Miaka 10 ya Utumishi: Kumbukizi mbaya ya matumizi ya pesa isiyofutika katika historia ya maisha yangu

Miaka 10 ya Utumishi: Kumbukizi mbaya ya matumizi ya pesa isiyofutika katika historia ya maisha yangu

Leo hii nilikua nawaza hadi kichwa kinauma..mimi najutia boom la chuo nililitumia vibaya Kuna sehemu niliambiwa ninunue kiwanja Cha laki 3 tu..nikapuuza..kwa Sasa Hilo eneo linauzwa m 10..kila nikiwaza ujinga huu naumia sana.
Nilipopata kazi yangu..nilikuwa nakaa kwa ndugu kwa mwaka mzima lakini sikutunza hata Mia..(ujinga mwingine nalifanya)

Lakini story yako imefutia hatia kumbe kunawaliofanya makosa kuliko Mimi .
Tujirekebishe tusonge mbele
Mkuu haya mambo ukiyafikiria yanauma sana
 
Kila kitu huja na makusudi yake kiongozi yaani mie nina umri kama wako mwaka wa tano kazini, hakuna jipya.

Nimekaa nimetafakari leo nikajiona msengerema sana, nimeamua kubadilika naacha anasa.
Sahihi kabisa.tuko wengi sema ndo kujifunza.asiyekubali kufel mahala hawez jifunza.
 
Kuna mda huwa tunafanya makosa mengi sana katika maisha tena mengine ya kujitakia kabisa ambayo ukiyakumbuka baadae unayajutia sana. Binafsi kama ningetumia mda vizuri ningekuwa mbali sana sana kimafanikio kuliko nilivo sasa.

Kipindi namaliza O' level baada ya matokeo kutoka nikapangwa Moshi Technical kwa elimu ya Advance, nikabadili kwenda Dar Es Salaam Institute of Technology (DIT) kusoma FTC kwa miaka 3, nilipomaliza tu nikaunganisha degree MIST, nikiwa semister ya kwanza na umri wangu wa 21yrs naelekea 22 mungu akawa upande wangu nikaajiriwa nikiwa kijana mdogo kabisa nikiwa na 21 kama technician katika moja ya taasisi inayolipa vizuri sana hapa nchini ikabidi niahirishe chuo kwa mda niingie kwenye ajira hii ilikuwa 2009 mwishoni, kwa kipindi hicho kwa hiyo level yangu nilikuwa nalipwa 840k kama mshahara kwa mwezi, bado kulikuwa na housing Allowance 240k,Transport allowance 200k, posho ya mawasiliano 60k, Lunch 150k na Extra duty ambayo hii tulikuwa tunaingiziwa wafanyakazi wote sawa kila mwisho wa mwezi 350k kwa kipindi hicho.

Ofisi ilikuwa inatoa mikopo kwa wafanyakazi wake wapya ya bila riba za kujengea nyumba, kwa level yangu kipindi hicho nilikopeshwa 48m na zikawa zinakatwa kwenye posho na sio kwenye mshahara. Kiukweli kitu ambacho ninakijutia mpaka leo nikikumbuka naumia sana basi ni miaka yangu 4 ya mwanzo kwenye ajira (2009-2012) nilipoteza pesa nyingi sana kwenye mambo ya kijinga kabisa na badala yake nikawa mtu wa hovyo sana kuliko kipindi chochote katika maisha yangu, nadhani umri na kutopata washauri wazuri pia kulichangia hili.

Nilipopangiwa kituo changu cha kazi nilipewa 3+m za kujikimu, karibia robo tatu za hizi pesa nilitumia kujivinjari na wasichana wa CBE waliokuwa wananitolea nje kipindi cha zamani na hata nilipopewa pesa ya mkopo wa ofisi sikuweza kufanya la maana kubwa la kuweza kujivunia japokuwa kiasi cha pesa katika huo mkopo nilitumia kuwajengea na kukarabati nyumba ya zamani ya wazazi na mwaka uliofuata nikakopa CRDB tena 15m kupitia mshahara wangu, kipindi nakopa hii pesa nilikuwa nakaribia kwenda likizo yangu ya mwaka na asilimia 80 ya hizi pesa niliitumia kwenye starehe na wanawake kwenye hoteli tofauti tofauti, Sasa nikawa nakatwa kwenye mshahara na posho zinakatwa kulipia madeni ya mkopo nikawa napata kiasi kidogo tu japo kwa matumizi ya kawaida kilikuwa kinatosha kwa kujibana ikizingatiwa wazazi nao tayari nilikuwa tegemeo lao, Nikaanza kuishi kwa kutegemea zaidi per diem za safari za kikazi.

