Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaama ajirusha kutoka ghorofani na kufa kutokana na kukosa ajira

Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaama ajirusha kutoka ghorofani na kufa kutokana na kukosa ajira

ngoja ni hakiki hii taarifa lakini huyu kijana ni kama nimemfananisha,sio mshikaji wangu kweli anayeishi geita.
 

Moja wapo laweza kuwa jawabu sahihi:

1. Kagundua ana tatizo la Nyuzi la Gitaa la ' Dally Kimoko '.
2. Kafumania Demu wake ' Wanamume ' wakifanya yao kwa Kusimamia Ukucha
3. Masela wamemkuta na Demu wa mwenzao kisha wakafanya yao na kwa msaada wa ' Video Shooting '
4. Stress za Maisha ( japo tupo wenye hizo Stress lakini bado tunakomaa tukiamini kuwa ipo Siku tutatoboa tu )
5. Kasababisha Kifo au hasara Kubwa mahala
6. Karogwa
7. Uwendawazimu wa ghafla umempata

R.I.P sana Marehemu.
Huwa unajisifu kwa akili ambazo huna lakini kuwa na staha ya kawaida tu.. Likes zinaishia jf ila ulichokifanya wala hakitobagua kuwa ID ni fake au real.. Mungu akusamehe lakini
 
sasa hakuna njia nyingine ya mtu kujiua mpaka ujitupe kutoka ghorofani au ndio matajiri wanatambika hivi siku hizi au labda ni kifafa
 
Ally (25), mkazi wa Kiloleli wilayani Ilemela jijini hapa anayedaiwa kuwa na elimu ya chuo kikuu, amejirusha katika jengo la la Rocky City Mall na kufariki dunia.

Imeelezwa kuwa Musa alichukua uamuzi huo kutokana na kuwa na msongo wa mawazo, kukosa kazi.

Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa Desemba 21, 2018 kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza, Advera Bulimba amesema tukio hilo limetokea leo saa saba mchana.

Bulimba amesema kijana huyo alionekana akiwa amelewa kupita kiasi na tangu Desemba 16, 2018 na alikamatwa na kuwekwa kituo cha polisi Kirumba, kilevi kilipopungua aliachiwa.

Amesema katika uchunguzi wa awali marehemu alibainisha kuwa alikuwa na msongo wa mawazo kwa sababu ya kukosa kazi licha ya kuwa na elimu ya juu.

Bulimba amesema baada ya polisi kumuachia alikwenda kunywa tena pombe na baadaye kujirusha kutoka ghorofa ya tatu na kukutwa na pombe kali na ugoro.

“Uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa kijana huyo amesema amejiingiza kwenye ulevi na asilaumiwe mtu yeyote.

Amesema amechukua uamuzi huo yeye binafsi, pia akidai yeye ni masikini hana baba wala mama,” amesema Bulimba.

Amesema mwili umehifadhiwa hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi licha ya kutotaja jina la hospitali hiyo.

Bulimba amesema, maandishi aliyokutwa nayo marehemu yalisomeka kwamba “yeye ana shahada sayansi ya kompyuta aliyoipata Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM).”

Chanzo:Mwananchi.

Post no.288 ya huu uzi, kuna mdau ametuma clip anayodai ni ya hili tukio.

Kwakweli video hiyo japo ni fupi tu,lakini ukiangalia, inasikitisha na kuumiza sana!
     
 
Nimemkumbuka marehemu Mohamed Bouazizi(graduate) wa Tunisia aliejua kwa kujichoma moto baada ya askari wa Jiji huko Tunisi nchini Tunisia, kukamata mali zake alizokuwa anauza kama mmachinga (street vendor) kutokana na kukosa ajira, tukio liliopelea maandamano ya kuwang'oa madikteta katika nchi kadhaa za kiarabu(Arab Spring) kwa kuanza na aliekuwa Raisi wa Tunisia,Ben Ali na baadae Mubaraka wa Misri kisha Gaddafi wa Libya.
 
Back
Top Bottom