Hujachelewa mkuu kwanza nikupongeze kwa kushtuka mapema.Mimi nilidhani hiyo tabia ni kujiendekeza lakini nimegundua katika hiyo stage ya kushika hela umri huo ni ngumu kuepuka vishawishi,miaka 8 iliyopita nilipata kazi arusha Mara tu baada ya kumaliza stashahada ya juu katika fani ya uhasibu nikiwa na umri wa miaka 24,Ukwel kazi ilinilipa vizuri kiasi ningeweza kufanya mambo Makubwa kwani kipato kilikua kinaruhusu,kama unavyojua totoz za kijenge,mushono,pinpoint bila kusahau babilon na maeneo mengine ya Arusha ilikua hatari,kuchukua fastjet kwenda Dar es salaam kula raha kitu cha kawaida sana,kupandisha ndege totoz kuja arusha kitu cha kawaida ,mitungi ndo usiseme .Mimi mwenyewe nilikua nakaa nakumbuka nahisi ni akili yangu ile au nilirogwa?lakini sasa nimeamua kusahau yaliyopita na kusonga mbele na maisha yanaendelea japo mambo si mazuri sana kama wakati ule....