Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaama ajirusha kutoka ghorofani na kufa kutokana na kukosa ajira

Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaama ajirusha kutoka ghorofani na kufa kutokana na kukosa ajira

Zero Hours

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2011
Posts
12,942
Reaction score
18,669
Ally (25), mkazi wa Kiloleli wilayani Ilemela jijini hapa anayedaiwa kuwa na elimu ya chuo kikuu, amejirusha katika jengo la la Rocky City Mall na kufariki dunia.

Imeelezwa kuwa Musa alichukua uamuzi huo kutokana na kuwa na msongo wa mawazo, kukosa kazi.

Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa Desemba 21, 2018 kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza, Advera Bulimba amesema tukio hilo limetokea leo saa saba mchana.

Bulimba amesema kijana huyo alionekana akiwa amelewa kupita kiasi na tangu Desemba 16, 2018 na alikamatwa na kuwekwa kituo cha polisi Kirumba, kilevi kilipopungua aliachiwa.

Amesema katika uchunguzi wa awali marehemu alibainisha kuwa alikuwa na msongo wa mawazo kwa sababu ya kukosa kazi licha ya kuwa na elimu ya juu.

Bulimba amesema baada ya polisi kumuachia alikwenda kunywa tena pombe na baadaye kujirusha kutoka ghorofa ya tatu na kukutwa na pombe kali na ugoro.

“Uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa kijana huyo amesema amejiingiza kwenye ulevi na asilaumiwe mtu yeyote.

Amesema amechukua uamuzi huo yeye binafsi, pia akidai yeye ni masikini hana baba wala mama,” amesema Bulimba.

Amesema mwili umehifadhiwa hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi licha ya kutotaja jina la hospitali hiyo.

Bulimba amesema, maandishi aliyokutwa nayo marehemu yalisomeka kwamba “yeye ana shahada sayansi ya kompyuta aliyoipata Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM).”

Chanzo:Mwananchi.

Police wamesomba Picha zimekataa kuupload. Ila nimeattach kwenye comment no 6 na 7.
 
Umefanikiwa kuanzisha uzi...
Sasa unaweza kuujazia nyama kidogo uzi wako ili hadhira wapate taarifa wanayostaili...
 
C54AB7C0-8CA5-45DB-ACA4-3157D5DB9562.jpeg
 
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza.

Police wamesomba waliokuwa wanapiga picha.

Habari kamili inakuja. Picha zimekataa kuupload. Ila nimeattach kwenye comment no 6 na 7.

Moja wapo laweza kuwa jawabu sahihi:

1. Kagundua ana tatizo la Nyuzi la Gitaa la ' Dally Kimoko '.
2. Kafumania Demu wake ' Wanamume ' wakifanya yao kwa Kusimamia Ukucha
3. Masela wamemkuta na Demu wa mwenzao kisha wakafanya yao na kwa msaada wa ' Video Shooting '
4. Stress za Maisha ( japo tupo wenye hizo Stress lakini bado tunakomaa tukiamini kuwa ipo Siku tutatoboa tu )
5. Kasababisha Kifo au hasara Kubwa mahala
6. Karogwa
7. Uwendawazimu wa ghafla umempata

R.I.P sana Marehemu.
 
Back
Top Bottom