Miaka 10 ya Utumishi: Kumbukizi mbaya ya matumizi ya pesa isiyofutika katika historia ya maisha yangu

Miaka 10 ya Utumishi: Kumbukizi mbaya ya matumizi ya pesa isiyofutika katika historia ya maisha yangu

Kuna mda huwa tunafanya makosa mengi sana katika maisha tena mengine ya kujitakia kabisa ambayo ukiyakumbuka baadae unayajutia sana. Binafsi kama ningetumia mda vizuri ningekuwa mbali sana sana kimafanikio kuliko nilivo sasa.

Kipindi namaliza O' level baada ya matokeo kutoka nikapangwa Moshi Technical kwa elimu ya Advance, nikabadili kwenda Dar Es Salaam Institute of Technology (DIT) kusoma FTC kwa miaka 3, nilipomaliza tu nikaunganisha degree MIST, nikiwa semister ya kwanza na umri wangu wa 21yrs naelekea 22 MUNGU akawa upande wangu nikaajiriwa nikiwa kijana mdogo kabisa nikiwa na 21 kama technician katika moja ya taasisi inayolipa vizuri sana hapa nchini ikabidi niahirishe chuo kwa mda niingie kwenye ajira hii ilikuwa 2009 mwishoni, kwa kipindi hicho kwa hiyo level yangu nilikuwa nalipwa 840k kama mshahara kwa mwezi, bado kulikuwa na housing Allowance 240k,Transport allowance 200k, posho ya mawasiliano 60k, Lunch 150k na Extra duty ambayo hii tulikuwa tunaingiziwa wafanyakazi wote sawa kila mwisho wa mwezi 350k na bado kukawa na safari nyingi sana ilikuwa ni kawaida kumaliza mwezi sijaona mlango wa ofisi, nakuwa safarini tu huko mikoani site kikazi napambana na per diem kila uchao.

Ofisi ilikuwa inatoa mikopo kwa wafanyakazi wake wapya ya bila riba za kujengea nyumba, kwa level yangu kipindi hicho nilikopeshwa 48m na zikawa zinakatwa kwenye posho na sio kwenye mshahara. Kiukweli kitu ambacho ninakijutia mpaka leo nikikumbuka naumia sana basi ni miaka yangu 4 ya mwanzo kwenye ajira (2009-2012) nilipoteza pesa nyingi sana kwenye mambo ya kijinga kabisa na badala yake nikawa mtu wa hovyo sana kuliko kipindi chochote katika historia ya maisha yangu, nadhani umri na kutopata washauri wazuri pia kulichangia hili.

Nilipopangiwa kituo changu cha kazi nilipewa 3+m za kujikimu, karibia robo tatu za hizi pesa nilitumia kujivinjari na wasichana wa CBE waliokuwa wananitolea nje kipindi cha zamani na hata nilipopewa pesa ya mkopo wa ofisi sikuweza kufanya la maana kubwa la kuweza kujivunia japokuwa kiasi cha pesa katika huo mkopo nilitumia kuwajengea na kukarabati nyumba ya zamani ya wazazi na mwaka uliofuata nikakopa CRDB tena 15m kupitia mshahara wangu, kipindi nakopa hii pesa nilikuwa nakaribia kwenda likizo yangu ya mwaka na asilimia 80 ya hizi pesa niliitumia kwenye starehe na wanawake kwenye hoteli tofauti tofauti, Sasa nikawa nakatwa kwenye mshahara na posho zinakatwa kulipia madeni ya mkopo nikawa napata kiasi kidogo tu japo kwa matumizi ya kawaida kilikuwa kinatosha kwa kujibana ikizingatiwa wazazi nao tayari nilikuwa tegemeo lao, Nikaanza kuishi kwa kutegemea zaidi per diem za safari za kikazi.

