Mhe. Tundu Lissu, Please Acha Kumsulubu Spika Wetu! Unammaliza Kabisa Hadi Ameshindwa Kazi!

Mhe. Tundu Lissu, Please Acha Kumsulubu Spika Wetu! Unammaliza Kabisa Hadi Ameshindwa Kazi!

naona umeamua kumsema madam speaker 'indirectly'. nimeisoma hoja yako nimegundua kuna ujumbe unajaribu kuufikisha. hasa sio kila kitu mwanamke anaweza kuhimili. na kale kamsemo cha mwanamke akiwezeshwa anaweza kakome kuanzia leo. wakomae watoke wakishindwa wabaki nyumbani. madam speaker amedhihirisha hilo.
 
Jamani km kun mtu ana video za matukio ya jana na leo naomba atupie japo n sisi tuone!!!
 
Nimekuelewa sana mleta UZI. Umecheza na akili za watu Pele, but ujumbe umefika, Makinda hafai, pia majukumu ya kupeana, mwisho wa siku yanaonekana!
 
Kuna anaitwa Nancy Pelosi ! Tatizo letu ni mfumo mbovu wa kuendesha nchi. Huyu Mama Makinda kinachomsumbua ni kuogopa vikao vya CCM jioni

Makinda ni mjumbe wa CC ya CCM. Hivyo hawezi kwenda kinyuma kama CC imeamua kutowapa nafasi upinzani bungeni!

Kwangu mimi mkakati wa sasa wa CCM kujaribu kunyamazisha wabunge wa upinzani, na kukalia kooni vyombo vya habari ili wasianike madhaifu ya CCM na serikali yake, ni hatua mbaya kwa CCM yenyewe.
 
Naomba katiba mpya itamke kwamba spika wa bunge ni lazima achaguliwe na wabunge. Maana nilichokiona hapa ni kwamba muhimili wa bunge haupo kabisa.

Katiba ya sasa unaijua kweli wewe au unaisikia tu?? kama huna cha kuchangia kaa kimya na sio kuongea vitu ambavyo huvijui !

kwani spika anachaguliwa na nani kwa mujibu wa katiba ya sasa ??
 
mkuu Pasco sio fair kabisa, Lissu anamchanganya mama wa watu hadi saa nyingine anashindwa kuongea kiinglish kizuri na anakosea jina la Lindu Lissu.
 
Last edited by a moderator:
Wanabodi,

Leo nimepata fursa ya kuliangalia bunge live asubuhi hii kupitia TBC-1,
Spika wa Bunge, Mhe. Anne Makinda ameshindwa kabisa kuliendesha bunge!, amepwaya sana na ameendesha kika bila confidence kabisa na mwisho wa maelezo yake, akamtaja Mhe. Tundu Lissu kama ndiye mbunge anayeongoza kwa kuleta vurugu bungeni, na Lissu aliponyanyuka kuomba muongozo wa Spika, akamvurumishia tena Spika Makombora mazito, na kama angeendela kidogo tuu!, Spika Makinda ange break down kwa machozi!. (Naamini akifika ofisini kwake, atajifungia kidogo na kuimalizia hasira yake the same way wanawake wote wanamalizaga hasira zao!.

Kwa kuzingatia sifa kuu iliyomfanya Mhe. Mama Makinda kuchaguliwa kuwa spika, huku Mhe. Tundu Lissu akiujua fika uwezo wa Madam Spika, kwanini anaendelea kumsulubisha kila apatapo fursa?!. This is not fair!.

Kwa vile Mama Makinda amepewa uspika because she is a lady, kwa uzi huu, namuomba Mhe. Tundu Lissu na wabunge wengine wa Kambi ya Upinzani, wanapokuwa na hoja za msingi, wamuaddress Madam Spika with courtesy of addressing a lady, ili ku restore confidence yake kuliendesha bunge ambapo kwa sasa, ameshindwa kabisa, amezuia hoja zote binafsi, hivyo leo bunge limekutana asubuhi tuu kwa kipindi cha maswali na majibu na kuahirishwa, natumaini kesho na keshokutwa itakuwa vivyo hivyo!, huu ni ufujaji bure wa rasilimali za Taifa!.

Nawauliza wajameni, hivi hiki anachofanya Mhe. Lissu na wabunge wengine wa upinzani, kumsubulu Madam Spika ambaye ni mwanamke bila huruma, ni sawa kweli?!.

Kiafrika, wanawanake ni ni watu wa kubembelezwa na kuonewa huruma!, hivi hawa wabunge wa upinzani ni watu wa aina gani wasio hata na huruma kwa wanawake?!, leo ilibakia kidogo tuu madam spika angelia!, jee hiki wanachofanya ni sawa kweli?!. Ni haki?!.

Nawaombeni tumtendee haki Spika wetu aendesha bunge kwa haki na kujiamini!.

Pasco.

Post hii ina kila kitu kinachofanya tusiendelee.
 
MAKINDA na NDUGAI hawastahili hata chembe ya huruma sio kutoka kwa Wabunge tu bali kwa Watanzania wote. Wameshindwa kutimiza wajibu wao kwa kuamini kuwa hakuna wa kuwauliza wala kuwagusa na wameliharibu Bunge letu kabisa. Nahisi jinsi wanavyoliendesha bunge watakuwa wanatekeleza maagizo fulani vinginevyo inabidi wapimwe akili zao.
 
