Mheshimiwa Rais sidhani kama kupenda Kwako kila mara ' Kumtajataja ' hadharani TISS DG Dkt. Kipilimba ni sawa Kiuweledi

Na kweli wewe popoma, kama Rais mwenyewe anajulikana, sembuse dg tiss?! Nadhani ukikua utaelewa mambo ya aina hii, ma-dg wote wa tiss tangu enzi za mwalimu watu wanawajua mpaka wanakolala!! hebu kula erythromycine kidogo utulize kipindupindu.
MPE YA UTI
 
Ni kweli mkuu kuna logic flani ipo kwa usiri wa hawa watu.
Mfano mdogo tu idara hii ni only one ambayo ofisi zake hazitambulishwi, huwezi kukuta bango linalokuelekeza kwamba hapa au huku ni ofisi ya Usalama wa taifa.
Nilishawahi kumhoji jamaa kuhusu usiri wao na kazi zao mipaka yake ikoje.
Nikapewa maelezo kwamba shughuli zao zote ni Siri Ila Kwa wao watumishi akanieleza kwamba kuna public security officers na secret security officers.
Nilielezwa kwamba hawa public security officers mara nyingi inajumuisha wale watu wenye vyeo DSO,RSO na deputy ,DG na hata deputy.
Akanieleza kwamba hawa ni public kwani wanahudhuria shughuli nyingi za kijamii kulingana na muundo wetu wanakuwa karibu na ma dc na rc kama wajumbe wa kamati za ulinzi na Usalama hivyo mara nyingi hawatengwi wakati wa utambulisho.
Hawa published c security officers Kwa maelezo ni wachache.
Kwenye Idara watumishi wengi ni ma secret security officers hawa hata baadhi ya wenyewe Kwa wenyewe hawajuani, hawa unaweza ukakuta wamekuwa attached sehemu mbalimbali hata kwenye mabenki binafsi unaweza ukamuona mtu anafanya kazi za u benki officer kumbe pia ni tiss. Na benki husika hata haijui Hilo.
Hata hivyo kufahamika Kwa hawa watu zaidi kipindi hiki kunatokana na maendeleo ya teknologia ya mawasiliano sio kweli kwamba akina Nyerere au mwinyi alikuwa hawatembei nao,ma dg wa tiss wa vipindi hivyo, walikuwepo pamoja kwenye nyadhifa na shughuli mbalimbali za kiserikali na walikuwa wanawatambulisha Ila Kwa kuwa teknologia ya habari ilikuwa duni kipindi hicho watu wengi walikuwa hawawafahamu
 
Mkuu mimi nimewacha kusoma threads zako kwa sababu ya fonts zako zinaniumiza macho. Labda unataka uwe unique humu katika style yako, nakumbuka niliwahi kukueleza hili na ukanikubalia kuwa mimi sikuwa wa kwanza kuleta haya malalamiko kwako kuhusu hili. Kwangu mimi nimeona kumbe hata JPM akishauriwa, suala la kukubali au kukataa ushauri ni haki yake ya msingi. Hence, hatuna haki ya kumjadili, kwa sababu hakupewa kura kuchukuwa ushauri au kujadiliwa na kila anayejisikia.
 
Mwanazuoni usiri ulikua zamani. USA mkuu wa CIA kabla ya kuchukua nafasi anawekwa kikaangoni na Senate. Watu ambao hawahitaji kujulikana ni wale waitwao MOLE. Hawa ni ma agent ambao hupelekwa kukusanya data kutoka mahali wanapofanya kazi. Hivyo ni lazima kuficha cover zao. Lakini huyu Kipilimba hakuna asiyejua kuwa ni mkuu wa ama Mkurugenzi wa Usalama wa TAIFA. Labda SHUSHUSHU mkuu wa JF Mheshimiwa Evarist Chahali atatusaidia kwa hili ama rafiki yake mtunzi wa kitabu cha Amazoni Yericko Kiboko Nyerere
 
Hoja ya mleta uzi, ilikuwa sabbu ya kumtaja taja...
na zaidi kuna wakati hata DDG naye alikuwa anamtaja..
so, kutajwa huku kunakuwa kunaleta viashiria gani ndani ya wasifu wa Rais na Nje ya wasifu wake???
 