Mwaka 2011 nilimpa mdada mmoja mimba alikuwa anamalizia diploma yake TPSC ikabidi nikae nae kama mke wangu hata hatukufanya harusi mwenyewe hakutaka kabisa japo wazazi wa pande zote walitaka tufunge harusi kanisani na sherehe ifanyike na kiukweli hata uchumi wangu ulikuwa hauruhusu hili nadhani wife alisoma upepo mapema , Nilimshirikisha Mkurugenzi wangu tulichoafikiana na mwenzangu kuhusu ndoa yetu na jinsi ya kupata cheti cha ndoa ili aweze kupata bima ya afya kupitia kazi yangu kama mke wangu halali, Wakubwa wanajuana bhana, usiku wa siku hiyohiyo ananipigia simu akinitaarifu tujiandae kesho yake anakuja kutuchukua tukasaini cheti cha ndoa nadhani ilikuwa ni RITA pale kama kumbukumbu zangu ziko sawa, lilikuwa ni jengo la ofisi za mkuu wa wilaya na mle ndani ndo kulikuwa na hizo ofisi za RITA sikujua hata kimelipiwa bei gani hicho cheti tulisaini tu na mashahidi zetu wawili wa pale ofisini akiwemo mkurugenzi then tukachukua vyeti tukamrudisha wife nyumbani mimi nikaingia kazini kuendelea na majukumu na hapa ndipo maisha mapya yalipoanza.

Mwaka 2012 nikahamishiwa Arusha na kupewa ruhusa ya kuendelea na masomo yangu ya shahada ATC kwa kujilipia mwenyewe, hapa pia ndipo nilipoanza kufeel ule ugumu wa maisha na kuona utofauti kati ya akili ya kikubwa na kitoto.Posho zina madeni, mshahara una madeni, safari zimepungua kwa sababu niko shule nina mke,mtoto wote wananiangalia mimi , maisha yalikuwa magumu sana kwangu kwa kipindi hicho huku nikiona wenzangu tulioajiriwa nao waliokuwa na umri mkubwa kidogo wao wakiwa mbali sana kimaendeleo na wakawa wananishangaa mimi kuona Inawezekanaje kuishi maisha yale ninayoishi na kwa namna ile tunayolipwa huku nikiwa sina majukumu mengi.

Baada ya kumaliza chuo 2015, ikabidi nijipange upya na mkopo ukawa umemalizikia na hata biashara sikuwa nayo pamoja na kukopa pesa zote hizo na kuugulia maumivu ya mkopo kwa miaka 5 na dogo nae anatakiwa aanze kindergarten na tayari ana mdogo wake mwingine😀😀 MAISHA HAYA. nikaanza kusuka mipango upya utafikiri ndio nimeanza ajira rasmi, Kibaya zaidi kipindi hicho wenzangu nilioajiriwa nao baadhi wako mbali sana, wana familia, wana nyumba nzuri, wana gari na biashara zao wakati mimi nimepanga chumba kimoja tu wakati huo mpaka namaliza masomo yangu ATC😎

Yale maisha na nikiwaangalia wenzangu itabaki kuwa kumbukumbu mbaya kichwani mwangu, uzuri nilitambua baadhi ya makosa yangu mapema nikajipanga upya nikiwa na akili ya kikubwa zaidi kuliko wakati ule, Japo sio sana ila somehow nime - win kidogo, lakini sio kama hatua walizo nazo wenzangu, ningekuwa na akili ya kikubwa kipindi kile ningekuwa mbali, mwaka jana nimetimiza miaka 10 ya utumishi wa umma nikiwa mwajiriwa na naelekea miaka 32 kiumri miezi michache ijayo bado ile kumbukumbu inagoma kabisa kufutika katika fikra zangu.unaweza kudhani natania lakini huu ndio ukweli kiasi ambacho nikikumbuka inaniuma sana hata kuandika hapa nakuwa kama napunguza mzigo wa maumivu wa ujinga wangu niliobeba moyoni

Pamoja na yote, mungu alinionesha mwanamke bora sana kwenye maisha yangu ambae hata sikuwahi kufikiria kumuoa ilitokea kama emergency tu hakuwa kati ya wasichana niliodumu nao kimahusiano kwa mda mrefu wala sikuwahi kumpenda, moyo wangu ulipenda kwingine kabisa na hata kwenye mipango yangu hakuwepo kabisa. Lakini kadri nilivoishi nae nimefahamu KWELI MKE BORA ANATOKA KWA MUNGU, mawazo yake yamebadili KABISA maisha yetu , kuna mda naona kabisa huyu kanizidi uwezo wa kufikiri hapa namzidi pesa tu, ni zaidi ya spiritual woman na mrembo haswa ni kivile tu wanaume huwa haturidhiki lazma tukaonje radha zingine nje.

