Mheshimiwa Alikuwa anafanya nini hapa?

Mheshimiwa Alikuwa anafanya nini hapa?

Amepita kwenye mioyo au amepitishwa kwenye box?
Amepita kwenye mioyo na wananchi wanasubiri wakapige tiki tu kwenye jina lake. Evelyn Salt hivi unajuwa kuwa ephen wangu kuzuiwa kutembelea jukwaa hili hadi tarehe 18 huko mwezi ujao.saizi ephen wangu amejishindia zake jukwaa la michezo .huko ndio nakokwenda kumpa faraja na kuondoleana upweke
 
Atapita tena na kuwaacha CHADEMA mkipiga porojo zenu.
Siyo rahisi watu wanahasira naye mno....hata aliye muhonga akajitoa kwenye ugombea, alipotea kabisa hajawahi kurudi ...raia walimchukia mno..Hata +255 Oparesheni ilipo pita huko hali ilikuwa dhahili kabisa Kigwangala amedhoofika sana kisiasa huko.
 
Hii ndiyo dini ya mwafrika sasa
images (2).jpeg
images (3).jpeg
images (4).jpeg
 
Ndugu zangu Watanzania,

Sitaki kuweka neno ila ndio hivyo kama mnavyoona kwenye picha hapa. Sijuwi Mheshimiwa alikuwa anafanyiwa nini .

Si unajuwa Tanzania mambo mengi mpaka wananchi wanachanganyikiwa na kushindwa washike nini na waache nini.

Ukigeuka huku unakutana na habari hii,ukienda kule unakuta vile,ukitazama mbele unaona vile. .kikubwa ni wewe uchague cha kutizama na uwe na misimamo yako binafsi.View attachment 3055439

Alichoandika Kigwangala kuhusiana na picha hii

View attachment 3055449
Kigwangala kupitia X:

Ndugu wapendwa Gen Zee, salaams.

Napenda kuwafahamisha ya kwamba hili vazi siyo uchawi! Wala uganga. Ni vazi la kimila; yanaitwa Masunzu, ama Nsunzu, ama nyie waswahili mnaita rasta.

Kwa mila na desturi zetu huvaliwa na warriors wanaitwa Sungusungu! Hawa ni askari wa jadi.

Wanaume wanavaa makubwa na yenye nakshi nzuri zaidi ya wanawake. Mjue kuwa hizo rasta zilizaliwa huku.

Ahsanteni sana.

Wakatabahu,
HK.
CCM na urozi ni dam dam
 
Uongo.mchawi huyo..Sungusungu bila Upinde na Shigi( kiji begi kidogo cha kubebea mishale)???.Sunzu ilipaswa kuwa ya manyoya ya kuku au bunela(nyuzi za katani).Hicho cha mkononi kinaitwa isale( kichoteo kinachotokana na aina fulani ya maboga)ndiyo kabisaaa hakina uhusiano na Sungusungu( Ndulilu).
Idimu unaharibu sana.
 
Back
Top Bottom