Miaka 100 baada ya kifo chako, utazaliwa kwa mara nyingine ukiwa na mwili mpya

Miaka 100 baada ya kifo chako, utazaliwa kwa mara nyingine ukiwa na mwili mpya

Mkuu, kwa sisi tuliopitia mafunzo ya kibudha, tahajudi, yoga, ashart, menio, sminla na chandral tunaufahamu ukweli wa mambo. Ukitaka vingi zaidi unatakiwa kuwa na access ya Dark Web. Wengine tumekuwa tukizungumza na mizimu, majini mpaka malaika wa mashetani kwa kiebrania. Upo hapo mkuu!
Dark web inaingiaje hapa 😂😂😂
 
Melki the Storyteller mimi ni mtu mweusi (Mwa Afrika)
Je nikifa baada ya hiyo miaka 100 naweza kuzaliwa Mchina au Mwaarabu au au Mzungu? Au kama ulikuwa mwafrika hata hiyo miaka 100 unazaliwa mwafrika tena?
1. Kama roho yako itafanikiwa kufutwa kumbukumbu zote, kuzaliwa ukiwa mzungu, au mtaifa mwingine hutokea

2. Kama roho yako itabaki na baadhi ya kumbukumbu, hisia za kuwahi kuwepo ama maono, wewe utazaliwa katika mnyororo ule ule wa ukoo, ama ukoo wa kiendana na wewe, ama shurutishi la tukio hasa hasa lile lililokupelekea kupoteza uhai, ama tukio lililoihangaisha sana akili yako, ama katika mazingira uliyowahi kuishi

3. Ujio wa roho yako kabla ya kumbukumbu zako kupotezwa kwa kiasi kikubwa, itapelekea kuzaliwa katika mwili wa mnyama ama mmea ili baada ya kifo chako tena, kumbukumbu ziendelee kufutwa

Itatokea nini kama roho yako itawekwa ndani ya Mbuyu?
 
Wakati tunapata uhuru tulikuwa 2 million now tuko more than 60 million izi roho zingine zimetoka wapi?
Kwenye mimea na wanyama ambao kwa sasa i/wanapotea kutokana na kukosa umuhimu. Na ni lazima iwe hivyo ili kubalance Ecology
 
Ndo maana hua nikaaa pekee Angu hua kuna hisia zinanijia kana kwambaa sijui mm ni mwanajeshii sometimes naweza kukaa seheme nikapotea kweny mawazo kua nipo sehem nimevaa nguo za kijeshii mara sijui natoa amri…….. kuna kipind miaka ya nyuma pind nipo chuo nilkua nimepanga sehem na hapo nilipokua kulikua na mdada ni mjeshi asa kila yule dada akifua hizo uniform zake nikigusaa nasisimkaa kinomaa [emoji23] nikiwambia washikaji zangu wanambia ety nimefall in love daah [emoji23]….. ila kiukwel ule msisimko ulikua sio wa kimapenzii kabsaa kabsaa…… kuna siku nilkua natembea ghfla tu hizo hisia zikaniajia nikajikuta nakimbia kama nafanya jogging hiv zile wanazofanya wajesh asubh au jion so nikajiona nipo kambinii kabsaa nakimbiaa na washiikaji hata siwajuii nikakimbia kama dk mbili mwanangu mmoja akanistua oyaa unakimbia wap aaah aiseee nilijiona chiziiii…… kuna vitu ving tu nafanya mara nyingii sanaa

NB: nilienda hospital kupima afya ya akili lakiniii nikakuta nnautimamu kamilii hakuna shidaa

Sasa mleta mada kwaio inawezekana hii roho ishawah kua mjeshiii kipind hikoo isije ikawa kuna mtu anacheza na akili yangu
Wewe ishu ni bangi nakujua
 