Nashehekea miaka yangu 10 ya utumishi nikiwa na mtazamo mpya kabisa wa kuacha kazi ndani ya miaka 5 ijayo nijikite zaidi kuendesha miradi na biashara zangu niliyofungua ili kufikia malengo yangu niliyojiwekea. Kwa sasa ni baba wa familia, nina watoto kadhaa na mwanagu wa kwanza nimempata nikiwa na miaka 23 tu kwa sasa ana 8yrs anaelekea 9 miezi michache ijayo

Mmmh technician hiyo hela ndo ulikuwa unapata kwa mwezi,shirika gani hilo?
 
Hicho kipato chako kinaonesha hukua mtumishi wa umma ( civil servant) tuulize sisi watumishi wa umma tukung'ate sikio vipato vyetu lazima utahoji naishije! Acha kaka halafu huu no mwaka wa tank hakuna ongezeko !utasikia mwenyewe anasema kama hutaki acha ikazi!!!!/ kwa kweli watu wamechakaaa mioyo
 
Mkuu jamaa aliajiriwa kwenye taasisi ya umma.. taasisi nyingi za umma kama tcaa, sua, muhas, toa, tra zina madaraja yao ya mshara ..ya grade zao za mishara siyo kama hizi common za waalimu
 
Andiko lako ni zuri sana, Kama litafanyiwa kazi litawasaidia wenfi sana. Wengi hatuna AKILI ya saving katk kidogo au kingi tunachopata.

48M + 15M = Kwangu ningehesabu Kama pensheni. Daaah . Take it easy jitahidi mwanao asifuate makosa yako. Mpende sana mkeo. Asingekuwepo ingekuwa chizi tayari.
 
Wazazi wanatakiwa sana kuangalia vijana wanaoajiriwa katika umri mdogo, ni bora hata kuwaelekeza kwa muda fulani juu ya matumizi ya pesa, saving and all na sio kukuona umeajiriwa basi ushakua mtu mzima wakati kiasi hicho kikubwa cha pesa za kila mara hujawahi kipata. Mwenyewe niliajiriwa at 22 first salary was 925k plus 1million per diem kila baada ya wiki 2 na hivi niliajiriwa mkoani yani kila ijumaa nipo airport naenda nyumbani kuona wazazi na mchumba. Looking back miaka mitano nyuma naona ningekuwa mbali sana tofauti na hapa nilipo leo maana umri unasonga na majukumu yanaongezeka
 
Hicho kipato chako kinaonesha hukua mtumishi wa umma ( civil servant) tuulize sisi watumishi wa umma tukung'ate sikio vipato vyetu lazima utahoji naishije! Acha kaka halafu huu no mwaka wa tank hakuna ongezeko !utasikia mwenyewe anasema kama hutaki acha ikazi!!!!/ kwa kweli watu wamechakaaa mioyo
Pole sana ndugu yangu, mimi nimeajiriwa na shirika la serikali yawezekana huelewi kuhusu utofauti wa maslahi kwenye taasisi za umma, ngoja nikupe mifano hai ya ndugu zangu wa karibu kabisa wanne ambao wameajiriwa hivi karibuni baada ya kutoka kapa huko JKT kupitia pale utumishi na wote wako cheo kimoja na elimu yao ni kidato cha nne tu, wameajiriwa taasisi tofauti, tuwape majina A,B,C na D.

