Kipindi nipo chuo tunakula boom, kuna jamaa yangu mmoja akasema bwana hili boom nataka ligawa lazima nimlipie dogo ada, sijui nifanye mini nyumbani dah nikasema ngoja na miye niwasuprise nyumbani kwa kusema dogo nimlipie ada nifanye na baazi ya mambo
Mda wa likizo ya semester ya kwanza mwaka wa kwanza nimerudi home nikaanza kueleza nachotaka kufanya bi mkubwa akamwita baba njoo usikie mipango ya mwanao, mzee akanisikiliza akasema sawa ebu wasiliana na ndugu zako washirikishe suala lako kidume nikawashilikisha jibu nililopewa sikuamini mpaka nikabaki nashangaa maana sikuwa familia yetu bora sana ila kwanini waliniambia vile
Ndugu na wazazi waliambia sasa ni hivi we we unasoma haya majukumu ya kusomesha nini utayakuta tu sisi hapa tunataka uje na matokeo hatutaki kusikia umedisco wala nini hilo boom lako kale bata kula bata uwezavyo ila hakikisha hapa unakuja na cheti, wakanisisitiza ukikwama uko jiongeze maana hatuitaji hata mia yako hilo boom lako limalize kila kitu uko hapa tunaitaji cheti ukiugua sema, ila sijui huna hela ya kula sijui nini boom unalo wakamaliza
Bwana si niliambiwa boom nile bata nikaanza kula bata kweli kweli du yani wiki moja tu boom limekata unaanza msoto mungu wangu pass ndefu mala hivi mala vile yani chuo nikaanza jifunza kumbe pesa inataka nidhamu ila nikawa nasahau boom likitoka tu bata wiki moja hoi msoto tena huo ujinga ukaja stop mwaka wa tatu nikaanza heshimu boom bajeti zikaanza pangika bata nakula ila la kihesabu maaana najua likikata boom msoto
So chuo tukajifunza pesa inaitaji heshima totoz zipo, starehe zipo haziishi
Tulipofika makazini ukipata mshahara wala uwazi anasa maana unajua ukijifanya mwana kuyatafuta basi utayapata tu