Yawezekana ni hofu tu. Wakuu wa hizi taasisi.za usalama ni very public figures. Mara nyingi hasa kwa yale mataifa yenye demokrasia wanajulikana na kutakiwa kuwajibika kwa uma moja kwa moja au kupitia wawakilishi. Kinachokuwa siri ni wale operatives wa huku chini ambao hawatakiwi kujulikana au kuwa na uwajibikaji kwa uma ulio wazi sana. Mifano tunaiona hasa Ulaya na Marekani.

Ila kwa mataifa yenye uelekeo wa kikomunisti, kidikteta, kijeshi na kidini bado hofu zimewatawala. Mambo mengi huendeshwa kwa siri na hata hawa wakuu hujifichaficha. Sababu zinaweza kuwa pamoja na uhalifu mwingi hasa wa kisiasa unaotendwa na hizi taasisi (kwenye mataifa ya aina hii).

Watanzania inabidi tuendelee kupambana tusije tukaangukia kwenye udikteta au utawala wa kijeshi. Inatubidi tuendelee kudai katiba mpya na tasisi huru na zenye kuwajibika kwa uma na siyo kwa aliyewateua.

Uelekeo wetu ni kuwa taifa lenye maendeleo ya viwango vinavyotambulika na dunia na lenye kidemokrasia ya viwango vya nchi za Ulaya. Tusipende kukimbilia mambo ya kikomunisti, kidikteta, na mengine yanayoenenda kinyume na demokrasia.
 
KUMTAJA JAMAA HADHARANI HAKUNA MADHARA COZ HUYO NI KIONGOZI TU NA SIO OPERATIVE AGENT, HATA WA MATAIFA MAKUBWA HUYA WANAJULIKANA NA KWENYE MITANDAO WAPO ILA WALE WANAOTEKELEZA MAJUKUNU NDO HUWA SIRI KUBWA SANA,

KWA MFAN ISRAEL HATA RUBANI WA NDEGE ZA KIVITA SURA YAKE HUWA HAINONYESHWI HATA AKIHOJIWA ILA WAKUU WAO HUONEKANA.



Gina Cheri Haspel (née Walker, October 1, 1956) is an American intelligence officer serving as Director of the Central Intelligence Agency (CIA) since 2018
.


Alexander Vasilyevich Bortnikov (Russian: Алекса́ндр Васи́льевич Бо́ртников; born 1951) is a Russian official. He has been Director of the FSB since May 12, 2008.





Director of Mossad
Incumbent
Assumed office

January 2016Prime Minister Benjamin NetanyahuPreceded by Tamir Pardo9th National Security Advisor (Israel) In office
August 2013 – January 2016Preceded by Yaakov AmidrorSucceeded by Yaakov Nagal (Acting)





The new head of MI6 has been named as Alex Younger, a career spy who has worked in the Secret Intelligence Service (SIS) for more than 20 years. He is replacing Sir John Sawers, who announced he was stepping down after five years as SIS chief earlier this year.Oct 3, 2014

 
Yaani nyie jamaa kila kitu mnahisi mnatishwa mara mnaonewa.Mnajihesabia haki hadi mnapitiliza.
 
Kaka mimi hii kitu nishaiona muda sana na inanitatiza lakini naamini jiwe hajui namna jamaa wanavyotakiwa kufanya kazi,ndo hoja ya wale wanaodai jiwe hakuandaliwa na mfumo kuwa state man inapata nguvu.
Wakati mwingine akimuinua hadi mimi nayefatilia kupitia TV naona aibu. Kwa mfumo wetu na muundo wa idara sio kila mtu anatakiwa kuonekana /kujulikana, ndo maana wenzetu kama UK wana idara zaidi ya moja kama MI5 na MI6 au kule US wana FBI na CIA.
Naamini mkuu alivyoanza phase one kuna vitu vingi alikuwa hayuko familia navyo na kadri muda unavyoenda naona pase ya kujifunza inaongezeka, kumbuka hata aina ya speech na approach ya mambo.
Kupitia jukwaa hili tunafikisha ujumbe sehemu husika, amini kupitia hapa JF tunaelimisha na utaona changes.

