Elections 2010 Mheshimiwa John Pombe Magufuli awe Rais wetu

Elections 2010 Mheshimiwa John Pombe Magufuli awe Rais wetu

Kwanza nadini ya CCM hawezi kukubarika kwa sababu wanajua kuwa atawasumgua kwa kutaka kwake sifa anaweza kufanya kitu cha ajabu bila hata ya kufikiria. Wanaojua vizuri mwanza watakumbuka vituko alivyofanya wakati wa uvunjaji wa kituo cha mafuta cha MOIL, alilazimisha kuvunja matokeo yake serikali iliwalipa pesa nyingi sana wale wahindi wa CCM! Kwa kupenda kujipendekeza JP alipongeza safari za raisi JK pamoja na kujua fika zinaliingiza taifa kwenye ghalama zisizo za lazima hii yote ni kwa sababu huyu mheshiwa anapenda sifa sana so alijipendekeza kwa JK kwa kumpa sifa zisizo na tija kwa watanzania of which watanzania sidhani kama tunahitaji raisi wa style hii. Kwa visasi ndo mwenyewe kumbukeni issue ya fast ferry za Azam alozileta lake Victoria, JP alitaka kumkomoa Mwandosya kwa vile alikuwa amekula karamu ya ujio wa meli hizo hivyo JP akajua kumkomoa ni kugoma kusaini boti hizo kupitishwa kwenye barabara zake kwa kisingizio ni nzito wakati kuna mitambo ya migodini ni mizito mara mbili ya boti hizo kila siku inapitishwa kwenye barabara zake na sisi watz tukishuhudia. Kwa kifupi JP hafai hata kidogo kuwa raisi, ikumbukwe tena aliwahi kupigiwa kelele na wananchi wa Buziku kwenye moja ya mikutano yake jimboni chato,alichokifanya ni kuwaambia kwa kisukuma " Buta baba gete mtalaibona ilami maisha ging'we pyee!" kilichotokea ni kuipindisha barabara ya lami ilotakiwa kupita Buziku akalazimisha ipite Chato ili kuwakomoa wananchi hao....sasa jamani tunamjadiri kuwa raisi wa nchi mtu wa aina hii? Labda kwa vile ni demokrasia acha tumuweke tena raisi wa majaribio kama tulivyofanya 2005 & 2010.
 
Hahahaa, ngoja kwanza nikamuulize Sundi, ile nyumba aliyohongwa na kuwanyima haki walioitumikia serikali kwa miaka lukuki aliirejesha?
 
tuambie wewe unayejifanya unamjua
tunataka hoja kwa hoja sio majungu tu ya kumchafua mtu

A very poor and most incompetent manager I ever worked with! Kwa taarifa yako (wewe na wengine mnaodhani Magufuli ni mchapa kazi) 99% ya "amri" anazotoa huwa zimefanyiwa kazi na mamlaka husika (mostly donors) yeye hurukia kutangaza ili kupata popularity.

Kiini cha watu kudhani Magufuli anaiwezea wizara anayoongoza in ujenzi wa barabara (ambazo practically zote ni donor-funded). Kwa taarifa yenu; donors wana-direct kila kitu, kuanzia procurement za consultants na contractors hadi malipo ambayo donor country hulipa directly kwenye account ya consultant/contractor. Serikali ina-manage 10% contribution (ambayo nayo mostly ni administration and local taxes). Ni sawa na mtu aje akujengee nyumba halafu wewe ujisifu kuwa umejenge nyumba!
 
