Elections 2010 Mheshimiwa John Pombe Magufuli awe Rais wetu

Elections 2010 Mheshimiwa John Pombe Magufuli awe Rais wetu

tuambie wewe unayejifanya unamjua
tunataka hoja kwa hoja sio majungu tu ya kumchafua mtu
ha ha aha waulize wananchi wa jimbo la Biharamulo alichowafanyia kupitisha barabara ya lami nyumbani kwao chato kisa yeye alikuwa waziri wa ujenzi na walikataa kumchagua kuwa mbunge uchaguzi wa 1990
 
Kwa muono wangu huyu bwana ndio anafaa kumrithi Kikwete, kwa Nchi yetu ilipofikia tunahitaji Rais mwenye msimamo na mbabe kama huyu jamaa, hatuhitaji tena mtu soft!!!!!

Hatuko tayari kupiga mbizi.
 
haya bana tuma salamu kwa watu watatu maana mnachuki binafsi na watu hadi mapovu yanawatoka,angekuwa ameandikwa slaa hapo ndo mngekuwa mnakenua mimeno tu kama mmetekenywa

ha ha aha waulize wananchi wa jimbo la Biharamulo alichowafanyia kupitisha barabara ya lami nyumbani kwao chato kisa yeye alikuwa waziri wa ujenzi na walikataa kumchagua kuwa mbunge uchaguzi wa 1990
 
Ukimjua utakuwa wa kwanza Kumpinga kwa Nguvu zote, Binafsi hata angegombea na nani siwezi mpa kura yangu
Mmmmmmmmmmmm absolutely true waulize wananchi wa jimbo la Biharamulo alichowafanyia alipindisha barabara ya lami ipite nyumbani kwao kisa eti yeye ni waziri wa ujenzi na wananchi wa Biharamulo walikataa kumchagua kuwa mbunge 1990 huyu jamaa ni mbinafsi sana: Rockon:
 
haya bana tuma salamu kwa watu watatu maana mnachuki binafsi na watu hadi mapovu yanawatoka,angekuwa ameandikwa slaa hapo ndo mngekuwa mnakenua mimeno tu kama mmetekenywa

Tunatakiwa kuweka sifa ambazo rais wa tano wa tanzania anatakiwa kuwa nazo. Tukishakubaliana hizi sifa ndio tunamuangalia Kama magufuli au mtanzania mwingine anazo. Hapo ndipo tutaweza kufanya maamuzi. Mimi naona sifa zifuatazo ni muhimu

Awe anamaono ya muda mrefu juu ya maendeleo ya nchin yake
Awe hapendi rushwa kwa mane no na vitend
Asiwe mdini, MKabila wall mbaguzi wa aina yeyot
Awe na uwezo wa kufanya maamuzi magumu kwa manufaa ya taiga
Awe mchapakazi
Awe humble with unquestionable character in terms of integrity and honesty
 
Hizi habari za majina manne manne tumekuwa Wahispania?

Ilianza Mizengo Kayanza Peter Pinda (Sounds like "Mizengwe Kaanza Kupita Pinda")

Sasa John Pombe Joseph Magufuli (Njooni Pombe Mkose Makufuli)

What's with all these names?

Mwisho tuta recite vizazi vyote kama Agano la Kale sasa.
 
Hapa ndio aliharibu

dkmagupombe.jpg

hapa anatandika bila huruma kikombe cha babu
 
Kwa muono wangu huyu bwana ndio anafaa kumrithi Kikwete, kwa Nchi yetu ilipofikia tunahitaji Rais mwenye msimamo na mbabe kama huyu jamaa, hatuhitaji tena mtu soft!!!!!


Ninamkumbuka sana Magufuli kwa haya yafuatayo:

1. Alipokuwa Mifugo na Uvuvi Tanzanzia kwa mara ya kwanza ilikamata maharamia wa kigeni waliokuwa wamezoea kupora samaki wetu - alitoka na msemo wa bahari yetu siyo shamba la bibi. Kikubwa zaidi maharamia hao tena wa kigeni wamehukumiwa kifungo ndani ya ardhi ya Tanzania, waziri gani mwingine kafanya tukio kama hili?? Huyu kwangu ni shujaa!

2. Miaka ya 2000 alikamata magari ya serikali zaidi ya 21,000 ikiwemo mitambo na pikipiki. Magari enzi hizo yalikuwa yakiandikwa mpaka majina binafsi mfano nakumbuka moja liliandikwa Mwakajinga! Isitoshe zoezi hilo limerudiwa juzi kati ambapo magari zaidi ya 1000 yamealikuwa yanatumika vibaya kwa kuwa yalikuwa na namba za kiraia - kwangu mimi huyu ni kiongozi anayelinda mali za umma na kuhimiza matumizi sahihi ya mali za umma. Lakini maadui zake walioguswa na zoezi hili wanamshambulia, ni jukumu la wananchi wa kawaida kulijua hili!!

