Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaama ajirusha kutoka ghorofani na kufa kutokana na kukosa ajira

Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaama ajirusha kutoka ghorofani na kufa kutokana na kukosa ajira

Nimemkumbuka marehemu Mohamed Bouazizi(graduate) wa Tunisia aliejua kwa kujichoma moto baada ya askari wa Jiji huko Tunisi nchini Tunisia, kukamata mali zake alizokuwa anauza kama mmachinga (street vendor) kutokana na kukosa ajira, tukio liliopelea maandamano ya kuwang'oa madikteta katika nchi kadhaa za kiarabu(Arab Spring) kwa kuanza na aliekuwa Raisi wa Tunisia,Ben Ali na baadae Mubaraka wa Misri kisha Gaddafi wa Libya.

hahahaha..kumbukizi nzuri sana hii
 
Naweza kuwa nimekabili hali ngumu kuliko hata huyo jamaa.

Yani yeye hata hela ya pombe alikuwa nayo..

Na elimu alikuwa nayo... So tumaini pia lilikuwepo.
So unachotaka kusema ni kuwa mtu ukiwa huna hela ya pombe ndio unastahili kujiua ??

Hivi unaelewa maana ya depression ?? Huu ugonjwa huwa hauchagui tajiri au masikini. Marekani huko depression inaua watu kila uchao. Depression imepelekea huko marekani mpaka watu wanashambulia wenzao kwa bunduki wanazomiliki kisha wengine kujiua.

Tatizo ni kwamba nchi zetu za kifukara mambo kama haya huwa hawayatilii maanani kama wewe unavyotumia hoja mfu kuongelea hili suala. Badala ya kujikita kwenye ISSUE zilizomuua Mmejikita kwenye WASIFU wa marehemu.
 
Computer Science Graduate wa Mlimani kashidwa hata kupata kazi ya kufundisha kwenye hivi vyuo vya Diploma na Certificates? maana vyuo vingi vinahitaji waalimu wa IT; sina uhakika kama hata walimu hawa wameshajaa kote.

Hapa hapo tuseme Bwana ametwaa? Unless kuna sababu nyingine lakini kama ni ya kukosa ajira si uamuzi sahihi.
usiseme kakosa kufundisha chuo vyeti vya diploma kama GPA haikuwa 3.8 and above unadhani ungefanya vipi application.Lakini bado amekosea sana kuutoa uhai wake
 
Hivi mkuu unaishi Tanzania gani hio ambayo eti unaenda wizarani tu unawaambia nipeni kazi mshahara laki tatu??

Kuingia tu geti la wizara hayo maswali utakayopigwa hapo mlangoni na walinzi hautarudi Tena aisee.
Nadhani haujawahi kwenda wizara yoyote hapa nchini.
Mwenyewe nimeshangaa sana huyu mtu, imgekuwa ni rahisi hivyo sidhani ka mtaani kungekuwa na jobless, wakat private sector kila siku zinapunguza watu, ye anasema eti uende wizarani utaje mshahara upewe kazi, bila kutangaza nafasi za kazi
 
Haya ndio matatizo ya kusoma theory mwisho wa siku no skills..
Degree za kwenye makaratasi Tanzania ni tatizo sana kwa sasa..

Serikali iamke na kujifunza hapa, tunawahitimu wengi ambao hawawezi kucompete internationally mwisho wa siku wanabaki kusubiri ajira kwenye kapu moja GOVT. Ukiwa na wahitimu wengi wenye uwezo wa kufanya kazi kimataifa inapunguza mzigo kwenye soko la ajira la ndani...
 
Waende google playstore, download metatrader 4, wajifunze na Demo account. Baada ya miezi michache, Wakiwa tayari wajiunge na real account iwe ajira yao ya kudumu.
Tunaongelea wataalamu wa computer science mkuu. Ukiweza kutatua shida za watu na kuwarahisishia maisha yao basi hao watu watakufanya uwe tajiri bilionea
 
Hivi ukiwa na degree kama hiyo yake uende wizarani au kampuni yoyote uombe kazi ya kujishkiza mshahara uwaombe laki 3 per month hupati kweli ajira ?
Kuna kampuni ambayo ukiwaomba mshahara hata wa laki 2 na accomodation watakataa ?
Sio rahisi kama ulivyoandika,tushawah omba volunteer full time buuure kabisa yan hautulipi chochote na bado tukakosa vile vile.
 
