Elections 2010 Mheshimiwa John Pombe Magufuli awe Rais wetu

Elections 2010 Mheshimiwa John Pombe Magufuli awe Rais wetu

Mjadala ni mzuri na muhimu sana, lakini hamjadili jambo hapo naona majungu tu yanatembea hapo. tuelezeni kwanini anafaa/hafai kuwa Rais wetu.
 
Magufuli hawezi, kwanza asafifhe mizani, pili arudishe nyumba alizogawa bure. Nadhani raisi ajaye ni Dr. Slaa

Wana JF nani asiyejua ya kuwa Rais ajaye ni Dr. Slaa ?. Mijadala mingine bhana nikutujazia saver ya JF.
 
Masaburi yupi mkuu, unamaanisha huyu mzee mtaalam wa matusi aliyesema wabunge wa Dar wanafikiria kwa kutumia ------ au Masaburi mwingine? Kama unamaanisha huyo pls niombe radhi. Mimi sio wa namna hiyo na sio mtu wa do or dies politics

Unaweza kufunguka zaidi mkuu?Kwa sababu huyu uliyesema ni mwanao emanuel nchimbi hata wizara aliyonayo sasa haiwezi,huyo salim hafai kutuongoza.Kwa hadhi ya ukatibu wa afrika aje agombe ubalozi wa nyumba kumi kweli? !!! Hata uwezo wake si ule kwa sasa,hafaii
 
mi pia magufuli namkubali, pamoja na kuwa na hizo kashfa mnazozisema nadhani ni mtu anaeweza kufanya wengine wafanye inavyotakiwa...ndo mtu wa namna hii anaeweza peleka taifa mbele...
 
Kwa muono wangu huyu bwana ndio anafaa kumrithi Kikwete, kwa Nchi yetu ilipofikia tunahitaji Rais mwenye msimamo na mbabe kama huyu jamaa, hatuhitaji tena mtu soft!!!!!
mwanzoni alitumwa na Mzee Mkapa akafanya vizuri.
ametumwa na JK lakini hajafikia performance ya kwanza, na angekuwa na msimamo kweli kuna baadhi ya mambo yameonekana siyo lakini hakuyafafanua.
Mimi nadhani huyu ni mzuri pale anaposimamiwa lakini kumpa asimamie, sielewi. Acha Mzee Salim aje ampe
kazi ya kufanya
 
Magufuli alitakiwa sasa awe gerezani Ukonga kwa uhujumu uchumi!Aliwapa nyumba za serikali ndugu zake zilizojengwa na Nyerere kwa mikono yake(Kuna picha maktaba zinaonyesha Nyerere akibeba mchanga kwenye karai kuwapa mafundi akijenga nyumba za Oysterbay)Magufuli ndiye waziri anaye ongoza kwa kuitia hasara serikali((Rejea uamuzi wake alipogoma kutii amri ya mahakama na kubomoa kituo cha mafuta-Mwanza)

Mkuu Magufuli hakuishia kuwagawia ndugu zake na jamaa zake tu, bali alikwenda mbali zaidi na kuzigawia nyumba ndogo zake. Mfano ulio hai ni ule wa nyumba aliyo mgawia DEMU wake aliyekuwa akisoma Geology hapa UDSM anayeitwa Sundi.

Mbali na kashfa ya nyumba Magufuli aliliingiza taifa hasara kubwa ya kupindisha barabara ya ki-mataifa na kuipitisha jimboni kwake Chato kinyume na ilivyokuwa imekusudiwa awali.
 
Anafanya kazi kwenye media, anachotafuta yeye ni popularity tu.
Na anatembelea miradi yenye hela tu.
For example toka aingia madarakani hajatembelea miradi ya sumbawanga
 
Mjadala ni mzuri na muhimu sana, lakini hamjadili jambo hapo naona majungu tu yanatembea hapo. tuelezeni kwanini anafaa/hafai kuwa Rais wetu.

Uko sahihi sana,lakini kuna baadhi ya wachangiaji wanalazimisha kuwa anachoamini ndicho bora sana,tunawaweka sawa ili twende sambamba.
 
Hebu endeleeni kumchambua maana sie wengine huwa tunamsikia tu kwenye ufunguzi wa ujenzi wa mabarabara.

.............nakwambia ! .............halafu uzuri wake yataishia humu humu JF, wal hayawi hayo wanayo taka yawe !:nono:
 
Kwa muono wangu huyu bwana ndio anafaa kumrithi Kikwete, kwa Nchi yetu ilipofikia tunahitaji Rais mwenye msimamo na mbabe kama huyu jamaa, hatuhitaji tena mtu soft!!!!!