3. Amejenga barabara za lami zaidi ya kilometa 11000 na mpaka CCM wamekuwa vihelele wakimtumia kwenye majukwaa ili afanye presentation kuhusu mafanikio ktk ujenzi wa barabara tangu uhuru, lakini kibaya zaidi humohumo ndani ya CCM kuna kundi lipo kimkakati kumvuruga pengine aonekane si kitu!

4. Kumekuwa na malamiko ya barabara kujengwa chini ya kiwango, Magufuli kawakaba makandarasi wote na sasa barabara ya Singida kwenda Shelui, upande wa Sekenke inarudiwa na Mkandarasi kwa gharama zake zipatazo shilingi bilioni 15 na juzi kati tumeona makamu wa rais akifungua ile ya Mbagala ambapo Mkandarasi alirudia kwa hela zake, leo Magufuli anaoneka mbaya?

5. Alipokuwa wizara ya ardhi alianzisha mradi wa Viwanja 20,000 kule Kigamboni na kurudisha uwajibikaji wa wafanyakazi wa ardhi kiasi cha wananchi kusifia huduma za Wizara, leo hii mtu huyu anaonekana si lolote ndani ya CCM

6. Akiwa Ujenzi alizuia meli kubwa kusafirishwa kwa njia ya barabara ambapo ingeharibu barabara na hata meli hilo lisingeweza kupita ktk madaraja , lakini CCM hawaoni hili??

7. Kuhusu nyumba nakumbuka lilikuwa ni Azimio la Serikali nzima ambapo baraka zilitoka ktk baraza la mawaziri na yeye alikuwa na jukumu la kutekeleza tu! Sasa wana CCM hata siku moja hawatokei kumtetea hata kwa maneno mepesi tu, mtu huyu anaonekana kwao mbaya! Lakini katika hili nakumbuka hata Nyerere aliuza nyumba za serikali mfano pale Magomeni, Mwanza( Ghana Cottage), Tabora etc wana CCM wameshindwa kutumia mfano huu kumlinda kijana wao???

8. Humu jamvini Watu wanaandika Magufuli kawahi kuwa meneja TANROADS Morogoro ? Uvivu wa kufuatilia taarifa sahihi za viongozi - Hebu angalia CV za wabunge ktk tovuti ya bunge kama Magufuli aliwahi ajiliwa na Wizara ya Ujenzi kama mtumishi wa Umma?

9. Aliwahi chafuliwa kwa kuandikwa na gazeti moja kwa kipindi cha Miezi minane mfululizo, na baadae aliyefanya/tekeleza kazi hiyo kazawadiwa ukuu wa wilaya fulani- sisi siyo wajinga, tunajua mambo hayo!

10. Katika chaguzi za mwaka 2000 na 2005 alipita bila kupingwa jimboni kwake Chato na hata chaguzi za 1995 na 2010 ukiangalia matokeo utajua ni jinsi gani wananchi wake wanamhusudu lakini leo hii watu wanataka kuupoteza ukweli!

11. Lakini hata hivyo, mawaziri wenzake wanakubaliana naye jinsi anavyofanya kazi bila kuogopa mtu!

12. Ndiye aliyeanzisha mfumo wa kujenga barabara kwa kutumia hela zetu za ndani bila kutegemea wafadhiri na alianzisha model ya design and build mpaka wenzetu jirani Kenya wakaja kuiga kipindi hicho Raila Odinga akiwa waziri wa barabara wa Kenya!

13. Ni waziri pekee aliyekaa Wizara ya ujenzi kwa muda mrefu penye vishawishi vya rushwa bila shutuma yeyote ile

WITO WANGU KWA MHESHIMIWA MAGUFULI:

1. Wanaokuchafua sio sisi CHADEMA bali ni wana CCM wenzako ambao kila kukicha wanakuogopa kwa vile unakubalika na wananchi walio wengi!

2. Nakushauri jiunge na CHADEMA ili uje kushirikiana na Dr . Slaa tayari kwa ukombozi wa taifa hili

3. NAKUSISITIZA MHESHIMIWA MAGUFULI NI WAKATI WAKO SASA KUHAMIA CHADEMA
 
Magufuli hafai, mtu wa visasi sana na pia akikujia juu ujue hujatoa cha juu. Bara bara nyingi zipo chini ya viwango lakini hawarudii kuna nini hapo.