Mwaka 2011 nilimpa mdada mmoja mimba alikuwa anamalizia diploma yake TPSC ikabidi nikae nae kama mke wangu hata hatukufanya harusi mwenyewe hakutaka kabisa japo wazazi wa pande zote walitaka tufunge harusi kanisani na sherehe ifanyike na kiukweli hata uchumi wangu ulikuwa hauruhusu hili nadhani wife alisoma upepo mapema , Nilimshirikisha Mkurugenzi wangu tulichoafikiana na mwenzangu kuhusu ndoa yetu na jinsi ya kupata cheti cha ndoa ili aweze kupata bima ya afya kupitia kazi yangu kama mke wangu halali, Wakubwa wanajuana bhana, usiku wa siku hiyohiyo ananipigia simu akinitaarifu tujiandae kesho yake anakuja kutuchukua tukasaini cheti cha ndoa nadhani ilikuwa ni RITA pale kama kumbukumbu zangu ziko sawa, lilikuwa ni jengo la ofisi za mkuu wa wilaya na mle ndani ndo kulikuwa na hizo ofisi za RITA sikujua hata kimelipiwa bei gani hicho cheti tulisaini tu na mashahidi zetu wawili wa pale ofisini akiwemo mkurugenzi then tukachukua vyeti tukamrudisha wife nyumbani mimi nikaingia kazini kuendelea na majukumu na hapa ndipo maisha mapya yalipoanza.

Mwaka 2012 nikahamishiwa Arusha na kupewa ruhusa ya kuendelea na masomo yangu ya shahada ATC kwa kujilipia mwenyewe, hapa pia ndipo nilipoanza kufeel ule ugumu wa maisha na kuona utofauti kati ya akili ya kikubwa na kitoto.Posho zina madeni, mshahara una madeni, safari zimepungua kwa sababu niko shule nina mke,mtoto wote wananiangalia mimi , maisha yalikuwa magumu sana kwangu kwa kipindi hicho huku nikiona wenzangu tulioajiriwa nao waliokuwa na umri mkubwa kidogo wao wakiwa mbali sana kimaendeleo na wakawa wananishangaa mimi kuona Inawezekanaje kuishi maisha yale ninayoishi na kwa namna ile tunayolipwa huku nikiwa sina majukumu mengi.

Baada ya kumaliza chuo 2015, ikabidi nijipange upya na mkopo ukawa umemalizikia na hata biashara sikuwa nayo pamoja na kukopa pesa zote hizo na kuugulia maumivu ya mkopo kwa miaka 5 na dogo nae anatakiwa aanze kindergarten na tayari ana mdogo wake mwingine😀😀 MAISHA HAYA. nikaanza kusuka mipango upya utafikiri ndio nimeanza ajira rasmi, Kibaya zaidi kipindi hicho wenzangu nilioajiriwa nao baadhi wako mbali sana, wana familia, wana nyumba nzuri, wana gari na biashara zao wakati mimi nimepanga chumba kimoja tu wakati huo mpaka namaliza masomo yangu ATC😎

Yale maisha na nikiwaangalia wenzangu itabaki kuwa kumbukumbu mbaya kichwani mwangu, uzuri nilitambua baadhi ya makosa yangu mapema nikajipanga upya nikiwa na akili ya kikubwa zaidi kuliko wakati ule, Japo sio sana ila somehow nime - win kidogo, lakini sio kama hatua walizo nazo wenzangu, ningekuwa na akili ya kikubwa kipindi kile ningekuwa mbali, mwaka jana nimetimiza miaka 10 ya utumishi wa umma nikiwa mwajiriwa na naelekea miaka 32 kiumri miezi michache ijayo bado ile kumbukumbu inagoma kabisa kufutika katika fikra zangu.unaweza kudhani natania lakini huu ndio ukweli kiasi ambacho nikikumbuka inaniuma sana hata kuandika hapa nakuwa kama napunguza mzigo wa maumivu wa ujinga wangu niliobeba moyoni

