Ufafanuzi wa na.3 Wanafunzi walinipa shida sana. Walitaraji kiwango cha juu sana kutoka kwangu. Walijua natokea mkoa wa nshomile. Nimwage ung'eng'e wa kufa mtu. Si unawajua hao jamaa? Fikiria kiingereza changu cha leo kilivyo. Wakati huo hata Uingereza sijaenda! Naongea neno moja la kizungu nalo pengine si sahihi. La pili la kisukuma na la tatu la kiswahili kwa lafudhi ya kisukuma. Hawanielewi. Siwaelewi. Hatuelewani. Natoa adhabu kufuru! Ndio wanazidi. Mwaka mmoja tu kama muongo mzima. Cha kufia nini? Wala sikufikiria maslahi nikalala mbele. Nyanza wakanipokea. Ualimu kama lugha haipandi acha kabisa.Very simple, nilikimbia ualimu kutokana na kutoelewana na Headmaster.
1. Mosi alikuwa akinisumbua Sana baada ya Mimi kugoma kuishi nyumba moja walimu wawili. Mimi napenda maisha ya kujitenga Sana.
2. Headmaster alikuwa akinisumbua nikae Ofisi moja tukiwa wengi, sikupenda hili na nilitaka nipewe ofisi yangu Kama alivyo yeye. Hata Ofisi ya chemistry nilishindwana na mwenzangu Mwl ................aliyekuwa mkuu wa idara. Pia mkuu wa idara ya Mathematics tulishindwana.
3. Wanafunzi walikuwa na kiburi mno na Mimi nina hasira. Lugola atawaambieni vizuri.
4. Masilihi duni na kutolipwa mishahara hata zaidi ya Miezi mitatu wakati wa Rais Mwinyi yalinikimbiza nikaondoka Sengerema secondary na kwenda kuwa Mkemia wa kiwanda mjini Mwanza.
5. Pamoja na hayo yoote nilifanikiwa kujenga nyumba ya vyumba vitatu slope yaani mabati flat dizaini ya banda. Headmaster na walimu wengine walinionea wivu Sana kwa kuwa Mimi nilijenga nyumba hiyo ya vyumba viwili na sebule.
Ni hayo tu.