Miaka 100 baada ya kifo chako, utazaliwa kwa mara nyingine ukiwa na mwili mpya

Dark web inaingiaje hapa 😂😂😂
 
Melki the Storyteller mimi ni mtu mweusi (Mwa Afrika)
Je nikifa baada ya hiyo miaka 100 naweza kuzaliwa Mchina au Mwaarabu au au Mzungu? Au kama ulikuwa mwafrika hata hiyo miaka 100 unazaliwa mwafrika tena?
1. Kama roho yako itafanikiwa kufutwa kumbukumbu zote, kuzaliwa ukiwa mzungu, au mtaifa mwingine hutokea

2. Kama roho yako itabaki na baadhi ya kumbukumbu, hisia za kuwahi kuwepo ama maono, wewe utazaliwa katika mnyororo ule ule wa ukoo, ama ukoo wa kiendana na wewe, ama shurutishi la tukio hasa hasa lile lililokupelekea kupoteza uhai, ama tukio lililoihangaisha sana akili yako, ama katika mazingira uliyowahi kuishi

3. Ujio wa roho yako kabla ya kumbukumbu zako kupotezwa kwa kiasi kikubwa, itapelekea kuzaliwa katika mwili wa mnyama ama mmea ili baada ya kifo chako tena, kumbukumbu ziendelee kufutwa

Itatokea nini kama roho yako itawekwa ndani ya Mbuyu?
 
Wakati tunapata uhuru tulikuwa 2 million now tuko more than 60 million izi roho zingine zimetoka wapi?
Kwenye mimea na wanyama ambao kwa sasa i/wanapotea kutokana na kukosa umuhimu. Na ni lazima iwe hivyo ili kubalance Ecology
 
Wewe ishu ni bangi nakujua
 
Mwandishi kasema inarudi kwa mwanadamu mwingine sio mnyama tofauti. Kwahiyo hapa teyari wewe ushaleta theory ingine ya kuongea na watu , congratulations.
Nafsi yako inachukua mwili mpya, ni kama zawadi au adhabu kulingana na matendo yako ulokuwa unayaishi hapa ulimwenguni. Hivyo unaweza kuzaliwa katika mwili wa mwanadamu either ktk familia ya kitajiri, yenye mamlaka, viongozi n.k, au ukazaliwa ktk familia ya kifukara. Pia unaweza pewa adhabu zaidi nafsi yako ikachukua mwili katika viumbe wengine kama panya, mbuzi, nyoka, kenge, mjusi, nzi, mende, simba, nyegere,samaki,popo bawa, n.k. Kumbuka mzunguko huu wa nafsi hauna mwisho lakini tujitahidi kufanya tahajudi ili tujiweke karibu zaidi na ile energy ndipo tunaweza vunja minyororo ya huo mzunguko. Yaan tutakuwa Kama upepo au Nuru ambapo hatutozaliwa tena wala kufa yaan itakuwa raha sana tutaishi milele.
 
Sonona haijakuacha mzima😅
 
Mim sitaki yaan nizaliwe upya nisiwakumbuke watoto wangu tena haina faida
 
Transmigration of the souls and reincarnation.

Hii kitu inaweza kuwa na ukweli japo ni mambo ya kusadikika bado.
 
Kwa hiyo baada ya miaka 100 roho hizi zinatafuta wanaume hai wanowapa mimba wanawake ili ziingie yaani zinazurura kuangalia watu wenzao wakigongana wapi mimba inashika ili ziingie, wakikosa wanaenda wapi?
 
Swali kwa nn najifeel MIMI KAMA MIMI kipindi hiki na sio kipindi kingine chochote ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…