Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaama ajirusha kutoka ghorofani na kufa kutokana na kukosa ajira

Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaama ajirusha kutoka ghorofani na kufa kutokana na kukosa ajira

Ana matatizo ya akili asisingizie ajira
Sure aiseeh.


Kuna watu wanapitia hali ngumu acha mchezo.

Mfano mtu hana ajira na bado ana maradhi yanamsumbua. Sembuse yeye huenda alikuwa mzima wa afya.

Haya ndio madhara ya ukisoma ili uajiriwe.

Mtoto wa kiume ni kupambana mpaka mwisho dhambi sana kukata tamaa.
 
RIP Kijana Ally.
Mungu aiweke tuu roho pema peponi.
Haya ni matokeo ya watu kuvamia fani, kwenye ulimwengu huu wa compyuta, mtu una degree ya computer science unasubiri kuajiriwa?.

Kifo hiki ni wake up call vyuo vyetu vikuu vipunguze kufundisha theory, twende kwenye kufundisha skills mtu akihitimu anakuwa equipped with skills na kujiajiri badala ya kutegemea kuajiriwa.

Kwenye masomo technical tufuate system ya Ujerumani ya apprentiship au uanagenzi, watu wakimaliza shule wanaanzia apprentiship program wakiisha
onyesha uwezo ndipo anaripoti chuo.
P
 
Ndio ujiue jamani? Usomi wake umemsaidia nini, alikuwa anatambua kabisa kuwa ajira ni ngumu..ameshindwa kujiajiri mwanaume mzima?
Mama kuna wengine wanakosa option kabisa. Wengine wanaamua kuwa wanawake tu wapate chochote kitu.
Sema marehemu hakujiongeza. Kusoma sio sababu ya kuajiriwa fani yake. Kuna wenzie saidia fundi hawakosi elfu 10 kwa siku
 
Kwa kweli Kukosa pesa inauma sana kwa kijana wa kiume sababu unahisi kama hauna thamani yeyote hapa ulimwenguni.
Lakini amekosea kujiua angetafuta ata mkopo akaanzisha biashara .
kujiua ni dhambi kubwa sana sababu unakua umekata tamaa na uwezo wa mungu kuwa hawezi kukutoa katkia tatizo ulilonalo
 
Back
Top Bottom