"A" alitangulia kuajiriwa TPA mwaka jana japo usaili walifanya wote na akafanikiwa yeye tu kupata ajira hapo miongoni mwao wote kama "Security Guard", amefika kule akakuta mshahara 800+k ukiongeza na overtime ambao wao inachanganywa kwenye mshahara pamoja at the end mshahara unasoma 1.3+m na wana posho 150k kila mwisho wa mwezi,alipelekwa mtwara kituo chake cha kazi na alipewa pesa ya kujikimu zaidi ya 3m.

"B" aliajiriwa Mahakama na akapelekwa mahakama ya wilaya flani huko kama Mlinzi pia mwaka jana hiyohiyo akapewa 500k ya kujikimu na akakuta mshahara laki tatu tu yaani 300k kwa mwezi na hakuna posho yoyote.

"C" Yeye aliajiriwa nadhani mwaka huu hapo DDC (Dar Es salaam Development cooperatin) kama "Security officer" pia, amefika kakuta mshahara 696k kwa mwezi na posho za zaidi ya 300k per month na pesa za kujikimu kapewa 900k

Huyu "D" na yeye ameajiriwa mwaka huu huko Ngorongoro Conservation kama mlinzi ( Askari wa wanyamapori) huyu kafika kule kakuta mshahara 960k na overtime inategemea na masaa yako ya ziada, na posho zingine nyingi na akapewa pesa ya kujikimu 3.4m

Nimejaribu kukupa mifano hii ya watu walioajiriwa vyeo vya chini kabisa ambao ni ndugu zangu wa karibu walioajiriwa hivi majuzi pamoja na kwamba ni kada moja na elimu yao ni sawa lakini unaona hapo kabisa kuna mmoja anaweza kumlipa mwingine mshahara wake wa mwaka mzima kutumia mishahara na posho zake za miezi isiozidi mitatu.

NADHANI UMEGUNDUA KITU HAPA.

Maslahi na mishahara inatofautiana kulingana na taasisi uliyopo boss
 
Wazazi wanatakiwa sana kuangalia vijana wanaoajiriwa katika umri mdogo, ni bora hata kuwaelekeza kwa muda fulani juu ya matumizi ya pesa, saving and all na sio kukuona umeajiriwa basi ushakua mtu mzima wakati kiasi hicho kikubwa cha pesa za kila mara hujawahi kipata. Mwenyewe niliajiriwa at 22 first salary was 925k plus 1million per diem kila baada ya wiki 2 na hivi niliajiriwa mkoani yani kila ijumaa nipo airport naenda nyumbani kuona wazazi na mchumba. Looking back miaka mitano nyuma naona ningekuwa mbali sana tofauti na hapa nilipo leo maana umri unasonga na majukumu yanaongezeka
pole sana ndugu lakini bado hujachelewa sana.
umri wetu bado unaruhusu kufanya makubwa.
 
Upele humuota asikuwa na kucha. Nalipwa 716k per month, take home 454k yaan nije nilipwe 1.2M kwa mwezi na hiyo 48M mkopo wa masharti nafuu kama hayo uliopewa nadhani ningekuwa mbali sana. Nafanya mambo yalio muhimu. Napanga bajeti yangu ambayo itakuwa chini ya mstari wangu wa matumizi. Nafanya biashara ambayo inamtaji wa wateja na inaleta faida nzuri kulingana na nilichowekeza.

Pole sana. Umri wako bado. Anza upya sahihisha makosa yako. Umewapa vijana somo zuri sana.
 
boss, umri nao unachangia kwa sasa kila kitu kimebaki historia huo ujinga umebaki kuwa kumbukumbu mbaya tu kwenye maisha yangu
 
umepata pesa bado kijana mdogo sana ni halali yako kufanya hivo.
kwenye maisha kila mtu ni lazma apite hii stage, wachache sana ambao hawapitii huku na uzeeni wengi wao lazma fanya upuuzi wa kushangaza hapo ndio unakuta mtu anachukua mafao anaenda kuolea mke wa pili.

