Miaka 10 ya Utumishi: Kumbukizi mbaya ya matumizi ya pesa isiyofutika katika historia ya maisha yangu

Dah....mi niiliyapitia kipindi naanza utumishi ilikuwa pombe pombe pombe na mimi hadi Leo bado sijakaa kwenye mstari ...!Mawazo chungu nzima kujitoa kwenye gambe Napo Ni ngumu...!Ila kidogo nimepunguza......
Unaweza kabisa kutoka kwenye mtego wa gambe, ukiamua tu unafanya mkuu
 
Mwenzako mi mpaka leo najuta kwanini sikuenda kusoma Diploma vyuo vya ufundi nikaenda Form 5. Mkuu, hili ntajilaumu maisha yangu yote.

Anyway, maji yameshamwagika. Fresh tu.
Hiyo njia waliitambua wachache, ndo imeshakula kwako mkuu
 
hahahahaha . . . hao ndugu nao nina wasi wasi na maono yao. Anyway pole sana mkuu. Hesabu za kimaisha ni jambo liliwashinda wengi tena kwa miaka mingi
 
hii ndio hulka ya vijana wengi, na tunaona ufahari sana kufanya ushenzi huu. Anyway, Mungu ni mwema ndio maana tunajitambua na kuacha upuuzi huu
 
It is never too late to start over especially when you realize you are in the wrong path. Hongera umeshtuka at age 32. Wengine wapo at 58 ila hawajashtuka bado
daah . . 58 na mtu hajashtuka tu ? anyway sishangai kwa sababu hata saa za kuamka hazifanani
 
nina miaka kama mi4 kazini
kinachoniuma ni kupoteza pesa kwenye biznz ambayo sikuwa na abc nayo😑😑😑😑
ulifanya biashara gani mkuu ? tupe uzoefu na sisi tujifunze kutokana na makosa ya watangulizi wetu
 
kweli andiko lake ni zuri sana, wengi tunapenda kulisoma kwa sababu lina clear lessons katika maisha yetu. Mimi nadhani angetuandikia season 2 yake, baada ya kujitambua alifanya nini kujikwamua, kutorudia makosa na hatua aliyopo na anachokifikiria kwa baadaye
 
Sio kwako tu hua nashauri Kama unauwezo wa kufungua miradi na una mtu sahihi wa kuisimamia fanya hivyo ila sio kuacha kazi completely. UTATESEKA ifanye Kazi yako kuwa chanzo kingine Cha mapato.
Ni kweli mkuu, sometimes tusikimbilie kuacha kazi. Tuzifanye kazi kuwa kama supportive instruments pale tunapokuwa tumesimama kiuchumi. Kimbia kimbia sio ishu sometimes
 
Na kweli hawa viumbe wanatutosa sana tukiwa hatuna kitu, tukizipata ile hasira tunawafagia tu
 
Usijali boss, tukipata mda
 
Na kweli hawa viumbe wanatutosa sana tukiwa hatuna kitu, tukizipata ile hasira tunawafagia tu
Daah . . . . inauma sana. Ni vema ungetusimulia season 2 ukatuelezea maendeleo yako mpaka sasa na unaionaje future yako angalau kwa miaka 10 ijayo
 
duuuh . . . . pole sana mkuu. Ndio ujana maji ya moto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…