ikulu ni mahala pa kuheshimika ukipeleka mwenyekislani Pombe Ma kufuli ataharibu sana
Kwanza nadini ya CCM
hawezi kukubarika kwa sababu wanajua kuwa atawasumgua kwa kutaka kwake
sifa anaweza kufanya kitu cha ajabu bila hata ya kufikiria. Wanaojua
vizuri mwanza watakumbuka vituko alivyofanya wakati wa uvunjaji wa kituo
cha mafuta cha MOIL, alilazimisha kuvunja matokeo yake serikali
iliwalipa pesa nyingi sana wale wahindi wa CCM! Kwa kupenda
kujipendekeza JP alipongeza safari za raisi JK pamoja na kujua fika
zinaliingiza taifa kwenye ghalama zisizo za lazima hii yote ni kwa
sababu huyu mheshiwa anapenda sifa sana so alijipendekeza kwa JK kwa
kumpa sifa zisizo na tija kwa watanzania of which watanzania sidhani
kama tunahitaji raisi wa style hii. Kwa visasi ndo mwenyewe kumbukeni
issue ya fast ferry za Azam alozileta lake Victoria, JP alitaka kumkomoa
Mwandosya kwa vile alikuwa amekula karamu ya ujio wa meli hizo hivyo JP
akajua kumkomoa ni kugoma kusaini boti hizo kupitishwa kwenye barabara
zake kwa kisingizio ni nzito wakati kuna mitambo ya migodini ni mizito
mara mbili ya boti hizo kila siku inapitishwa kwenye barabara zake na
sisi watz tukishuhudia. Kwa kifupi JP hafai hata kidogo kuwa raisi,
ikumbukwe tena aliwahi kupigiwa kelele na wananchi wa Buziku kwenye moja
ya mikutano yake jimboni chato,alichokifanya ni kuwaambia kwa kisukuma "
Buta baba gete mtalaibona ilami maisha ging'we pyee!" kilichotokea ni
kuipindisha barabara ya lami ilotakiwa kupita Buziku akalazimisha ipite
Chato ili kuwakomoa wananchi hao....sasa jamani tunamjadiri kuwa raisi
wa nchi mtu wa aina hii? Labda kwa vile ni demokrasia acha tumuweke tena
raisi wa majaribio kama tulivyofanya 2005 & 2010.
 
Jina lako linafanana nawe,ila nakuibia siri kwamba J.P.Makufuli hafai kuwa rais,sababu kubwa sana,huyu jamaa ni mtu wa kisasi sana.Namfahamu tangu akiwa TANROAD Morogoro.Si kila kinachong'aa kwako kinang'aa na kwa wengine.

Hapo kwenye red ...................... JPM alishawahi kufanya kazi TANROAD?? AU unajizungumzia mwenyewe??
 
Tangia awaambie watu wa Kigamboni wakitaka wapige mbizi eti kwa sababu walimzomea kwa kitendo chake cha kufanya kivuko kuwa biashara simuoni kama mtu muungwana na mwenye hekima. Ni mgomvi na mwenye kutumia maguvu kuliko akili. Karibia asilimia kubwa ya wazazi wa kigamboni waliokuwa na watoto wanasoma upange wa mjini wamewatoa watoto wao huko kwa kushindwa kulipia gharama za MAGARI kwenye kivuko. HAkuwasamehe hata watoto hao wasafiri bure kwenda kusoma ni mdharimu kama wadharimu wengine wa CCM. HAFAI
 
Kwa muono wangu huyu bwana ndio anafaa kumrithi Kikwete, kwa Nchi yetu ilipofikia tunahitaji Rais mwenye msimamo na mbabe kama huyu jamaa, hatuhitaji tena mtu soft!!!!!

kazi inayomfaa Magufuli ni kuwa discipline master kwenye shule ya sekondari ya wavulana watukutu, hilo nina uhakika ataliweza sana. Kuchapa viboko.
 
Kwa iyo unasama magufuli ana msimamo???

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Kwa muono wangu huyu bwana ndio anafaa kumrithi Kikwete, kwa Nchi yetu ilipofikia tunahitaji Rais mwenye msimamo na mbabe kama huyu jamaa, hatuhitaji tena mtu soft!!!!!

