Ninamkumbuka sana Magufuli kwa haya yafuatayo:
1. Alipokuwa Mifugo na Uvuvi Tanzanzia kwa mara ya kwanza ilikamata maharamia wa kigeni waliokuwa wamezoea kupora samaki wetu - alitoka na msemo wa bahari yetu siyo shamba la bibi. Kikubwa zaidi maharamia hao tena wa kigeni wamehukumiwa kifungo ndani ya ardhi ya Tanzania, waziri gani mwingine kafanya tukio kama hili?? Huyu kwangu ni shujaa!
2. Miaka ya 2000 alikamata magari ya serikali zaidi ya 21,000 ikiwemo mitambo na pikipiki. Magari enzi hizo yalikuwa yakiandikwa mpaka majina binafsi mfano nakumbuka moja liliandikwa Mwakajinga! Isitoshe zoezi hilo limerudiwa juzi kati ambapo magari zaidi ya 1000 yamealikuwa yanatumika vibaya kwa kuwa yalikuwa na namba za kiraia - kwangu mimi huyu ni kiongozi anayelinda mali za umma na kuhimiza matumizi sahihi ya mali za umma. Lakini maadui zake walioguswa na zoezi hili wanamshambulia, ni jukumu la wananchi wa kawaida kulijua hili!!
3. Amejenga barabara za lami zaidi ya kilometa 11000 na mpaka CCM wamekuwa vihelele wakimtumia kwenye majukwaa ili afanye presentation kuhusu mafanikio ktk ujenzi wa barabara tangu uhuru, lakini kibaya zaidi humohumo ndani ya CCM kuna kundi lipo kimkakati kumvuruga pengine aonekane si kitu!
4. Kumekuwa na malamiko ya barabara kujengwa chini ya kiwango, Magufuli kawakaba makandarasi wote na sasa barabara ya Singida kwenda Shelui, upande wa Sekenke inarudiwa na Mkandarasi kwa gharama zake zipatazo shilingi bilioni 15 na juzi kati tumeona makamu wa rais akifungua ile ya Mbagala ambapo Mkandarasi alirudia kwa hela zake, leo Magufuli anaoneka mbaya?
5. Alipokuwa wizara ya ardhi alianzisha mradi wa Viwanja 20,000 kule Kigamboni na kurudisha uwajibikaji wa wafanyakazi wa ardhi kiasi cha wananchi kusifia huduma za Wizara, leo hii mtu huyu anaonekana si lolote ndani ya CCM
6. Akiwa Ujenzi alizuia meli kubwa kusafirishwa kwa njia ya barabara ambapo ingeharibu barabara na hata meli hilo lisingeweza kupita ktk madaraja , lakini CCM hawaoni hili??
7. Kuhusu nyumba nakumbuka lilikuwa ni Azimio la Serikali nzima ambapo baraka zilitoka ktk baraza la mawaziri na yeye alikuwa na jukumu la kutekeleza tu! Sasa wana CCM hata siku moja hawatokei kumtetea hata kwa maneno mepesi tu, mtu huyu anaonekana kwao mbaya! Lakini katika hili nakumbuka hata Nyerere aliuza nyumba za serikali mfano pale Magomeni, Mwanza( Ghana Cottage), Tabora etc wana CCM wameshindwa kutumia mfano huu kumlinda kijana wao???
8. Humu jamvini Watu wanaandika Magufuli kawahi kuwa meneja TANROADS Morogoro ? Uvivu wa kufuatilia taarifa sahihi za viongozi - Hebu angalia CV za wabunge ktk tovuti ya bunge kama Magufuli aliwahi ajiliwa na Wizara ya Ujenzi kama mtumishi wa Umma?
9. Aliwahi chafuliwa kwa kuandikwa na gazeti moja kwa kipindi cha Miezi minane mfululizo, na baadae aliyefanya/tekeleza kazi hiyo kazawadiwa ukuu wa wilaya fulani- sisi siyo wajinga, tunajua mambo hayo!
10. Katika chaguzi za mwaka 2000 na 2005 alipita bila kupingwa jimboni kwake Chato na hata chaguzi za 1995 na 2010 ukiangalia matokeo utajua ni jinsi gani wananchi wake wanamhusudu lakini leo hii watu wanataka kuupoteza ukweli!
11. Lakini hata hivyo, mawaziri wenzake wanakubaliana naye jinsi anavyofanya kazi bila kuogopa mtu!
12. Ndiye aliyeanzisha mfumo wa kujenga barabara kwa kutumia hela zetu za ndani bila kutegemea wafadhiri na alianzisha model ya design and build mpaka wenzetu jirani Kenya wakaja kuiga kipindi hicho Raila Odinga akiwa waziri wa barabara wa Kenya!
13. Ni waziri pekee aliyekaa Wizara ya ujenzi kwa muda mrefu penye vishawishi vya rushwa bila shutuma yeyote ile
WITO WANGU KWA MHESHIMIWA MAGUFULI:
1. Wanaokuchafua sio sisi CHADEMA bali ni wana CCM wenzako ambao kila kukicha wanakuogopa kwa vile unakubalika na wananchi walio wengi!
2. Nakushauri jiunge na CHADEMA ili uje kushirikiana na Dr . Slaa tayari kwa ukombozi wa taifa hili
3. NAKUSISITIZA MHESHIMIWA MAGUFULI NI WAKATI WAKO SASA KUHAMIA CHADEMA