Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaama ajirusha kutoka ghorofani na kufa kutokana na kukosa ajira

Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaama ajirusha kutoka ghorofani na kufa kutokana na kukosa ajira

Hao wengi wao wakiwa chuo wanatembea vifua mbele wakiamini wakimaliza tu ni ajira..rafiki yangu alidunda mtaani miaka mitatu na degree yake ya uchumi aliyoipata kwa shida sana pale saut kutokana na hali duni ya wazazi wake..leo hii yupo ofisi ya makamu wa rais..sasa angejiua ingekuwaje.. huyo ameathiriwa na ukosefu wa pesa za pombe alizojifunzia kunywa chuo kupitia boom.
 
Msomi huyo.
R.I.P.
Ila komputer studies unaweza ukang'amua kwenye theory ila kivitendo kama haujui ni haujui, sio kama sheria unaweza zuga na vijimaneno watu wakakuona kichwa kumbe hamna kitu.
 
Bwana ametoa na bwana ametwaa...ss ndugu zako wa sayansi ya kompyuta tutaendeleza mapambano ya ajira
 
Kwa sasa kampuni yako/yenu inapumilia mashine , mpaka 2020 labda utakuwa na wewe umeanza kuelewa maamuzi ya Ally, RIP Ally
RIP Kijana Ally.
Mungu aiweke tuu roho pema peponi.
Haya ni matokeo ya watu kuvamia fani, kwenye ulimwengu huu wa compyuta, mtu una degree ya computer science unasubiri kuajiriwa?.

Kifo hiki ni wake up call vyuo vyetu vikuu vipunguze kufundisha theory, twende kwenye kufundisha skills mtu akihitimu anakuwa equipped with skills na kujiajiri badala ya kutegemea kuajiriwa.

Kwenye masomo technical tufuate system ya Ujerumani ya apprentiship au uanagenzi, watu wakimaliza shule wanaanzia apprentiship program wakiisha
onyesha uwezo ndipo anaripoti chuo.
P
 
Hawachelewi kumwita mchochezi
Nimemkumbuka marehemu Mohamed Bouazizi(graduate) wa Tunisia aliejua baada ya askari wa Jiji huko Tunisi nchini Tunisia kukamata mali zake alizokuwa anauza kama mmachinga kutokana na kukosa ajira tukio liliopelea maandamana ya kuwang'oa madikteta katika nchi kadhaa za kiarabu(Arab Spring) kwa kuanza na aliekuwa Raisi wa Tunisia,Ben Ali na baadae Mubaraka wa Misri kisha Gaddafi wa Libya.
 
Ally (25), mkazi wa Kiloleli wilayani Ilemela jijini hapa anayedaiwa kuwa na elimu ya chuo kikuu, amejirusha katika jengo la la Rocky City Mall na kufariki dunia.

Imeelezwa kuwa Musa alichukua uamuzi huo kutokana na kuwa na msongo wa mawazo, kukosa kazi.

Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa Desemba 21, 2018 kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza, Advera Bulimba amesema tukio hilo limetokea leo saa saba mchana.

Bulimba amesema kijana huyo alionekana akiwa amelewa kupita kiasi na tangu Desemba 16, 2018 na alikamatwa na kuwekwa kituo cha polisi Kirumba, kilevi kilipopungua aliachiwa.

Amesema katika uchunguzi wa awali marehemu alibainisha kuwa alikuwa na msongo wa mawazo kwa sababu ya kukosa kazi licha ya kuwa na elimu ya juu.

Bulimba amesema baada ya polisi kumuachia alikwenda kunywa tena pombe na baadaye kujirusha kutoka ghorofa ya tatu na kukutwa na pombe kali na ugoro.

“Uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa kijana huyo amesema amejiingiza kwenye ulevi na asilaumiwe mtu yeyote.

Amesema amechukua uamuzi huo yeye binafsi, pia akidai yeye ni masikini hana baba wala mama,” amesema Bulimba.
Amesema mwili umehifadhiwa hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi licha ya kutotaja jina la hospitali hiyo.

Bulimba amesema, maandishi aliyokutwa nayo marehemu yalisomeka kwamba “yeye ana shahada sayansi ya kompyuta aliyoipata Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM).”
     
Mungu amuondolee adhabu zoote
 
Moja,Hana ajira hana pesa ila kalewa chakali.

Pili, polisi siku hizi wanakamata walevi na kuwasweka ndani?? Pombe zikiisha wanarudishwa majumbani.
 
Hivi ukiwa na degree kama hiyo yake uende wizarani au kampuni yoyote uombe kazi ya kujishkiza mshahara uwaombe laki 3 per month hupati kweli ajira ?
Kuna kampuni ambayo ukiwaomba mshahara hata wa laki 2 na accomodation watakataa ?
Usijitoe akili, eti uende wizarani, uombe kazi utaje na mshahara ili wakupe kazi, unadhani ni rahisi tu kama unavyotamka
 
Aliyumba tu !watu tumekosa ajira lakini hatuna wenge na bado tunadunda na umasikini wetu.
 
Back
Top Bottom