Huu ndiyo gharama anayolipa Speaker Anna Makinda. Kwa kweli ni kipindi kirefu sana amekuwa akiwadhrau wbunge wa upinzani. Wabunge wa upinzani amekuwa wakitoka nje ya Bunge kuonyesha kutoridhika kwao na maamuzi ya Speaker ya kupindisha kanuni za Bunge. Kwa busara ndogo ya wabunge wa CCM walidhani huo ni ushindi wasijue kuwa watanzania tulikwisha aapa kuwa 'TUMEONEWA KIASI CHA KUTOSHA, TUMENYENYESWA KIASI CHA KUTOSHA TUMEPUUZWA KIASI CHA KUTOSHA! Sasa basi. Ujasiri wa kukataa kupuuzwa bado tunao, tulikataa kwa wakoloni na sasa tunakataa kwa CCM. Hatuwezi tena kupuuzwa na Makinda walaNdungai. Tanzania ni yetu sote hatuombi kwa Makinda, Ndungai wala kwa wabunge wa CCM.
Mkumbuke kuwa Tume ya Jaji Nyarari iliona 80% ya watanzania ilikataa vyama vingi, 20% ndiyo iliyokubali mfumo wa vyama vingi. Kwa busara ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alikubali kuwakubali wachache kuliko wengi. Somo la Mwalimu kwa wana CCM ni kuwa si mara zote wengi wanakuwa sahihi, maranyingine wachache wanakuwa sahihi.Jifunzeni kuamua mambo kwa hoja sio kwa wingi hata kama ni upuuzi
Respect is a two way traffic. If you want to be respected you must respect others too.
 
JK mwenyewe alisema bora anyimwe Upresidar apewe Dr Slaa lakini sio Lisu sasa huyu Mbululu wenu Makinda mtamuonea huruma sana mpaka mwaka 2015. Acheni wakomeshwe unafiki wao huo ndio mshahara wa dhambi ya kumhujum mzee wa spee and standard.
 
Dah mkuu PASCO kweli wewe ni mwandishi wa habari mkongwe sana...
Sfi sana...Nimeisoma mara nne nne.....
 
Kwa nini anaongea gender inequality kwenye siasa. Only gender equality pertain in politics.

Hutaki kukubali kama wanawake wanataka wawe kama wanaume pamoja na kuwa hawataki wanaume wawe kama wanawake.

Mh. Makinda yuko kwenye hicho kiti kwa 'MERIT' kama wachapuzi wake wanavyotaka kutuaminisha, basi nasi tunatumaini atafanya kazi yake kwa kiwango cha "MERIT" tunayoaminishwa.

Mbona bunge la UK lilikuwa na mwanamke ambaye aliendesha bunge kwa kiwango cha hali ya juu kwa miaka mingi na kumudu vizuri ukilinganisha na aliyepo sasa pamoja na kupata makombora ya hapa na pale, ukizingatia bunge la waingereza kiwango chake ni cha juu.

Uanawake siyo sababu ya msingi kisiasa kama atakuwa fair and firm.

Nini hitimisho lako juu ya jinsi Lissu anavyomfanya Bi Kiroboto kama ambavyo lilivyokusudio la mleta uzi ,Mkuu Pasco
 
Last edited by a moderator:
Akyanani nimefurahia sana kazi iliyofanywa na team ya upinzani kwa kupokezana, natumaini umma
 
Kuna kazi nyingine ambazo mtu yeyote anaweza kuzifanya ila sio SHERIA. Kaka yangu Lissu anachofanya ni kumvuruga akili Spika, matokeo yake anajikuta amepwaya na kutoka nje ya mstari kabisa. Hii inaweza mwathiri mwanamke akajikuta ameingia P...od bila kutarajia.
tehe tehe.....akiwa mjamzito anaweza zaa live au....? nway nafurahi sana kwa kinachoendelea bungeni kwani chadema ndo inazidi kuchanja mbuga
 
Uma wa watanzania wameona umuhimu wa wabunge wa upinzani
 
Ikiwa 'mnadhimu mkuu" wa kambi ya upinzani hiyo ndio nidhamu yake, tutegemee nini kutoka upinzani bungeni?
 
Bunge la wakati huu lina Speaker na Naibu speaker vimeo kuliko wakati wote!.
 
Pasco,
Bunge ni sehemu ya uwakilishi wa wananchi. Halipaswi kuongozwa kichama au kiitikadi yoyote.
Ni siku nyingi Makinda na Ndugai wameligeuza bunge kama ukumbi wa familia zao.

Tunajua Makinda hakuwa na uwezo aliwekwa tu kwa kisingizio cha wanawake kwa kutumika na mafisadi.
Tunajua Ndugai anautaka uspika hivyo kujipendekeza ndio dini yake kwa sasa.
Lakini wasituharibie public place kama ile. Bunge si mahali pa kucheza mdumange au kitchen Party.

Mi nadhani wabunge waendelee kumvua nguo Makinda na Ndugai ili dunia ione kwanini sisi ni masikini.

Linajadailiwa suala nyeti la elimu, wanatokea wapuuzi kuzima mjadala kwasababu tu ya akili zao finyu.

Makinda na Ndugai kama wanataka waombe ukuu wa mikoa au wilaya waondoke bungeni.
Hawa ni aibu na fedheha ya taifa. Makinda hana soni wala haya hivyo hapaswi kupewa heshima kike.
Wanawake tunawajua walivyo na stara, wanavyojali familia na matatizo yanayowakumba.

Makinda anawasaliti wanawake katika hoja ya Mbatia kuhusu elimu na ile ya Mnyika kuhusu maji.
Msaliti wa mama na dada zetu wanaoumia kwa uzito wa majukumu ya kifamilia hapaswi kulinganishwa au kupata msamaha kama akina mama wengine wengi wenye heshima na akili zao

Hii ni 2013 upuuzi sasa hakuna.

Mwache asulubiwe tena ningefarijika kama pressure ingepanda akapunzike Appolo.
 
Back
Top Bottom