Hapa ndio aliharibu

dkmagupombe.jpg
 
Ukimjua utakuwa wa kwanza Kumpinga kwa Nguvu zote, Binafsi hata angegombea na nani siwezi mpa kura yangu

ni kajizi hako ila kanajifichia kwa kujifanya kanakomaa na wezi lakini wapi. mnakumbuka kaliwahi kumnunulia demu wake nyumba za serikali wakati demu hakuwa mfanyakazi wa serikali?
 
Uko sahihi sana,lakini kuna baadhi ya wachangiaji wanalazimisha kuwa anachoamini ndicho bora sana,tunawaweka sawa ili twende sambamba.

Sasa wewe ni mgumu ki vip kuelewa,au huoni sababu wanazotoa hapa..
Usijifanye kichwa kigumu..
Tayar wanaema hafai kw sababu ni fisadi kw kutoa nyumba za taifa, ana jazba,mtu wa visasi,sio mkwlei..we unataka nn sasa..
Nenda sehemu nyingine achia greater think wachangia au we soma tuu na usichangia pia ni hekima..
 
Hapa ndio aliharibu

dkmagupombe.jpg

Afadhari wewe uliyeonyesha picha hii na kusema ukweli kuliko mtiririko wa comment za wengine kwenye huu uzi. Hata mimi ninakubaliana na wewe, viongozi wetu walioenda kupata kikombe cha huyu Babu hawakuwatendea haki wananchi hasa wale waliofariki njiani au kwa kuacha kutumia dawa walizopewa hospitali kwa ajiri ya kikombe fake.

Kwetu sisi tusiyemfahamu vizuri JPM tunashindwa hapa kupata undani wake. Comment nyingi zinachagizwa na majungu au maneno ya vijiweni huku wengine wakitanguliza itikadi kabla ya ukweli kuhusu JPM.
 
....uzuri,atatufahamu watanzania wote by age,character,names,location,heights,weights,color,habitat na........mengineo mengi!yaani mpk akiona mwandiko tu....anajua huyo nani!
 
Unaweza kufunguka zaidi mkuu?Kwa sababu huyu uliyesema ni mwanao emanuel nchimbi hata wizara aliyonayo sasa haiwezi,huyo salim hafai kutuongoza.Kwa hadhi ya ukatibu wa afrika aje agombe ubalozi wa nyumba kumi kweli? !!! Hata uwezo wake si ule kwa sasa,hafaii
Ni kwamba CCM na makundi yote unayoyajua wewe, huyu ndoo peke yake anatoka kundi hili na kwenda kuongea kundi hili mchana kweupeeee. makundi yote yanamkubali. Ila mimi binafsi nasema hivi. CCM hawana jipya mtu ukimtaja mtu ndani ya CCM maana yake unadhani CCM ikiendelea kutawala nchi hii kutatokea mabadiliko kitu ambacho ni ndoto ya mchana. Mabadiliko ya nchi hii yanaletwa na watu wengine au chama kingine sio CCM. Hao nimewataja kuwa wanaweza wakashinda kuteuliwa ndani ya chama chao sio kuongoza nchi hii kwa sasa.
Umesema nifunguke nasema sasa hivi Tanzania inatakiwa tuwape Chadema nao tuwaone japo najua utasema uongozi sio kitu cha kubahatisha lakini wanasiasa wote siwezi kuwawekea zamana maaana wanabadilika sana wakiingia madarakani.
Unaweza kupendekeza CUF, nitaomba unitajie hata harufu ya mabadiliko kule Zbar ambako wanashiriki uongozi. Wameshindwa ndiyo maana wananchi mategemeo yao wanayapeleka kwa wanauamsho
 
A very poor and most incompetent manager I ever worked with! Kwa taarifa yako (wewe na wengine mnaodhani Magufuli ni mchapa kazi) 99% ya "amri" anazotoa huwa zimefanyiwa kazi na mamlaka husika (mostly donors) yeye hurukia kutangaza ili kupata popularity.