Asante kwa uzalendo mkuu, unaipenda Tanzania.
 
Juzi nimehoji hivi ni lazima mtu kila siku apost thread humu?Kuna watu yaani wanapost vitu vya ajabu sana na wengi ni kutaka sifa za likes tu.Kiujumla jamaa ujuaji mwingi sana na akiambiwa ulichopost ni pumba anakuja juu kwa matusi.
 
Kuna vyeo vya idara ya usalama watu wanajulikana na siyo siri kama huyo DG wa usalama wapo hata mikoa RSO na wilayani DSO kila mtu anamjua na anajua kazi zake.Sioni kama ni tatizo hata pale anapotajwa hadharani.na hata huwa wana mikutano yao ya kimataifa duniani huko wanakutana na picha wanapiga za pamoja na zinasambaa pia mfano nakumbuka walikutano Kigali Rwanda wakuu wote wa Idara ya usalama kwa nchi za africa.
 
Nilikuja kumjua mkuu Wa tiss baada ya Ulimboka kunatwa na huyu Wa sasa lkn huko nyuma sikuwahi kuwasikia wala kuwaona nami nahitaji kuelewa zaidi kulikoni
 
Amtaje au asimtaje hadharani, watu wakihitaji kumjua watamjua tu. Ifikie wakati tuamini integrity ya watu wetu. Hata hivyo TISS ni chombo halali cha serikali kwahiyo hakuna ubaya mkuu wao kufahamika. Kazi zao kua siri ni sawa ila sio executives.
Pamoja na mambo mengine, Rais JPM anajivunia kazi aliyomkabidhi na anayoifanya DG wa TISS hususan kwa tempo na mfumo wake wa utawala.
Akiwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, nadhani pia ndiye aliyemshauri kuwa na walinzi wengi zaidi kuliko viongozi waliomtangulia. Hali halisi ya usalama wake, Rais Magufuli anahitaji ulinzi mkubwa sana wakati wote na popote dhidi ya wanaopinga juhudi za kuwaletea watanzania nchi ya viwanda, na asali na maziwa.
 
Nimefurahi kuskia maneno yako mkuu, naamini kama ulivyosema terms and conditions are applied. Pitia comments zote na yule mjinga wa Kilombelo aliyepo Ng'ambo akijibu nitag
 
Mkuu hivi Mzee hawezi kudhuliwa na wabaya wetu kupitia kupeana mikono?
 
Usalama wa Taifa si kila jambo ni siri, DG na Deputy wake ni lazima wajurikane.

Kwa mfano Usalama wa Taifa zonal wanafanyakazi na public, hata wewe kama una jambo la kushare nao unaweza kwenda ofisini kwao hawapo kwa kificho.

Kuna manyoka yamejaa BOT na TRA hao ndio siku zote hata familia yake haijuwi kama ni wa kitengo.
 
Wewe Husikii fahari kumtambulisha Baba yako aliyekuzaa?Aliyesababisha uwepo Duniani?Yaaani unajijua kabisa pasipo huyu(japo hakuwa yeye bali Taasisi) nisingekuwepo Duniani kutumbua maraha haya.
 
Kutambulika sio hoja mbaya, ni watumishi wetu wa umma. Ni sawa na Wapenzi wawili mke na mume tunawajua na tumeshuhudia mpaka ndoa yao, lakini wayafanyayo wakiwa faragha hatuyajui hivyo haijalishi huyu kumjua ilimuradi ayatendayo tunaona matokeo tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…