Mbagala na kule Sekenke , Singida zinarudiwa fuatilia utajua na zingine zaidi!
 
Magufuli alitakiwa sasa awe gerezani Ukonga kwa uhujumu uchumi!Aliwapa nyumba za serikali ndugu zake zilizojengwa na Nyerere kwa mikono yake(Kuna picha maktaba zinaonyesha Nyerere akibeba mchanga kwenye karai kuwapa mafundi akijenga nyumba za Oysterbay)Magufuli ndiye waziri anaye ongoza kwa kuitia hasara serikali((Rejea uamuzi wake alipogoma kutii amri ya mahakama na kubomoa kituo cha mafuta-Mwanza)

Kesi hii ilihujumiwa pindi Magufuli alipohamishwa Wizara na kupelekwa ardhi na ndipo ule ugonjwa wa serikali wa kutoshinda kesi ukaendelea, nahisi hata aliyeshinda kesi hiyo hajalipwa mpaka leo! Angalia Magufuli kasimamia ile kesi ya wavuvi haramu mpaka serikali imeshinda, so hata ile ya Mwanza tungeshinda lakini Ndo hivyo tena!
 
magufuli ni mwizi wa nyumba za serikali,arudishe kwanza

Yalikuwa ni maamuzi ya serikali nzima JK kipindi hicho akiwemo iweje umuhukumu yeye binafsi, yeye alitekeleza kama waziri mwenye dhamana! Au nawe ndo wale wanawahukumu kwa kuwaandika majina watendaji wa serikali badala ya kuishitaki serikali?
 
Jina lako linafanana nawe,ila nakuibia siri kwamba J.P.Makufuli hafai kuwa rais,sababu kubwa sana,huyu jamaa ni mtu wa kisasi sana.Namfahamu tangu akiwa TANROAD Morogoro.Si kila kinachong'aa kwako kinang'aa na kwa wengine.

Mkuu unatia kichefuchefu angalia tovuti ya bunge na pitia CV ya Magufuli uone kama aliwahi fanya kazi Morogoro ? Majitu mengine bana?
 
Sitompa kura yangu kwa kuwa miongoni mwa kundi la viongozi wachache wenye elimu bali wasiojali historia ya nchi hii kwa kuhusika kubadilisha "Old Bagamoyo Road" nakuwa "Mwai Kibaka"!!!!
 
Mkuu Magufuli hakuishia kuwagawia ndugu zake na jamaa zake tu, bali alikwenda mbali zaidi na kuzigawia nyumba ndogo zake. Mfano ulio hai ni ule wa nyumba aliyo mgawia DEMU wake aliyekuwa akisoma Geology hapa UDSM anayeitwa Sundi.

Mbali na kashfa ya nyumba Magufuli aliliingiza taifa hasara kubwa ya kupindisha barabara ya ki-mataifa na kuipitisha jimboni kwake Chato kinyume na ilivyokuwa imekusudiwa awali.

Achana na majungu

Mkuu barabara unayosema naijua sana na sikubaliani na hoja yako kwani feasibility study ilifanywa na consultant kutoka South Africa na ikaonekana economically feasible inayopita Chato kuliko Biharamulo na leo hii kila mtu ni mashahidi wa hili, lakini isitoshe consultant huyo huyo alishauri pia baadae ijengwe ile inayoelekea Biharamulo kwa vile ilikuwa premature kipindi kile ya Chato imequalify kujengwa, kinachoendelea sasa hivi ni pia ile iendayo Biharamulo inajengwa kwa kiwango cha lami na kandarasi najua yupo site!
 
Kwa muono wangu huyu bwana ndio anafaa kumrithi Kikwete, kwa Nchi yetu ilipofikia tunahitaji Rais mwenye msimamo na mbabe kama huyu jamaa, hatuhitaji tena mtu soft!!!!!

Mwambie magufuli arudishe nyumba za serikali alizowauzia vigogo wenzake na kusababishia serikali hii mzingo na hasara kubwa kwa viongozi wapya wa serikali ya mhe. Kikwete kuishi mahotelini kwa gharama kubwa.
 
Kwa mtu smart anayemjua Magufuli au anayejua sihasa hawezi kudhubutu hata kufikiria hivyo!!! pale hakuna kitu!anajua kucheza na media tu full stop!!! lakini kumpa nchi hapana...nitahama!! jamani kuongoza nchi siyo kukurupuka na kukaripia kwenye vyombo vya habari tu,kha! ni zaidi ya hapo...kweli wajinga ndio waliwao!

