Mhe. Tundu Lissu, Please Acha Kumsulubu Spika Wetu! Unammaliza Kabisa Hadi Ameshindwa Kazi!

Aisee!!!sentensi yako ya mwisho umenimaliza.ngoja niseme hivi si vyema CCM kuendelea kulipeleka bunge kishabiki na kuuona upinzani hauna lolote bungeni,watanzania wanaona hoja toka upande wa pili jinsi wabunge 40 +wanavyoweza kuwatoa kamasi wabunge 300+ wa chama tawala na spika wao,CCM wanajua na walijua kuwa makinda hana uwezo ila walimchagua kishabiki wakidhani wanamkomoa SITTA,mbona sioni wakienda kumsaidia kujibu maswali ya akina MNYIKA,LISSU NA WENGINE???.
 
Mkuu pasco heshima kwako vijana wako kazini wanafanya kazi walioyo tumwa na watanzania nchi nzima kama speaker kafuta hoja binafsi basi zitapelekwa kwa wananchi wa tanzania,hukumu itatoka huko ambayo haitamwangalia mtu usoni ni kichapo tu.mh.tundu antipas lissu anapiga kazi na akianza kuchangia watanzania kokote kule waliko humsikiliza sio mkorofi alisha wahi sema sessesion za bunge la tanzania ni "silly season" majira ya kujadili vitu vya kipuuzi ambavyo havitekelezeki wacha wawagalagaze tu ccm k'bu hawako kwa ajili ya watanzania!!!
 

lol Pasco, umeanza tena mchezo wa reverse pyschology :smile:, hivyo hapa unamwambia Mh Tundu Lissu atumie wembe ule ule alioutumia jana kumnyoa spika Mh Anna Makinda, amnyoe nao tena siku za usoni.

Bila shaka Mh Tundu Lissu amekusoma kwa utuo
 
Last edited by a moderator:
Kwani alipewa U speaker au aligombea mbona sikuelewi mtoa mada ? huyu mama hajalazimishwa alisema anaweza na apewe akapewa sasa nini. Piga kazi Tundu Lisu



 
Last edited by a moderator:
 
Pasco,
Kuwa mkweli kwa nafsi yako; hivi ukiwa mwanamke ndio uendeshe mambo kiholela tu? Hivi kuwa mwanamke ndio kutozingatia kanuni na sheria? Mimi ni mwanamke na ninaamini kuwa mwanamke si kiumbe dhaifu (kama wengi wanavyotaka kutusaidikisha) na hata kama akiwa dhaifu (huenda kutokana na malezi yaliojikita katika kumfanya mwanamke awe dhalili/ duni/ mnyonge) bado iko fursa ya kujengewa uwezo na kujiimarisha.
Anne Makinda ni miongoni mwa wanawake wa KiTz waliopata fursa hiyo. Tangu nasoma primary school miaka ya 80's huyu mama ni kiongozi. Amepitia ngazi nyingi hadi kuwa hapo. Kinachomfanya awe mnyonge na ashindwe kusimamia shughuli za bunge si uanamke wake, si ukali na ukweli wa Tundu bali ni tatizo lake la kujikomba na kutaka kubeba chama chake. Anne si mzalendo wa kweli na hana nia ya dhati ya kuisimamia serikali.

Mbona Jenister Mhagama ni mwanamke (eti hukalia kiti hicho kwa vipindi vichache tu), hana muda mrefu bungeni kama Anne lakini anamudu majukumu yake kisawasawa? Jenister anajua kujisimamia na kusimamia shughuli zake na kwa sasa ndiye pekee akikalia kiti hicho Bunge linakwenda.
Tundu hamshambulii Anne na wala hana chuki naye au kumdharau kwa kuwa ni mwanamke. Tundu hujenga hoja na kusimamia mambo ya msingi hata kama yupo Ndungai mwanamume mwenzake. Hapa tatizo ni Kiti kupwaya sana; angalia utendaji wa Ndungai na Mabumba (hovyo kabisa!)


