Miaka 10 ya Utumishi: Kumbukizi mbaya ya matumizi ya pesa isiyofutika katika historia ya maisha yangu

Miaka 10 ya Utumishi: Kumbukizi mbaya ya matumizi ya pesa isiyofutika katika historia ya maisha yangu

Dah....mi niiliyapitia kipindi naanza utumishi ilikuwa pombe pombe pombe na mimi hadi Leo bado sijakaa kwenye mstari ...!Mawazo chungu nzima kujitoa kwenye gambe Napo Ni ngumu...!Ila kidogo nimepunguza......
Unaweza kabisa kutoka kwenye mtego wa gambe, ukiamua tu unafanya mkuu
 
Mwenzako mi mpaka leo najuta kwanini sikuenda kusoma Diploma vyuo vya ufundi nikaenda Form 5. Mkuu, hili ntajilaumu maisha yangu yote.

Anyway, maji yameshamwagika. Fresh tu.
Hiyo njia waliitambua wachache, ndo imeshakula kwako mkuu
 
Kipindi nipo chuo tunakula boom, kuna jamaa yangu mmoja akasema bwana hili boom nataka ligawa lazima nimlipie dogo ada, sijui nifanye mini nyumbani dah nikasema ngoja na miye niwasuprise nyumbani kwa kusema dogo nimlipie ada nifanye na baazi ya mambo

Mda wa likizo ya semester ya kwanza mwaka wa kwanza nimerudi home nikaanza kueleza nachotaka kufanya bi mkubwa akamwita baba njoo usikie mipango ya mwanao, mzee akanisikiliza akasema sawa ebu wasiliana na ndugu zako washirikishe suala lako kidume nikawashilikisha jibu nililopewa sikuamini mpaka nikabaki nashangaa maana sikuwa familia yetu bora sana ila kwanini waliniambia vile

Ndugu na wazazi waliambia sasa ni hivi we we unasoma haya majukumu ya kusomesha nini utayakuta tu sisi hapa tunataka uje na matokeo hatutaki kusikia umedisco wala nini hilo boom lako kale bata kula bata uwezavyo ila hakikisha hapa unakuja na cheti, wakanisisitiza ukikwama uko jiongeze maana hatuitaji hata mia yako hilo boom lako limalize kila kitu uko hapa tunaitaji cheti ukiugua sema, ila sijui huna hela ya kula sijui nini boom unalo wakamaliza

Bwana si niliambiwa boom nile bata nikaanza kula bata kweli kweli du yani wiki moja tu boom limekata unaanza msoto mungu wangu pass ndefu mala hivi mala vile yani chuo nikaanza jifunza kumbe pesa inataka nidhamu ila nikawa nasahau boom likitoka tu bata wiki moja hoi msoto tena huo ujinga ukaja stop mwaka wa tatu nikaanza heshimu boom bajeti zikaanza pangika bata nakula ila la kihesabu maaana najua likikata boom msoto

So chuo tukajifunza pesa inaitaji heshima totoz zipo, starehe zipo haziishi

Tulipofika makazini ukipata mshahara wala uwazi anasa maana unajua ukijifanya mwana kuyatafuta basi utayapata tu
hahahahaha . . . hao ndugu nao nina wasi wasi na maono yao. Anyway pole sana mkuu. Hesabu za kimaisha ni jambo liliwashinda wengi tena kwa miaka mingi
 
Aisee!

Hela ulioichezea inauma sana. Umenikumbusha mbali sana, naumia sana imeniletea mpaka Insomnia.

Ufahari, Umalaya, Ulevi vimeniletea hasara kubwa sana maishani. Muda niliopoteza sitoweza upata tena. Nilisanuka Ufahari na Pombe nikakatilia mbali. Umalaya nikapunguza kwa 99% hii 1% iliyobaki ni ugonjwa wangi na vitu vifupi vyeupe.

Sina ile hela tena lakini walahu nina amani. Pressure ndogo ndogo tu za kawaida basi.