Pamoja na yote, mungu alinionesha mwanamke bora sana kwenye maisha yangu ambae hata sikuwahi kufikiria kumuoa ilitokea kama emergency tu hakuwa kati ya wasichana niliodumu nao kimahusiano kwa mda mrefu wala sikuwahi kumpenda, moyo wangu ulipenda kwingine kabisa na hata kwenye mipango yangu hakuwepo kabisa. Lakini kadri nilivoishi nae nimefahamu KWELI MKE BORA ANATOKA KWA MUNGU, mawazo yake yamebadili KABISA maisha yetu , kuna mda naona kabisa huyu kanizidi uwezo wa kufikiri hapa namzidi pesa tu, ni zaidi ya spiritual woman na mrembo haswa ni kivile tu wanaume huwa haturidhiki lazma tukaonje radha zingine nje.

Nashehekea miaka yangu 10 ya utumishi nikiwa na mtazamo mpya kabisa wa kuacha kazi ndani ya miaka 5 ijayo nijikite zaidi kuendesha miradi na biashara zangu niliyofungua ili kufikia malengo yangu niliyojiwekea. Kwa sasa ni baba wa familia, nina watoto kadhaa na mwanagu wa kwanza nimempata nikiwa na miaka 23 tu kwa sasa ana 8yrs anaelekea 9 miezi michache ijayo
Kitu nimegundua. Tuko wengi wa design yako. Ila kustuka mapema ndo jambo LA kumshukuru Mola.

Kitu mpk sasa nimejifunza. Kwa haya maisha ya vijana sisi wa karne hii omba sana upate mke anayejitambua na mwenye malengo na kujua life. Apo ata kama ushakosea kiasi gani bado utakaa sawa kupitia yeye.
 
Kitu nimegundua. Tuko wengi wa design yako. Ila kustuka mapema ndo jambo LA kumshukuru Mola.

Kitu mpk sasa nimejifunza. Kwa haya maisha ya vijana sisi wa karne hii omba sana upate mke anayejitambua na mwenye malengo na kujua life. Apo ata kama ushakosea kiasi gani bado utakaa sawa kupitia yeye.
Kabisa mkuu
 
Yani sijui atatokea rais mwingine tupige hela kama enzi za jk mimi kwa upande wangu nilikua nasafiri na ndege tu hadi nikawa nashangaa watu wanawezaje kusafiri na basi unachoka sana ha ha ha ha saizi nimeludi kule kuleee japo nna private car ila ni muoga ku drive njia kubwa
😅😅, kwasasa hata uchovu huuhisi eeh?
 



Ila wizara ya ajira ingekuwa inawapa semina vijana pale tu wanapoanza kazi kuhusu maswala ya matumizi ya mishahara na posho.

Taasisi kama Bank ABC wanavyosumbua rookies sasa kuchukua mikopo.

Lesson learned!!
 
Mimi nina miaka 5 kasoro miezi 2 katika utumishi wangu. Ninajutia mkopo wangu wa kwanza kufungulia duka. Ila huko nyie mnalipwa vizuri sana, ningekuwa huko kwa hii miaka 5 ningeacha kazi.
Nimejenga nyumba na kununua pikipiki moja tu. Maisha magumu mno kwangu mimi
 
Hongera Mkuu,

Unapokosea kuandika kwa kalam ya wino, bado umepewa nafasi ya kufuta ili uandike upya.

Unapokosea kuchora kwa pensel basi ufuto wa penseli upo ili urekebishe mchoro wako.

Kinapoharibika kitu bado iko nafasi ya kutengeneza.

Hivyo kwenye maisha kila mmoja amepewa 'second chance' yani nafasi ya pili ili kurekebisha pale alipokosea.

Hongera kwa kutambua hilo na nakutakia mafanikio na sasa utakua makini zaidi.
Kuna point imegusa hapa maisha yangu....hakika nafasi ya pili kurekebisha tumepewa..ukichezea hiyo you are finished
 
Mimi nina miaka 5 kasoro miezi 2 katika utumishi wangu. Ninajutia mkopo wangu wa kwanza kufungulia duka. Ila huko nyie mnalipwa vizuri sana, ningekuwa huko kwa hii miaka 5 ningeacha kazi.
Nimejenga nyumba na kununua pikipiki moja tu. Maisha magumu mno kwangu mimi
Pole sana Mkuu. Ni kwamba Biashara ilianguka ama?
 
Back
Top Bottom