Mheshimiwa Rais, kabla ya watoto kurudi shule, wewe toka kwanza nyumbani kwako Chato rudi ofisini Ikulu

Wewe inakuuma nini raisi akiwa Ikulu ndogo? Kakae ww ikulu kama imekua nongwa
Sio inatuuma nini. Magu alizunguka nchi nzima kuomba kura, hadi kupiga pushapu. Kapewa kazi anaanza kuleta za kuleta. Aliapa kuilinda katiba. Aende ofisini akapige kazi. Nyumbani ni nyumbani tu, hata nyumbani kwa rais. Kwani yeye ni rais wa maisha? Nyumba imejengwa iwe nyumbani, ikulu imejengwa iwe ikulu. Watu hilo hawaelewi
 
Umenena vema Sana Kaka. Asiwachuuze wanetu wakati yeye kajificha

Kabla ya kuzifungua hizi sule kuna matayalisho yanatakiwa kufanywa!!! Kuna suala la SAFE DISTANCING kwa jamaii je hili limeshuhulikiwa kabla ya shule kufunguliwa? Matamko ya viongozi kwamba waanze kusherehekea kwani corona imekwisha ni hatari sana kwa usalama wa nchi!!! Corona bado ni tishio duniani kote na tunashuhudia watu wanakufa kwa wingi nchi nyingine kwahiyo tuwe waangalifu na hawa wapenda sifa!!
 
Mimi sijui sababu lakini wapo maraisi kama Paul Biya wa Cameroon anaishi France kwa muda mrefu tu.Pia marehemu Raisi Felix Houphouet Boigny wa Ivory Coast alikaa sana France .
Labda iwe fursa kwa wenye mitaji kujenga mahotel ,kwa wageni wa Raisi.huko Chato.
 
Kwa mujibu wa sheria za nchi ofisi rasmi ya raisi ni Ikulu, Ikulu zozote zilizo ndani ya nchi na wala siyo nyumbani kwake.

Kwa sasa zaidi ya siku 50 Rais anafanyia kazi za nchi ndani ya nyumba yake huko Chato, sijajua yale mafaili confidential ya nchi anayaweka sebuleni kwake au dining room, hili hakuna anayelijua.

Hata hivyo raisi juzi kwenye hotuba ya kisiasa aliyoitoa akiwa madhabahuni alisikika akisema kuwa anakusudia kufungua vyuo maana anaamini nchini mambo ni shwari korona siyo tishio sana.

Mimi ningependa kumwambia ndugu rais kwamba, kabla ya kufungua vyuo rudi kwanza ofisini. Wakati akiwataka maelfu ya watumishi ambao ni waalimu warudi mashuleni kuchapa kazi basi ni muhimu naye akarudi katika ofisi ambayo kisheria ndiyo anayopaswa kufanyia shughuli za kiofisi.

Nyumba ya rais huko Chato siyo ya kwake peke yake, ni yake na mkewe. Mkewe ana haki ya kuchagua mtu gani aingie ndani ya nyumba hiyo, hata hivyo Ikulu siyo yake na mkewe kwa hiyo hawana haki ya kumkatalia mtu yeyote kwenda kupata huduma ya raisi au taasisi ya uraisi yenye ofisi zake Ikulu.

Kitendo cha raisi kufanyia kazi za nchi kwenye nyumba yake binafsi kinawanyima haki ya kupata huduma za kiofisi wananchi wengi wenye kutaka kupata huduma za kiofisi za raisi.

Kitu kingine ni kwamba nyumba ya raisi huko Chato haikujengwa makhsusi kuwa na hadhi ya Uraisi, haikuwekewa vifaa vyote vya ulinzi stahiki wa mtu anayekalia kiti cha rais, kwa hiyo ni security risk kwa rais kuendelea kukaa kwenye nyumba hiyo binafsi.

Kama rais anadhani Korona ipo under control atoke huko Chato kwenye nyumba ya mama yetu mama Janet aje kwenye nyumba ambayo wananchi wamemuweka afanye kazi zetu.

Ndugu rais uko nje ya ofisi kwa muda mrefu sasa, rudi ofisini!
Kwa Mujibu wa sheria ipi mkuu, ebu itaje hyo sheria na sisi mbumbumbu wa sheria tuijue
 
1589976249700.png
 
Ukipitia hoja za wadau humu utagundua tatizo la Tanzania sio viongozi ni wananchi.
 
Hao kina Bashite na JIWE wanatuambia tufanye kazi na tupige kazi kama kawaida huku tukichua tahadhari wakati wao wenyewe wamejificha,mimi mpaka nione wao kwanza wakifanya ziara kama awali na jiwe akirudi kula upepo wa bahari,kwenda kwenye vijiwe,kwenda kanisani kila jumapili kama ilivyo ada yake,bashite na yeye kuzunguka na comvoy yake mitaa yote ya Dar,wakifanya hivyo ndio nitaamini wanachomaanisha ila wakiendelea kujificha ficha press conference au kuonekana kwenye TV kila baada ya wiki mbili nitazidi kuchanganya na zangu akili za kuambiwa.
Hahaha...jf raha sana, haya katoka chimbo sasa semeni jingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom