Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaama ajirusha kutoka ghorofani na kufa kutokana na kukosa ajira

Haya Ndio Matatizo Ya Mfumo Wa Elimu Ya Kwetu Tumejengwa Au Kutayarishwa Kuajiriwa Tu Baada Ya Kuhitimu Elimu Zetu! Hata Wale Wanaosomea Masomo Ya Sanaa, Biashara Nao Wanatoka Wakijua Wanaenda Kuajiriwa Mwisho Wa Siku Ndio Hayo Ya Kujiua Au Ulevi Wa Kupindukia, Unakuwa Na Msongo Wa Mawazo Unaharibika Kisaikolojia. Elimu Imekupa Maarifa, Imepanua Uelewa Wako Wa Kufikiri Na Kutatua Matatizo Itumie Kufanya Mambo Mengine Kama Kilimo,biashara, Ufugaji, Sanaa Nk. Unaanzaje Kujiua Kijana Mdogo Tena Mwenye Elimu? Ni Upumbavu.
 
Ni muda muafaka wenye utaalamu wa afya ya akili (mental health) waione fursa na kufungua vituo vya ushauri na tiba mbadala (therapy).

Watanzania kama zilivyo nchi nyingi wanamatatizo mengi kama msongo wa mawazo (depression), kukata tamaa, kuvunjika moyo na matatizo mengine yanayosababishwa na changamoto za maisha. Hivyo kukiwa na sehemu za kuwatia moyo na pengine kufunguka matatizo ya ndani inasaidia kupata unafuu (heal) na maisha yanasonga.

Mara nyingine mtu akiwa na changamoto anaona kama wote wanaomzunguka hawafai na wanamhujumu hivyo hawezi kuwaeleza yanayomsibu. Hatimae akili ikishindwa kuhimili anaona hakuna namna anafikia maamuzi ambayo sio mazuri.
 
Hii ni habari mbaya sana kwa serikali ya CCM baada ya kushindwa kuajiri kwa miaka 8 sasa....mnataka wasomi waliohitimu wakale wapi? Waingie kwenye siasa? MiCCM ni mijitu ya ajabu sana.
 
Popoma hizo sababu namba 1 na 2 ndo zinawezekana zaidi kwa mtu wa umri huo.
 
Mimi Tumaini Geofrey Temu limbukenitutababanana humuhumu nilisha tibiwa kichaa niwemuachia nyie na raisi wenu,, 2020.. Mrema agustino wariri mkuu Mama Maria Malkia Amitipal Sing Bhogal,,,
Temu akili bado haijakaa sawa hebu rudi tena ukatibiwe au Mirembe ipo hapa Nchini, mwenzako Mrema si Waziri Mkuu tena ni Boss wa Parole . Mama Maria kwa sasa yupo Msasani
Duh kazi kwelikweli vijana watajimaliza awamu hii
 
1. Kama kweli polisi walibaini ana msongo wa mawazo na wakamwacha basi walipoteza weredi katika kazi yao.


2. Watalaam wa Counselling waichungulie hiyo fursa ya msongo wa mawazo na kuanzisha ofisi ili watoe huduma hiyo kwa hitaji na kuajiri wengine
 
Hii ni habari mbaya sana kwa serikali ya CCM baada ya kushindwa kuajiri kwa miaka 8 sasa....mnataka wasomi waliohitimu wakale wapi? Waingie kwenye siasa? MiCCM ni mijitu ya ajabu sana.
Serikali tangu imeingia madarakani imeajiri watumishi 6000's only,ajabu sana yaani on avarage inaajiri watumishi 2000's/year wkt wasomi ni maelfu wanaotoka ma vyuoni huko.
 
Mmmhhh! Sidhani kama angekosa kitu cha kufanya; kuna uwezekano mkubwa alikuwa anachagua ajira ndiyo pale anayoitaka haitokei.
Mbaya zaidi kuona pombe ndiyo suluhu ya alichokuwa akiwaza; wahenga walikwisha sema pombe si chai. Makosa ni yake mwenyewe kwa kuchukua uamuzi dhaifu mno.
 
Haya matukio yametokea awamu hii kwa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…