Miaka 10 ndani ya JF

Miaka 10 ndani ya JF

Siku mbili zilizopita RRONDO nimetimiza miaka kumi ndani ya JF. Wengi huwa wanauliza kwanini nimejiita RRONDO ni Rajon Rondo ambae nilikuwa nafananishwa nae kwenye basketball court.

Katika miaka hii 10 sijawahi kupigwa ban na haina maana ni mtakatifu basi tu inatokea. Nimepata marafiki wengi sana,connections za biashara kibao. Kifupi nilipojiunga JF mpaka leo nimepiga hatua.

Kiukweli nilijiunga 2006 au 7 enzi za Jambo Chat kama sijakosea, baadae mhusika mkuu akanishawishi nijiunge forum kwani kuna mijadala mizuri.

Ile ID ya enzi hizo niliiacha kwasababu nilijilipua sana kwasababu ya ujana. Ila Maxence Melo inabidi sasa niwe Platinum member kwani shingapi?

Happy New year everyone
Umenikumbusha Rajon Rondo wa wakati ule. Alikuwa na pasi za hatari, akikupiga hiyo fake sasa utatamani kuomba sub. Nini Imani nawe ulikuwa machachari kama yeye mpaka ukapewa hilo jina.
 
Back
Top Bottom