Mwandishi kasema inarudi kwa mwanadamu mwingine sio mnyama tofauti. Kwahiyo hapa teyari wewe ushaleta theory ingine ya kuongea na watu , congratulations.
Nafsi yako inachukua mwili mpya, ni kama zawadi au adhabu kulingana na matendo yako ulokuwa unayaishi hapa ulimwenguni. Hivyo unaweza kuzaliwa katika mwili wa mwanadamu either ktk familia ya kitajiri, yenye mamlaka, viongozi n.k, au ukazaliwa ktk familia ya kifukara. Pia unaweza pewa adhabu zaidi nafsi yako ikachukua mwili katika viumbe wengine kama panya, mbuzi, nyoka, kenge, mjusi, nzi, mende, simba, nyegere,samaki,popo bawa, n.k. Kumbuka mzunguko huu wa nafsi hauna mwisho lakini tujitahidi kufanya tahajudi ili tujiweke karibu zaidi na ile energy ndipo tunaweza vunja minyororo ya huo mzunguko. Yaan tutakuwa Kama upepo au Nuru ambapo hatutozaliwa tena wala kufa yaan itakuwa raha sana tutaishi milele.
 
Na ndivyo ilivyo. Baada ya kifo chako tu, utapotea kwenye uwepo wa huu ulimwengu kwa muda wa miaka 100 baada ya hapo utazaliwa tena kwa mara nyingine

Kipindi cha hiyo miaka 100 ndiyo huitwa LRP ( Life Refractory Period), kipindi hiki kipo kwa lengo la kufuta kumbukumbu zote zilizopo kwenye akili ya roho husika ili kuzuia kumbukumbu kuhama kutoka mwili mmoja kwenda mwili mwingine, japokuwa kwa baadhi ya watu wengine asilimia chache za kumbukumbu uhama kutoka mwili mmoja kwenda mwingine, hapo ndipo hutokea kile tunaita de jávù, au baadhi ya watu kuexperience mambo ambayo hawajawahi kuyapitia

Kumbuka, mwili ni lazima ufe ili kukamilisha kile tunaita Ecological System. Idadi ya roho zilizopo ulimwenguni ni zile zile, hazijawahi kuongezeka ama kupungua, maana rahisi ni kuwa kamwe hautotoweka ulimwenguni mazima, ila tambua kuwa baada tu ya kufa, hauto experience fahamu yoyote, unakuwa sawa na mtu aliyelala usingizi mzito mpaka pale utakapomaliza miaka yako yote 100 ya LRP

Niwatakie maandalizi mema ya vifo na mapokezi mema ya kuzaliwa kwa mara nyingine baada ya miaka 100 baadae
Sonona haijakuacha mzima😅
 
Mim sitaki yaan nizaliwe upya nisiwakumbuke watoto wangu tena haina faida
 
Transmigration of the souls and reincarnation.

Hii kitu inaweza kuwa na ukweli japo ni mambo ya kusadikika bado.
 
Kwa hiyo baada ya miaka 100 roho hizi zinatafuta wanaume hai wanowapa mimba wanawake ili ziingie yaani zinazurura kuangalia watu wenzao wakigongana wapi mimba inashika ili ziingie, wakikosa wanaenda wapi?
 
1. Kama roho yako itafanikiwa kufutwa kumbukumbu zote, kuzaliwa ukiwa mzungu, au mtaifa mwingine hutokea

2. Kama roho yako itabaki na baadhi ya kumbukumbu, hisia za kuwahi kuwepo ama maono, wewe utazaliwa katika mnyororo ule ule wa ukoo, ama ukoo wa kiendana na wewe, ama shurutishi la tukio hasa hasa lile lililokupelekea kupoteza uhai, ama tukio lililoihangaisha sana akili yako, ama katika mazingira uliyowahi kuishi

3. Ujio wa roho yako kabla ya kumbukumbu zako kupotezwa kwa kiasi kikubwa, itapelekea kuzaliwa katika mwili wa mnyama ama mmea ili baada ya kifo chako tena, kumbukumbu ziendelee kufutwa

Itatokea nini kama roho yako itawekwa ndani ya Mbuyu?
Swali kwa nn najifeel MIMI KAMA MIMI kipindi hiki na sio kipindi kingine chochote ?
 
Back
Top Bottom