Wazungu tuliwajua ni Makaburu, na hata Wangekuwa weusi ni makaburuuu tuuuu.....CCM mbovu
 
tuambie wewe unayejifanya unamjua
tunataka hoja kwa hoja sio majungu tu ya kumchafua mtu
anafaa kijiunga na mzee yusufu,alishamalizwa na mwenyekuti wake wa chama.hata wewe unalijua hilo.kwahiyo hatufai.
 
tuambie wewe unayejifanya unamjua
tunataka hoja kwa hoja sio majungu tu ya kumchafua mtu

Mkuu unakujaga juu akitajwa urais mtu mwingine zaid ya EL!!! Kwa taarifa yenu watanzania
mpango wetu ni kuliweka pembeni kabisa hili dude linaitwa ccm.so hatuna haja ya kujua sifa
za wagomea wa ccm.
 
Magufuli hafai, mtu wa visasi sana na pia akikujia juu ujue hujatoa cha juu. Bara bara nyingi zipo chini ya viwango lakini hawarudii kuna nini hapo.

Pamoja na kwamba ninaichukia sana ccm lakini pia hua spendi mtu kusingiziwa, Barabara zilizo jengwa chini ya kiwango nyingi zilikua chini ya bwana shukuru kawambwa (nimeanza kuhofia kumwita Dr cause of his capability) baadhi yake ni ile ya Kilwa Road na Singida Nzega, barabara hii pamoja na kwamba mkataba ulikuwepo tokea enzi ya Mkapa chini ya Magufuri lakini Kikwete alimtoa kwenye wizara hiyo na kumwingiza bwana Shukuru Kawambwa, hapo ndipo usimamizi ulipopwaya, ameingia mzee wa kilomita, barabara hizo zote zime/zinarudiwa, kwahili naomba tumtendee haki. Hapo kwenye italic na red, sijaelewa, visasi vya kibinafsi au kwa walioliibia taifa? Ingawa hapa kwenye kuliibia taifa sidhani kama naye huyu ana sifa za usafi, lipo swaga la nyumba za serikali, yeye ndiye alikua kinara wa uuzaji na leo tunasafa!
 
Mkuu unakujaga juu akitajwa urais mtu mwingine zaid ya EL!!! Kwa taarifa yenu watanzania
mpango wetu ni kuliweka pembeni kabisa hili dude linaitwa ccm.so hatuna haja ya kujua sifa
za wagomea wa ccm.
Ni bora mzijue kwasababu hao ndio watawatawala.mtake msitake
 
naona umetembelewa na popobawa leo ndo maana hujitambui...nadhani aliwahi kukulala hakukulipa ndo maana unamchukia...

ccm mmebakia matusi,sikushangai wewe unayetegemea upuuzi huu ndo upate mkate wa kila siku,kwani hata mabosi wenu wanatukana
 
Mh Magufuli? Refer tu ile scandal ya DFP (Donor Funded Project) plate numbers ndiyo mtajua "umakini" wa huyu jamaa. Tatizo Watanzania wana danganyika kirahisi. Mtu akijionyesha onyesha kwenye t.v. kuwafokea watu ndiyo wanamuona mchapakazi. Hamja koma tu kuuziwa mbuzi kwenye gunia?
 
Magufuli anafaa urais kwa vigezo vp? Kukariri kilometer ya barabara ndiyo anafaa kuwa Rais? Kama una akili timamu/timilifu ndani ya Serikali ya CCM huwezi fanya kazi timilifu. Rais anayeweza kufanya kazi kweli yuko nje ya Serikali ya CCM
 
Kwa muono wangu huyu bwana ndio anafaa kumrithi Kikwete, kwa Nchi yetu ilipofikia tunahitaji Rais mwenye msimamo na mbabe kama huyu jamaa, hatuhitaji tena mtu soft!!!!!
Kwa mtu smart anayemjua Magufuli au anayejua sihasa hawezi kudhubutu hata kufikiria hivyo!!! pale hakuna kitu!anajua kucheza na media tu full stop!!! lakini kumpa nchi hapana...nitahama!! jamani kuongoza nchi siyo kukurupuka na kukaripia kwenye vyombo vya habari tu,kha! ni zaidi ya hapo...kweli wajinga ndio waliwao!
 
Back
Top Bottom