Bahati mbaya kwa upande wake ni kuwa amekalia kiti nyakati ambazo idadi ya waTz (raia na wabunge) wanaojibu "hewala bwana" kwa kila jambo inapungua kila uchwao. Hivi sasa watu tunataka ujenge hoja zenye ushahidi wa kisayansi/ zilizofanyiwa utafiti wa kutosha. Ukileta longo longo ili kufunika kombe "mwanaharamu" hapiti na watu tunakomalia hadi ukweli ujulikane.
Tundu Lissu ni miongoni mwa waTz ambao hawana unafiki na wataka koleo iitwe kwa jina lake na si kijiko kikubwa!
Kama katika Chama chetu CCM tungekuwa na akina Tundu Lissu japo mmoja tu leo hii mwenyekiti wetu asingezungukwa na kundi la wanafiki. Hawataki ukweli utafutwe na ujulikane. Hawataki maendeleo ya kweli ya Taifa. Kunapokuwa na tatizo na uozo hawamwelezi ukweli Mwenyekiti wetu; matokeo yake leo Mwenyekiti wetu anaonekana dhaifu, hafai na hana uwezo wa kuongoza. Mara zote wanafiki hawa wamempotosha mwenyekiti na au amezungumza au kufanya maamuzi ambayo mwisho wa siku inakuwa aibu kwake, kwa chama na kwa taifa.
Kutokana na kuwa na wanafiki hawa waliomzunguka Mwenyekiti na Rais wetu leo Tz tumekuwa kichekesho na aibu kwa mataifa mengine. Leo heshima yetu imeshuka na hata baadhi ya watu wameanza kuandika "eti Tanzania iingizwe katika maajabu ya dunia kutokana na vituko vya serikali" Hii ni AIBU ISIYOVUMILIKA.
Hebu nitaje mifano michache tu ya kauli za wanafiki hawa:
1. Waziri anamhimiza Rais aendelee na safari za kwenda Ulaya na Asia kuomba omba wakati tuna rasilimali kibao! Ukimsikia utadhani anamhimiza kwa nia njema; mnafiki huyu. Anataka Rais aendelee kwenda kuombaomba mikopo ambayo hatutaweza kuilipa hata kizazi cha 10; na kinacholetwa waziri huyu na wenzake wanaishia kuiba na kujinufaisha wenyewe!

2. Waziri aliekabidhiwa ofisi ya umma; alizaliwa kabla ya uhuru na akakulia katika falsafa ya ujamaa na kujitegemea anajitapa kwenye vyombo vya habari eti, "Tunaheshimika sana ndio maana tunakopesheka". Hivi kweli KUKOPA NI HESHIMA???? Maandiko matakatifu yenyewe yanasema "AKOPAYE NI MTUMWA WA AKOPESHAYE". Halafu leo tunakuwa na waziri anayefurahia utumwa! Miaka 50 baada ya uhuru na rasilimali kibao tulizonazo!!!!
Kwa taarifa yako huyu waziri, katika jimbo lake ambalo kwa asili ni kame; changia na uharibifu wa mazingira halmashauri ya wilaya na wataalam wa kilimo kwa nia njema wanahimiza kilimo cha mtama. Lakini waziri huyu anaitumia njaa ya watu hawa kama mtaji wake wa kupata kura. Hataki waguswe na kuwajibishwa wanapotezembea kulima mtama. Mara wanapokusa mavuno wanamtumia ujumbe na yeye anaomba serikali walete mahindi ya msaada. Kwa njaa ya kujitakia kila mwaka waziri kafanya mtaji wa kupata KURA ili ALE!

3.
 
Ukikubali kazi uwe tayari kwa yote yanayoendana na hiyo kazi. kama kazi immeshinda aachie ngazi. Ameyataka mwenyewe kwa kuilinda serikali ya chama chake CCM. Agelikuwa anafuata taratibu na kanuni za kendesha shughuli za Bunge haya yote yasingelitokea.
 
 
 
 
Hivi mtu anapodai haki yake ni kosa?sasa inakuaje kwa tundu lissu anapoona haki za wabunge wa upande wa upinzani zinakiukwa na kuhoji anaitwa kinara wa fujo?je ni busara kwa mtu anayejua haki na wajibu wake kukaa kimya huku akiona atendewi haki? Mimi nadhani watu wa kulaumiwa ni mhe.spika na naibu spika kwa kushidwa kutenda haki kwa wabunge wa upinzani na kuwatolea maneno makali.mbona ktk kipindi cha uongozi mhe. Sitta bunge lilikuwa na mvuto kwa watanzania?kwa nini bunge ili lishindwe?kusoma hatuwezi hata kuangalia picha hatuwezi ? Tunataka bunge litoe haki sawa kwa vyama bila kujali rangi zao,dini wala kabila kwa faida ya taifa letu....
 
Pole Makinda, Pole Ndungai, jamaa wamewatosa, na nyinyi hamkujua moto utakaowakuta.

Lisu and co, Kaza buti hadi kieleweke
 
Hiyo ndiyo maana ya kuitwa chief whip,lazima ajutie kuwa kibaraka wa chama chake,angefuata miongozo ya bunge bila kupindisha kusingekuwa na shaka nae angeitwa speaker wa viwango.

Kwa uwendeshaji huu wa huyu Mh. Makinda wa Bunge hapa lazima tumkumbuke Mh. Sitta jinsi alivyolimudu bunge la kipindi chake na kuweza kuruhusu mijadala iliyowafanya wananchi waujue ujinga wa Serikali yetu.
 
...wakiendelea hivyo iko siku madame speaker ata-'crack', confidence imepotea kabisa! Lisu usilegeze kabisa...
 
women are emotional and men are logical. And because women are emotional they can't think properly specific in solving the matter at hand rather than satsfy their emotional. Kama huamini nachosema nipe logic ya kuzuia hoja binafsi kama si hisia za chuki na ubinafsi uliokubuhu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…