Mheshimiwa rais usitumie mabilioni ya maskini Watanzania kushinda uchaguzi au kujitetea pale unapokosea

Mheshimiwa rais usitumie mabilioni ya maskini Watanzania kushinda uchaguzi au kujitetea pale unapokosea

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
16,427
Reaction score
22,418
Tafadhali mheshimiwa rais tunaomba sana usitumie fedha nyingi za walipa kodi maskini kwa ajili ya kushinda uchaguzi. Watanzania wanahitaji maji ya kunywa, barabara angalau za vumbi, vituo vya afya, elimu ya msingi, nk.
Inasikitisha mno kuona mabilioni ya fedha ambazo zingetumika kuwasaidia watanzania zinakwenda kutumika katika kampeni za wewe kushinda uchaguzi.

Hivi kwani wewe mheshimiwa rais unagombea na nani wa kuhitaji mabilioni uli ushinde wakati kila kitu kipo chini ya amri yako kuanzia jeshi la polisi, tume ya uchaguzi, wasimamizi wa uchaguzi hadi bunge na jeshi la wananchi?

Kwa hakika hakuna haja ya kuweka picha yako kwenye kila kitu kuanzia redio, pikipiki, hadi ndege. Tunaomba utumie fedha hizo kuwaletea wananchi maendeleo mathalan vituo vya afya, maji ya bomba na hata barabara za changarawe.
 
Back
Top Bottom