Je Dr.Mwakyembe anayesifiwa kila kukicha na vyombo vya habari naye mtasema anacheza na media?? Wabongo kazi kweli!
 
Mkuu unatia kichefuchefu angalia tovuti ya bunge na pitia CV ya Magufuli uone kama aliwahi fanya kazi Morogoro ? Majitu mengine bana?

Si kila waziri anaweza kuwa raisi wa nchi. Mhe. Magufuli ana uthubuti wa kupewa majukumu na kuyasimamia na si vinginevyo. Kwa misimamo yake bora abaki kuwa waziri kwani zaidi ya hapo anaweza kuongoza nchi kidikteta.
 
Mkuu unatia kichefuchefu angalia tovuti ya bunge na pitia CV ya Magufuli uone kama aliwahi fanya kazi Morogoro ? Majitu mengine bana?

Si kila waziri anaweza kuwa raisi wa nchi. Mhe. Magufuli ana uthubuti wa kupewa majukumu na kuyasimamia na si vinginevyo. Kwa misimamo yake bora abaki kuwa waziri kwani zaidi ya hapo anaweza kuongoza nchi kidikteta kwa ni kati watu wanaofikiri wajua kila jambo kitu ambacho ni hatari sana kwa kiongozi wa juu kabisa.
 
Kwanza nadini ya CCM hawezi kukubarika kwa sababu wanajua kuwa atawasumgua kwa kutaka kwake sifa anaweza kufanya kitu cha ajabu bila hata ya kufikiria. Wanaojua vizuri mwanza watakumbuka vituko alivyofanya wakati wa uvunjaji wa kituo cha mafuta cha MOIL, alilazimisha kuvunja matokeo yake serikali iliwalipa pesa nyingi sana wale wahindi wa CCM! Kwa kupenda kujipendekeza JP alipongeza safari za raisi JK pamoja na kujua fika zinaliingiza taifa kwenye ghalama zisizo za lazima hii yote ni kwa sababu huyu mheshiwa anapenda sifa sana so alijipendekeza kwa JK kwa kumpa sifa zisizo na tija kwa watanzania of which watanzania sidhani kama tunahitaji raisi wa style hii. Kwa visasi ndo mwenyewe kumbukeni issue ya fast ferry za Azam alozileta lake Victoria, JP alitaka kumkomoa Mwandosya kwa vile alikuwa amekula karamu ya ujio wa meli hizo hivyo JP akajua kumkomoa ni kugoma kusaini boti hizo kupitishwa kwenye barabara zake kwa kisingizio ni nzito wakati kuna mitambo ya migodini ni mizito mara mbili ya boti hizo kila siku inapitishwa kwenye barabara zake na sisi watz tukishuhudia. Kwa kifupi JP hafai hata kidogo kuwa raisi, ikumbukwe tena aliwahi kupigiwa kelele na wananchi wa Buziku kwenye moja ya mikutano yake jimboni chato,alichokifanya ni kuwaambia kwa kisukuma " Buta baba gete mtalaibona ilami maisha ging'we pyee!" kilichotokea ni kuipindisha barabara ya lami ilotakiwa kupita Buziku akalazimisha ipite Chato ili kuwakomoa wananchi hao....sasa jamani tunamjadiri kuwa raisi wa nchi mtu wa aina hii? Labda kwa vile ni demokrasia acha tumuweke tena raisi wa majaribio kama tulivyofanya 2005 & 2010.

1. MOIL nasikia kesi ilichakachuliwa pale wizarani pindi Magufuli alipohamishwa na kupelekwa ardhi na ndo maana wale wahindi hawakuruhusiwa kujenga tena pale, nafikiri kuna ukweli!

2. Fast Ferry za AZAM zisingeliweza kupita pale Ruvu kwa kuwa dimensions zake hazikucomply na mizigo iliyoruhusiwa kupita barabarani, hata madaraja hayakuwa na uwezo wa kupitisha mizigo huo mkubwa, hapa namtetea

3. Ile barabara ya Buziku, sasa hivi inajengwa kwa kiwango cha lami inaitwa Bwanga - Biharamulo, naijua sana barabara hii, so atalaumiwa labda kuchelewa kuijenga, lakini hata hivyo kule Biharamulo tayari kulikuwa na barabara ya Kagoma - Lusahunga 154 km ilikuwa inajengwa kipindi hii ya Magufuli inajengwa sasa Sibiu pengine una chuki naye binafsi!
 
Back
Top Bottom