Miaka 10 ya Utumishi: Kumbukizi mbaya ya matumizi ya pesa isiyofutika katika historia ya maisha yangu

Miaka 10 ya Utumishi: Kumbukizi mbaya ya matumizi ya pesa isiyofutika katika historia ya maisha yangu

Afadhali umestuka mapema ..ni wake up call kwa tulio wengi! Mi naona vitu vya msingi ili tusipotee sana ni kama ifuatavyo:
  1. Kua karibu na Mungu kwa kumaanisha ili atupe hekima na maarifa
  2. Kua na marafiki/ kampani sahihi inayokupa wivu wa kimaendeleo..ukikaa karibu na watu wanaoongea maendeleo inafungua akili...
  1. Sikushauri uachane na starehe kama utaweza kupunguza kidogo labda ila usiachee
 
Kuna watu umewasaidia.umeshituka mapema wanzako wanashitukaga wakiwa kwenye around 56yrs hivi ndiyo wagutuka kwamba wanaelekea kustaafu
Mkuu yaani unamaanisha mtu anaweza kula bata zaidi ya miaka 30 na akaja kushtuka karibia na kustaafu?
 
Kujikwaa si kuanguka na hata ukianguka unaweza kuinuka tena. Haya ndiyo maisha,kupanda na kushuka.
 
Mkuu ikawaje
Siri siwezi simulia humu mana wata connect dot nitadakwa tuu ila jua nimeshuhudia mambo yakutisha na ya ajabu mno nikiwa na umri mdogo sana pia nilibahatika kumiliki pesa nyingi nikiwa mdogono sana nashukuru Mungu mwanamke wangu alikuwa na akili mno ila bila uyu dah cjui...
 
Oooh sawa ndugu yangu
 
daah naona watu humu ni story za mishahara wakati mimi ndo bado sina hata pakujishkiza na kuokota angalau visenti...ingawa katika maisha kuna sehemu na mimi nilifanya mistake ingawa nafsi yangu inagoma kabisa kujutia ile mistake na inaniambia nilikua sahihi...but namzigo mzito sana rohoni mwangu,nafsi yangu inauma sana...sometimes najiuliza nilimkosea nini mungu..but thank you jamiiforum kwa kuwa moja ya sehemu ambayo kichwa changu angalau kinajipumzisha
 
Duuuh pole sana mkuu
 
Hongera mkuu kwa kjitambua miaka 10 baada ya kuajiriwa.
Shukuru Mungu ulizinduka na kuona mapana ya maisha.

Sisi wengine yaliyotupata ni noma kabisa.
Baada ya kufanya kazi miaka 12 mimi nikafukuzwa kazi kama kibarua.
Kosa?
Nilikuwa napiga mzigo na kupata umaarufu kuliko bosi wangu.
Ulaji wa kijinga kijinga nilukataa katakata na kazi ilikuwa mbele ili kutimiza malengo!

Wazee wa mitoso wakakaa chini na kusema huyu kijana anaingia mjini kwa pupa, atatuulia wanetu kwa njaa.

Mipango ikasukwa na kukamilika ,shutuma zikatolewa na kuhakikiwa na wapambe. Mwisho wa siku nikatakiwa kujieleza ndani ya wiki kwa nini nisione mlango wa kutokea nje.

Nikajitetea weee lakini wapi.
Mwisho nikapewa barua ya TOKA!

Hapo ndo maisha yakaanza .
Sina nyumba nina pagala, nikahamia humo humo, nfanyeje sasa!
Lakini Mungu hamtupi mja wake.

Nilipiga mzigo wa kazi binafsi za kujiajiri kiwenda wazimu, tena lile kiwenda wazimu haswa.
Hela ikaingia tena kuliko ile hela ya ajira.

Kufumba na kufumbua miaka mitano imepita na mi naendelea na mzigo spidi ile ile.
Sasa na pochi ikakubali, tena pochi si ya kitoto.

Nikanunua gari toka Japani, ya kwanza, mwaka mwingine uliofuata ya pili kwa mamsapu, Mwaka wa nne ya tatu , tena 4WD. Nyumba ikakamilika na ikawa poa kabisa.

Aliyenitimua job tukakutana hoteli moja maarufu huko Jiji letu Kuu, wote tukila bata! Alitahayari hata kunitazama usoni alishindwa.

Sasa hivi nilipo ni viwango ambavyo nsingefikiri kuvipata katika ajira.
Mungu ana makusudi katika kila limpatalo binadamu.
Mungu kweli ni mkubwa sana juu ya yote.

(N.B. Huu mkasa ni wa kweli kabisa na nimeuandikia kitabu ambacho kimechapishwa Marekani)
Daaah kaka, Inabidi nikutafte
 
daah naona watu humu ni story za mishahara wakati mimi ndo bado sina hata pakujishkiza na kuokota angalau visenti...ingawa katika maisha kuna sehemu na mimi nilifanya mistake ingawa nafsi yangu inagoma kabisa kujutia ile mistake na inaniambia nilikua sahihi...but namzigo mzito sana rohoni mwangu,nafsi yangu inauma sana...sometimes najiuliza nilimkosea nini mungu..but thank you jamiiforum kwa kuwa moja ya sehemu ambayo kichwa changu angalau kinajipumzisha
Usikate tamaa Mr. Complex, Mungu ni mwema siku zote na ipo sehemu nzuri yenye neema aliyokuandalia.
Zamu yako itafika tu.
 
Back
Top Bottom