Mheshimiwa Shabiby Aifagilia Bajeti Kuu, ampa tano Waziri wa Fedha, Akiwatetea Bodaboda

Mheshimiwa Shabiby Aifagilia Bajeti Kuu, ampa tano Waziri wa Fedha, Akiwatetea Bodaboda

Ambakucha

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2019
Posts
435
Reaction score
733
Wakati akiritirisha maoni, ushauri kwenye kuchangia Bajeti Kuu ya Serikali ya Mwaka 2025-2030, Mbunge wa Gairo kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Ahmed Shabiby amesema kuwa, kwa mara ya kwanza mwaka huu (2026) ameona bajeti iliyo bora sana katika bajeti nyingi alizowahi kushuhudia.
Mbunge huyo kutoka jimbo hilo lililopo ndani ya Mkoa wa Morogoro ambaye kila anaposimama bungeni huzungumza hoja zenye 'kutrendi' mitandaoni, alisema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan alipata jicho lenye hekima kumteua waziri makini, Balozi Khamis Mussa Omar (Mbunge) kuwa Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sababu ni mtu mwadilifu sana.
Mara nyingi mheshimiwa Shabiby amekuwa akiwashukia mafisadi na wala rushwa nchini, lakini safari hii katika mchango wake wa jana alisema anampongeza rais kwa kumteua waziri huyo huku akimpongeza waziri mwenyewe kwamba amekuwa bora katika wizara hiyo ambayo ndiyo moyo wa nchi yoyote duniani.
Aidha, sambamba na pongezi kwa rais na waziri, mbunge huyo aliipongeza kamati ya bunge ya bajeti, naibu waziri wa fedha na taasisi zote zilizomsaidia kutengeneza bajeti.
"Kwenye ukweli tutasema ukweli. Kama kuna kuna, kuna kona. Kama pako vizuri tutasema pako vizuri. Kwenye bajeti za nyuma, wabunge tumekuwa tukipiga kelele za misamaha. Mara utasikia fulani kapata msamaha. Fulani kapata msamaha, kasamehewa kodi.
"Lakini safari hii wizara imezingatia. Mafuta katoa ushuru. Pamba kalinda viwanda vyetu vya ndani vya nguo. Huo sasa ndiyo uzalendo na uadilifu. Siyo misamaha tu. Hii ni bajeti bora sana," alisema mheshimiwa Shabiby na kupigiwa makofi na waheshimiwa wabunge wenzake.
Katika hatua nyingine, akiendelea kuchangia bajeti hiyo, mbunge huyo ambaye pia ni mfanyabiashara mkubwa na mmiliki wa mabasi ya kisasa yanayojulikana kwa jina la Shabiby Line, aliwazungumzia Maafisa Usafirishaji Tanzania (maarufu kama bodaboda).
Alisema kwa sasa nchini, pikipiki ndiyo kipaumbele. Siyo anasa tena kama zamani.
Aliongeza kusema kuwa, sehemu kubwa ya nchi siku hizi, pikipiki ndiyo mkombozi. Siyo starehe tena (kama zamani). Akasema kuna maeneo mengi ya nchi, pikipiki zimekuwa kama Ambiulensi (ambulance) za kubeba wagonjwa kuwakimbiza hospitali kupatiwa matibabu.
Hivyo, mheshimiwa Shabiby akaomba wizara iwaondolee ushuru wa asilimia tano kwenye ununuzi ili vijana wengi waweze kumiliki pikipiki zao, isipokuwa kwa wale wanaomiliki pikipiki nyingi ndiyo wahesabiwe kuwa ni wafanyabiashara hivyo walipe kodi.
Lakini akasema kuwa, asilimia tisini (90%) ya bodaboda nchini hawana leseni za kuendeshea vyombo hivyo vya moto na siyo kwa sababu hawataki, bali gharama za kupata leseni hizo ni kubwa mno kwao.
Alisema ili dereva wa bodaboda aweze kupata leseni ya udereva anatakiwa kufanya mambo manne yafuatayo;
Kwanza; lazima alipe shilingi 100,000 itakayomuwezesha kusomea udereva chuoni.
Pili; lazima alipe shilingi 3,000 ili afanyiwe testi baada ya mafunzo ya udereva.
Tatu; lazima alipe shilingi 10,000 ili akatiwe leseni ya dereva mwanafunzi (Learner) maafuru barabarani kwa jina la L.
Nne; lazima alipe shilingi 70,000 kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa ajili ya kupata leseni kamili.
Mheshimiwa Shabiby akasema jumla ya malipo yote hayo ni shilingi 183,000 ambazo alisema anaamini vijana wengi hawana kiasi hicho cha pesa ili kuweza kupata leseni. Akaomba ikiwezekana leseni iwe shilingi 50,000 tu bila kuwepo mambo mengine na vijana wafundishwe kuendesha bodaboda na polisi jamii.
Aliongeza kuwa, yeye hajawahi kuona kijana yupo barabarani anafundishwa kuendesha bodaboda na wakufunzi wa vyuo husika (kama ilivyo kwa magari) hali inayodhihirisha kuwa, wengi wao hawana leseni.
Akasema: "Kwa hiyo naiomba Serikali iwapunguzie gharama hiyo. Na kwa sababu wako wengi nchini serikali itapata mapato mengi sana."
Hii ni mara ya pili kwa mheshimiwa Shabiby kusimama bungeni kuwatetea bodaboda kuhusu gharama kubwa ya upatikanaji wa leseni.
Screenshot_20260616_162241_Google.jpg
Screenshot_20260616_162449_Google.jpg
 
Ila samia amejua kuwapachika wzbr wenzake maeneo yote nyeti nyeti.
Kilichobaki na kuwa na IGP mzanzbar
 
Shabiby..ndo mana tajiri, jamaa anaufahamu ssana kijamii, kiuchumi. Sijui why wanamchukuliaga kama babu tale
Ila one day.
 
Back
Top Bottom