Pambana kwa vile tayari ulishashtuka karibia miaka 5 iliyopita
 
[emoji848][emoji848][emoji848]
 
Yeah,22 yrs ni mdogo mno kukamata noti za kila mwezi plus marupurupu ungezisotea usingezichezea na hata kama ungezichezea basi zingeacha alama mfano nyumba,gari mbovu mashamba,ila kule kutoka tu shule na bado unawaza kuendelea kusoma ajira hii hapa,pesa mingi usingerudi viunzi na upo kwenye right track andiko lako limesaidia weng hasa waajiriwa.

Mkuu kwa sisi(mimi) nimepitia msoto sana katika maisha yangu nimetokea familia ya kimasikini mno yaani basi tu tena ya single mother mwenye 5 kids na mimi nikiwa first born nimeparangana sana kusoma lakini hata kidato cha nne nmekimaliza kwa mateso sana,mazingira yalichangia sana kufeli nikachaguliwa vyuo vya ualimu,utumishi wa umma,afya na ugavi hakuna nilichofanikiwa kujiunga nacho maana hata mia mbovu sikuwa nayo,nikaingia mgodini mwaka na ushee hollah,

Nikaingia kutafuta mali za mjerumani sijui pasi,rupia,n.k hollah

Nikarudi shamba kulima miaka mitatu hollah
Nikabuni mbinu ya kutafuta pesa kwa kutumia taaluma yangu ya kidato cha nne tu,nikaajitolea kufundisha nursery mwaka na nusu,.............

Mpaka muda huu naandika namshukuru sana Mungu,amenithibitishia kwamba akiamua kukupa ridhiki hachagui akupe kupitia ulichokitarajia,........

Nimejenga nyumba nzuri tu ya kuishi,nina shule yangu ya English medium nursery mpaka primary.

Ukinikuta nafundisha hutakaa uamini kama nimeishia kidato cha nne, mimi siyo mkurugenzi mwenye shule mpaka leo hajulikani,kuna mkuu wa shule ndiyo meneja yeye anajua mimi ni mwangalizi tu kuna utawala pia,walimu na wafanyakazi wanalipwa na my Mrs ambaye ndiye mhasibu wa shule na yeye anafahamu kuwa mimi nina asilimia kidogo tu za umiliki kama 25% zilizobaki ni za wafadhili,kumbe ninaown hisa 100%.
Ninafundisha kama mwajiriwa na ninalipwa kama walimu wengine.
Mkuu naomba niishie hapa ila katika maisha kuna mambo mengi watu tunatembea nayo tu.
Hongera Sana lakini experience inachangia maana umepitia mengi..shida Ni ujana..wengi ujana ulituangusha
 
Jaribu kutafuta njia ya kuendesha miradi yako ukiwa ndani ya hiyo ajir.... Nawaza tu kama mkeo anauwezo mpe kazi ya kuisimamia hiyo miradi ila uhakikishe umeiweka sawa kisheria kuhusu umiliki wake. Pia Jenga tabia ya kuifanyia ukaguzi wa kimahesabu Kila baada ya muda Fulani hata kwa kuajiri mtaalamu (USIIAMINI SANA JINSIA KE na umeshasema she is smart than you)

Kwanini nimekwambia endesha miradi ukiwa kazini??

Emagine mtu Alie acha kazi 2018 akawekeza katika bishara ya kununua vitu online na kuuza na kapiga pesa sanaaa kipindi hicho kwa Sasa anahali gani??

Sio kwako tu hua nashauri Kama unauwezo wa kufungua miradi na una mtu sahihi wa kuisimamia fanya hivyo ila sio kuacha kazi completely. UTATESEKA ifanye Kazi yako kuwa chanzo kingine Cha mapato.
 
Boss Ahsante sana kwa huu ushauri wako
 
Mfano hai kuna kaka angu alikuwa anasema "aah dogo mi huyu dem hata simpendi kabisa napita nae tu kispoti" ,, mara kidogo tu kampiga mimba kwahyo ikabidi mjuba aoe kimazabe mazabe tu,,, cha kushangaza saiv wana watoto watatu ndoa ina miaka 15,, na wanapendana vizuri tu

Sent using Jamii Forums mobile app
haya mambo haya ni mungu tu mda mwingine anatenda, unajikuta unaoa pale ulipokuwa huna mapenzi napo
 
Pole sana ndugu yangu, mimi nimeajiriwa na shirika la serikali yawezekana huelewi kuhusu utofauti wa maslahi kwenye taasisi za umma, ngoja nikupe mifano hai ya ndugu zangu wa karibu kabisa wanne ambao wameajiriwa hivi karibuni baada ya kutoka kapa huko JKT kupitia pale utumishi na wote wako cheo kimoja na elimu yao ni kidato cha nne tu, wameajiriwa taasisi tofauti, tuwape majina A,B,C na D.

