Hongera mkuu kwa kjitambua miaka 10 baada ya kuajiriwa.
Shukuru Mungu ulizinduka na kuona mapana ya maisha.
Sisi wengine yaliyotupata ni noma kabisa.
Baada ya kufanya kazi miaka 12 mimi nikafukuzwa kazi kama kibarua.
Kosa?
Nilikuwa napiga mzigo na kupata umaarufu kuliko bosi wangu.
Ulaji wa kijinga kijinga nilukataa katakata na kazi ilikuwa mbele ili kutimiza malengo!
Wazee wa mitoso wakakaa chini na kusema huyu kijana anaingia mjini kwa pupa, atatuulia wanetu kwa njaa.
Mipango ikasukwa na kukamilika ,shutuma zikatolewa na kuhakikiwa na wapambe. Mwisho wa siku nikatakiwa kujieleza ndani ya wiki kwa nini nisione mlango wa kutokea nje.
Nikajitetea weee lakini wapi.
Mwisho nikapewa barua ya TOKA!
Hapo ndo maisha yakaanza .
Sina nyumba nina pagala, nikahamia humo humo, nfanyeje sasa!
Lakini Mungu hamtupi mja wake.
Nilipiga mzigo wa kazi binafsi za kujiajiri kiwenda wazimu, tena lile kiwenda wazimu haswa.
Hela ikaingia tena kuliko ile hela ya ajira.
Kufumba na kufumbua miaka mitano imepita na mi naendelea na mzigo spidi ile ile.
Sasa na pochi ikakubali, tena pochi si ya kitoto.
Nikanunua gari toka Japani, ya kwanza, mwaka mwingine uliofuata ya pili kwa mamsapu, Mwaka wa nne ya tatu , tena 4WD. Nyumba ikakamilika na ikawa poa kabisa.
Aliyenitimua job tukakutana hoteli moja maarufu huko Jiji letu Kuu, wote tukila bata! Alitahayari hata kunitazama usoni alishindwa.
Sasa hivi nilipo ni viwango ambavyo nsingefikiri kuvipata katika ajira.
Mungu ana makusudi katika kila limpatalo binadamu.
Mungu kweli ni mkubwa sana juu ya yote.
(N.B. Huu mkasa ni wa kweli kabisa na nimeuandikia kitabu ambacho kimechapishwa Marekani)