Mi natoa ONYO: Kuna Member wa Humu JF ana mahusiano na mchumba wangu. Tusije Kulaumiana Bure

Mi natoa ONYO: Kuna Member wa Humu JF ana mahusiano na mchumba wangu. Tusije Kulaumiana Bure

Kama kweli wewe ni kidume mtaje mkware wako

Nyagei
 
[emoji38][emoji38] huyo mchumba nae hjiewi km yeye ni mchumba wa m2.? wanaume sk zote wakiona utelezi wanateleza tuu hawajali huko mbele watakumbana na nini[emoji2][emoji2] dili na huyo demu tyuu[emoji53].
Uliepewa onyo broh jichungulie[emoji22][emoji85][emoji126][emoji126][emoji126]
 
Nimelazimika kusema hili ingawa najua wengine mnaweza kukebehi na kunidhihaki. Haina shida nimeamua kusema iwe kama angalizo maana kuna siku nitakuja tu kufanya reference. Sisi wengine hatujui sana kuzungumza au kurushiana maneno. Hii naweka tu kama ushahidi ili nikimfanya mtu kama ambacho nilimfanya shababy mmoja mwaka 2015 tusilaumiane.

Mimi nina mchumba ambaye kwa sasa ni mwezi wa 5 nipo naye. Kazi zangu ni za safari safari sana, so kila wakati nakuwa safarini ili niandae mazingira mazuri ya maisha yetu ya ndo hasa ukichukulia ye mchumba wangu amemaliza chuo mwaka wa 2 sasa hana kazi. Yeye ana muda mwingi sana so anakuwa home na sometime mishe mishe zake ila ni muda sasa naona amezoeana na member mmoja humu ndani ambaye amekuwa mara nyingi akiuza sana chai na habari zake za ajabu ajabu. Ni mhuni na baradhuli tu huyo member wala si mtu wa staha hata kidogo mimi ni mtu mstaraabu sana na mpole.

Nilianza kuona kila mara huyo member akianzisha thread huyu mchumba wangu analike na anachangia sana na huwa akisoma anasoma anacheka mpaka machozi yanamtoka muda wote akiwa nami anajisahau anaaanza kusoma threads za huyo jamaa baadaye nikamwambia mi sipendi anavyokuwa occupied sana na huyo jamaa mpaka anajisahau anasema "ila wanaume wengine bwana yaani ukikaa na huyu kaka itakuwa mtu hata stress huana unacheka tu" hilo liliniudhi maana asili yangu mimi ni mtu ambaye nipo serious na sina sana stories hasa za kipuuzi puuzi kama za huyo member humu ndani za ngono na jinsi wanavyotendana na wanawake.

Siku moja kweli ananiambia hebu siku moja nasi tujaribu hii style ya .... nikashangaa katamka jina nikamwambia kwa upole kuwa kwa nini anakuwa obsessed na huyo jamaa mhuni na malaya?" akaniambia "aaah.. Nawe baby una mind vitu vidogo tu mtu mwenyewe hata simjui" juzi juzi hapa akawa ananambia unajua good girls wanapenda sana bad boys..sikutilia maanani lakini nlianza kuona mashaka pale nilipoona anasema anataka aonane na huyo mtuniliingia kwenye inbox texts zake jamiiforums nikakuta anawasiliana naye sana wanacheka wanataniana na sometime wanachat maneno mpaka huyu mchumba anasema ameloana hili lilinikwaza hasa anaposema "wee..naomba nikuone live maana una vituko sana"

Nimeamua kuwa hili suala niliweke wazi huyu dada mimi nlishamhudumia sana chuo mpaka amemaliza ni mimi nlikuwa natoa ada kumwonesha tu kuwa nipo serious pesa za kutoka kwa wazazi wake alikuwa anatumia kufanyia mambo yake na nilimruhusu nikamwambia basi aangalie kama anaweza zifanyia kazi flan ya kuzalisha, she didnt do anything progressive with the money.

Leo hii mwendawazimu mmoja humu ndani anataka kuja kufanya masikhara na mchumba wangu its ok..mi naweza kumwachia ila afaham atarudisha pesa zangu zote nlizotumia kama si direct bas itakuwa indirect najua kwa nini nasema hivi na simtishii...yeye si mwanaume?ajaribu tu kumgusa huyu mchumba wangu kimapenzi atanifahamu kuna post iliwekwa humu kama sikosei mwaka jana..Kuna mtu alifanywa kitu kibaya sana kudandia wake za watu gharama aliyolipa ilikuwa kubwa na mpaka sasa anaendeleakulipa toka mwaka 2015.

Nimetoa tu hili kama angalizo.
Duh ,,
 
Sio kwa biti hilo hahhahahahaha watu hawataki mchezo na hivi pesa ilivyokuwa ngumu kuipata halafu watu wanakuja kuchukua miliki za watu ngoja tuanagalie picha litaishia wapi.. Je steringi ata_survive mpka mwisho au ndiyo tusubiri part two
 
Ila sidhan kama huyo mpenzi anafaa kuwa a good future Mama.
Moja ya vipindi alitaka hata ikiwezekana a pretend basi ni kipindi hiki akiwa bado anaitwa Mchumba
 
angalia sana. tena nakwambia angalia sana. we unadhani ni mwanaume sana kuliko wengine. si ndiyo? nakwambia jiangalie watu kunyamaza usituone kama mafala. jiangalie maana utakuja kujilaumu sana hapo baadaye.... we si mbabe? unajua sana mapenzi? unajua kuchat na wanawake? haina shida bro. mi sijui matusi..ila endelea tu . endelea sana tu.
Gugume ni muhusika Mkuu aisee sina ubishi Juu ya hilo ila sio poa
 
nilishamema mwanzoni ni GuDume tuu huyu, masta umeona sasa povu la mwenye mchumba wake?
Inaonekana anatabia mbaya kwasababu ametajwa na zaidi ya watu watatu hivyo kuna ukweli kabisa na majibu yake kwa mshkaji ni ya dharau sana na kejeli mno
 
Back
Top Bottom