"A" alitangulia kuajiriwa TPA mwaka jana japo usaili walifanya wote na akafanikiwa yeye tu kupata ajira hapo miongoni mwao wote kama "Security Guard", amefika kule akakuta mshahara 800+k ukiongeza na overtime ambao wao inachanganywa kwenye mshahara pamoja at the end mshahara unasoma 1.3+m na wana posho 150k kila mwisho wa mwezi,alipelekwa mtwara kituo chake cha kazi na alipewa pesa ya kujikimu zaidi ya 3m.

"B" aliajiriwa Mahakama na akapelekwa mahakama ya wilaya flani huko kama Mlinzi pia mwaka jana hiyohiyo akapewa 500k ya kujikimu na akakuta mshahara laki tatu tu yaani 300k kwa mwezi na hakuna posho yoyote.

"C" Yeye aliajiriwa nadhani mwaka huu hapo DDC (Dar Es salaam Development cooperatin) kama "Security officer" pia, amefika kakuta mshahara 696k kwa mwezi na posho za zaidi ya 300k per month na pesa za kujikimu kapewa 900k

Huyu "D" na yeye ameajiriwa mwaka huu huko Ngorongoro Conservation kama mlinzi ( Askari wa wanyamapori) huyu kafika kule kakuta mshahara 960k na overtime inategemea na masaa yako ya ziada, na posho zingine nyingi na akapewa pesa ya kujikimu 3.4m

Nimejaribu kukupa mifano hii ya watu walioajiriwa vyeo vya chini kabisa ambao ni ndugu zangu wa karibu walioajiriwa hivi majuzi pamoja na kwamba ni kada moja na elimu yao ni sawa lakini unaona hapo kabisa kuna mmoja anaweza kumlipa mwingine mshahara wake wa mwaka mzima kutumia mishahara na posho zake za miezi isiozidi mitatu.

NADHANI UMEGUNDUA KITU HAPA.

Maslahi na mishahara inatofautiana kulingana na taasisi uliyopo boss
Kuna mda mwingine nawaona watunga sera wa hii nchi ni wapumbavu sana, mtu mwenye shahada kwenye taasisi za kawaida na serikali kuu anazidiwa mshahara mara mbili na Mlinzi, msaidizi wa ofisi au Telephone Operator mwenye elimu ya kidato cha nne tu.
Na ile kamati ya mishahara sijui hata imeishia wapi, Miongoni mwa vitu ambavyo vinanitia kero ni huu utofauti mkubwa wa mishahara serikalini

Ofisini kwetu kuna Telephone operator amehania taasisi nyingine mshahara anaolipwa sisi na degree zetu hatumfikii hata nusu unabaki kuduwaa tu, sijui waliwaza nini hawa viongozi kwenye hii miongozo ya mishahara serikalini... PUMBAVU ZAO
 
Mkuu ulifaidi ila vyema umesharekebisha uliokosea.
Mimi sina nilichokosea wala kupoteza sijawahi kula bata au kuwa na unafuu wa maisha,Ni mwajiriwa ila kutokana salary haikidhi hadi sasa sina asset yoyote wala biashara majukumu ya familia(mama pamoja na wadogo zangu) yamenibana kiasi kwamba hadi kununua nguo unaona ni dhambi,dogo yupo semester ya mwisho chuo ila hadi saivi naandika hapa sielewi ada anaipataje,kama benk nilishakopa ili niwalipie ada na 1 june anatakiwa chuo, kwa kiasi fulani nashukuru Mungu hata ili naamini atanisimamia litapita tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom