuss about CDM.
 
Where is Rejao, Ritz & Co? Sijawaona tangu hili vuguvugu la kura 70 zianze!

Actually, wateteaji wengi CCM humu ndani wameingia mitini siku hizi, kama vile Mwita25, Faiza Foxy n.k. Kulikoni???
 
"Watu wenye mawazo tofauti, hata wakiwa wachache, lazima wawe na haki ya kutoa mawazo yao katika majadiliano bila ya hofu ya kusumbuliwa; mawazo yao na yashindwe katika hoja za majadiliano, siyo kwa vitisho au mabavu" - J. K. Nyerere.

Hongera wabunge wachache wa CCM kwa kuweka maslahi ya taifa mbele kwa kusaini kutokuwa na Imani na WM.
 
Kumbe Ole Sendeka na Anna Kilango-Malecela wanaunga mkono ufisadi. Siwaamini tena!
Wote ni maslahi binafsi, kupata nafasi ya kutafuna nchi.
Hata ndoa yake na Mzee Tingatinga ililenga kuwa first lady ajianzishie biashara ikulu kama che nkapa
 
Waraka wa Zitto ndio uwe mwongozo wa upigaji kura 2015. Yeyote asiyesaini OUT!
 
Gravita ni umuhimu, hata character ya shetani ina gravita, as in umuhimu. Kwa kuwa inawavuta watu kwenye mabaya. Gravita = gravity, sasa usitake ku limit gravita kwa definition ya kwanza tu ya integrity.

Katika chama kilichojaa ufisadi, fisadi mkubwa kabisa ndiye mwenye gravita kuliko hao kina Filikunjombe, Salim na Mwandosya ambao nao si mali kitu. Wamejaa rushwa na woga wote tu.

Ukijua kusoma utaona sijatoa applause popote, nimestate.

Agreed except for the red part, which for me it was not necessary!
 
lengo la kikwete ni kumuondoa pinda hapo kitini..

Hilo sio lengo lake hasa ila analazimika kufanya hivyo. Kikwete ana tabia ya kuwabebesha mizigo yake wasaidizi wake, alifanya hivyo kwa Lowasa wakati wa Richmond, sasa atafanya hivyo kwa Pinda. Kimsingi dili hizi zinamhusu yeye mwenyewe, Lowasa kesha eleza, tusubiri Pinda naye akibinuka, naye ataeleza...

Suala kubwa hapa ni kwamba, its time now for Kikwete and his government to go!
 
Back
Top Bottom