Nimemkumbuka marehemu Mohamed Bouazizi(graduate) wa Tunisia aliejua kwa kujichoma moto baada ya askari wa Jiji huko Tunisi nchini Tunisia, kukamata mali zake alizokuwa anauza kama mmachinga (street vendor) kutokana na kukosa ajira, tukio liliopelea maandamano ya kuwang'oa madikteta katika nchi kadhaa za kiarabu(Arab Spring) kwa kuanza na aliekuwa Raisi wa Tunisia,Ben Ali na baadae Mubaraka wa Misri kisha Gaddafi wa Libya.
So kwa hii akili unayoionesha humuunapenda na hapa iwe hivo sio
 
Kusema ukwel komputer science ni moja ya kozi niligundua ningeweza tengeza ajira nyingi sana,lkn ndo hivyo Umri umeenda, kwani naona fani sio tu ni nzuri lkn ina potential nyingi sana hasa kipindi hiki Cha sayansi na technology kwenye utawala Huu wa jiwe..issue ya huyo Musa ni nzitoo, kwa Sababu walio wengi pia hatujui background yake, ni kitu Gani alikuwa anapitia ...wanajamiiji forum tujifunze kutokudge vitu ambayo hatuvijui ukwel wake hasa inapotokea issue ya mtu kujitoa uhai..kukosa ajira sio suala dogo kama wengine wanavyofikiria..na kama hujawai pitia kipindi hicho unaweza sema lolote unalojiskia. Kwa kusema hivyo sio kwamba nakubaliana na maamuzi ya Musa hapana, Maamuzi aliyofanya Musa sio sahihi na nahisi alikosa exposure kama wengine walivyosema. Lkn pia inawzekana alikosa mtu wa Karibu kumfariji na kumtia Moyo... kwa mpande mwingine, Kuna wasiwai sana juu ya ukaribu wake na Mungu wake kwani kipindi Cha ukosefu wa ajira usipokuwa Karibu na Mungu wako unaweza fanya chochote, stress is one of the very bad disease, trust me kama hujawai pitia hutaelewa hii.
Hii iwe ni changamoto kwa serikali,kwamba Kuna bomu linatengenezwa...serikali isipo isipo jipanga vizuri na kila siku kupanda majukwaani kudanganyana, Mambo makubwa Zaid yanakuja..
Nawasilisha.
 
MKUU KILA NIKIIINGALIA HII COMMENT HUWAGA SINA MBAVUUUUU[emoji23][emoji23][emoji23], AMA KWELI WATZ WAMEVURUGWA, mkuu uliwaza nn kabla ya kucomment hahahaha
Mkuu kuna wadada wadangaji ukiwaanbia ugumu wa maisha hawaelewi kabisa. Kazi kunanga watu mitandaoni. Ukute anachomiliki ni Tako, Simu ya tecno au G-Tide na Danga la ambalo ni mume mtukufu wa MTu.
 
Inasikitisha sana watu wanaongea kimzaha mzaha eti kwanini asingejiajili

Mtaji angetoa wapi? Hata Desktop Computer yahitaji pesa.

Kusema kuwa Marehemu alikuwa ni Chizi ni kumkosea heshima.

Ukweli alikuwa na Depressions, Msongo wa Mawazo ulimsumbua Wanaojua Psychology watatuambia kuliko Hao waswahili hapo juu wanaodakia maneno bila kujua marehemu alipitia mangapi?

Kumjudge mtu bila kujua yamemsibu mangapi ni upimbi uliopitiliza. Musiisemee nafsi ya mtu huenda kuna yaliyomkuta zaidi ya hayo mliyosikia

La muhimu ni kumuombea tu uko aendako apate pumziko la amani kuliko kumkejeli kwa uamuzi aliochukua.
Issue ni kuwa hizo hela alizokuwa akipata kwa nini aliamua kulewea badala ya kufungua hata genge, baba nitilie au muuza mitumba kwa nini alikuwa akilewea?
 
Kwa elimu aliyokuwa nayo,angeenda ata shule ya kata akafundisha part time...na maisha yange songa,kuliko kuchukua maamuzi ya kujiua.
 
Hivi mkuu unaishi Tanzania gani hio ambayo eti unaenda wizarani tu unawaambia nipeni kazi mshahara laki tatu??

Kuingia tu geti la wizara hayo maswali utakayopigwa hapo mlangoni na walinzi hautarudi Tena aisee.
Nadhani haujawahi kwenda wizara yoyote hapa nchini.
Labda kwa kuwa ni Tanzania yetu mkuu
 
HOTUBA FUPI KUHUSU MAREHEM

marehem alikaliliii weeee, alivyo maliza madarasa yake akajitupa kutoka gorofani

Bwana ametoa bwana ametwaa, jina la bwana lihimidiwe
 
So unachotaka kusema ni kuwa mtu ukiwa huna hela ya pombe ndio unastahili kujiua ??

Hivi unaelewa maana ya depression ?? Huu ugonjwa huwa hauchagui tajiri au masikini. Marekani huko depression inaua watu kila uchao. Depression imepelekea huko marekani mpaka watu wanashambulia wenzao kwa bunduki wanazomiliki kisha wengine kujiua.

Tatizo ni kwamba nchi zetu za kifukara mambo kama haya huwa hawayatilii maanani kama wewe unavyotumia hoja mfu kuongelea hili suala. Badala ya kujikita kwenye ISSUE zilizomuua Mmejikita kwenye WASIFU wa marehemu.
Mkuu madai ni kwamba kajiua kwa kukosa ajira.
But nadhani ishu ni kukosa ustahimilivu kwenye changamoto.
 
Back
Top Bottom