Bandiko lako limenitonesha aisee
hii ndio hulka ya vijana wengi, na tunaona ufahari sana kufanya ushenzi huu. Anyway, Mungu ni mwema ndio maana tunajitambua na kuacha upuuzi huu
 
It is never too late to start over especially when you realize you are in the wrong path. Hongera umeshtuka at age 32. Wengine wapo at 58 ila hawajashtuka bado
daah . . 58 na mtu hajashtuka tu ? anyway sishangai kwa sababu hata saa za kuamka hazifanani
 
Andiko lako ni zuri sana, Kama litafanyiwa kazi litawasaidia wenfi sana. Wengi hatuna AKILI ya saving katk kidogo au kingi tunachopata.

48M + 15M = Kwangu ningehesabu Kama pensheni. Daaah . Take it easy jitahidi mwanao asifuate makosa yako. Mpende sana mkeo. Asingekuwepo ingekuwa chizi tayari.
kweli andiko lake ni zuri sana, wengi tunapenda kulisoma kwa sababu lina clear lessons katika maisha yetu. Mimi nadhani angetuandikia season 2 yake, baada ya kujitambua alifanya nini kujikwamua, kutorudia makosa na hatua aliyopo na anachokifikiria kwa baadaye
 
Sio kwako tu hua nashauri Kama unauwezo wa kufungua miradi na una mtu sahihi wa kuisimamia fanya hivyo ila sio kuacha kazi completely. UTATESEKA ifanye Kazi yako kuwa chanzo kingine Cha mapato.
Ni kweli mkuu, sometimes tusikimbilie kuacha kazi. Tuzifanye kazi kuwa kama supportive instruments pale tunapokuwa tumesimama kiuchumi. Kimbia kimbia sio ishu sometimes
 
Aisee , ulipata mkopo mkubwa sana. Mi ningeupata huo au hata nikiupata sasa hivi God willingly nitapiga hatua kubwa sana.
Anyway, asante kwa kushea mkuu ila umenifundisha mambo mengi sana. Kujitambua ni mzigo sana kwetu sisi vijana. Tukizipata lazima totoz tuzifagie kweli kweli. Ila wakati mwingine tunalipiza tu kutokana na machungu tunayopitia wanavyotutosa tukiwa majalala tunaumia sana. Sikulaumu kaka. It was more than a foolish age lakini hukuwa na jinsi. Uliwafagia sawa sawa kwa sababu ya hasira uliyokuwa nayo. Naamini kwa sasa umeshaiacha hiyo tabia. Like you said, ulikuwa ni ujana tu
Na kweli hawa viumbe wanatutosa sana tukiwa hatuna kitu, tukizipata ile hasira tunawafagia tu
 
kweli andiko lake ni zuri sana, wengi tunapenda kulisoma kwa sababu lina clear lessons katika maisha yetu. Mimi nadhani angetuandikia season 2 yake, baada ya kujitambua alifanya nini kujikwamua, kutorudia makosa na hatua aliyopo na anachokifikiria kwa baadaye
Usijali boss, tukipata mda
 
Na kweli hawa viumbe wanatutosa sana tukiwa hatuna kitu, tukizipata ile hasira tunawafagia tu
Daah . . . . inauma sana. Ni vema ungetusimulia season 2 ukatuelezea maendeleo yako mpaka sasa na unaionaje future yako angalau kwa miaka 10 ijayo
 
Hujachelewa mkuu kwanza nikupongeze kwa kushtuka mapema.Mimi nilidhani hiyo tabia ni kujiendekeza lakini nimegundua katika hiyo stage ya kushika hela umri huo ni ngumu kuepuka vishawishi,miaka 8 iliyopita nilipata kazi arusha Mara tu baada ya kumaliza stashahada ya juu katika fani ya uhasibu nikiwa na umri wa miaka 24,Ukwel kazi ilinilipa vizuri kiasi ningeweza kufanya mambo Makubwa kwani kipato kilikua kinaruhusu,kama unavyojua totoz za kijenge,mushono,pinpoint bila kusahau babilon na maeneo mengine ya Arusha ilikua hatari,kuchukua fastjet kwenda Dar es salaam kula raha kitu cha kawaida sana,kupandisha ndege totoz kuja arusha kitu cha kawaida ,mitungi ndo usiseme .Mimi mwenyewe nilikua nakaa nakumbuka nahisi ni akili yangu ile au nilirogwa?lakini sasa nimeamua kusahau yaliyopita na kusonga mbele na maisha yanaendelea japo mambo si mazuri sana kama wakati ule....
duuuh . . . . pole sana mkuu. Ndio ujana maji ya moto
 
Back
Top Bottom