Kiini cha watu kudhani Magufuli anaiwezea wizara anayoongoza in ujenzi wa barabara (ambazo practically zote ni donor-funded). Kwa taarifa yenu; donors wana-direct kila kitu, kuanzia procurement za consultants na contractors hadi malipo ambayo donor country hulipa directly kwenye account ya consultant/contractor. Serikali ina-manage 10% contribution (ambayo nayo mostly ni administration and local taxes). Ni sawa na mtu aje akujengee nyumba halafu wewe ujisifu kuwa umejenge nyumba!

Donors hawafadhili Wizara ya Magufuli tu bali wanafadhili Wizara karibu zote, hivyo huko kwingine nako tungewasikia hao Mawaziri nao!
Na Bw. Magufuli kila Wizara aliyopelekwa alionekana ni mchapa kazi na lazima utamsikia, alikuwa Wizara ya Uvuvi ambayo ilikuwa haijulikani kabisa lkn akasikika kwa kukamata wavuvi haramu tangu amaeondoka Uvuvi na yo kimyaaa, kasimamia barabara nyingi tu Tanzania mfano br. ya kwenda Mbagala ambayo ilikuwa chini ya kiwango sasa inarudiwa chini ya usimamizi wake, kipande cha Sekenke huko Singida sasa Mkandarasi anarudia kwa Usimamizi wake, hivyo hoja hapa ni kwamba anaweza asiwe mkamilifu kama sisi wote tulivyo lkn ukimlinganisha na Mawaziri tulionao, NDIYO, ni mchapakazi!
 
Slaa hata akihamia CCM hatakuja kuwa rais wa Tanzania

Mkuu inakupasa ufunguke; Rais mtarajiwa siyo Slaa bali ni Dr. Slaa kiboko cha mafisadi, sipati picha mtaweka wapi nyuso zenu nyie masalia mara baada ya uchaguzi mkuu 2015. Dr. Slaa ndiyo rais mtarajiwa, funguka Njomba hiyo ndo habari ya mjini.
 
Donors hawafadhili Wizara ya Magufuli tu bali wanafadhili Wizara karibu zote, hivyo huko kwingine nako tungewasikia hao Mawaziri nao!
Na Bw. Magufuli kila Wizara aliyopelekwa alionekana ni mchapa kazi na lazima utamsikia, alikuwa Wizara ya Uvuvi ambayo ilikuwa haijulikani kabisa lkn akasikika kwa kukamata wavuvi haramu tangu amaeondoka Uvuvi na yo kimyaaa, kasimamia barabara nyingi tu Tanzania mfano br. ya kwenda Mbagala ambayo ilikuwa chini ya kiwango sasa inarudiwa chini ya usimamizi wake, kipande cha Sekenke huko Singida sasa Mkandarasi anarudia kwa Usimamizi wake, hivyo hoja hapa ni kwamba anaweza asiwe mkamilifu kama sisi wote tulivyo lkn ukimlinganisha na Mawaziri tulionao, NDIYO, ni mchapakazi!

"Mkuu ni vyema tukaweka ushabiki wa kisiasa pembeni na tukaongelea hali halisi ilivyo nchini. Let say Magufuli anakuwa Rais, je unatarajia mabadiliko gani ndani ya mfumo huu wa CCM unaoundwa na watu wale wale, na wenye fikra zile zile ?"
 
Hayo ni mambo mengine, wala mimi kwenye siasa sipo, Mimi nimevutiwa tu na utendaji kazi wake nikilinganisha na hawa wengine waliopo, sasa kama anafaa kuwa Raisi na kama ataweza kuubadilisha mfumo uliopo hilo ni swali gumu sana, kwa maana mabadiliko hayaletwi na mtu mmoja bali ni ushirikiano, hivyo kama sisi wenyewe kama jamii hatutaki au hatuko tayari kubadilika ili kuboresha maisha maisha yetu, hakuna kitu mtu mmoja anaweza kufanya!
 
Back
Top Bottom