Miaka 12 ya mapenzi, visa na mikasa nikiwa na Renata
Sehemu ya kwanza
Wadau kwa kuwa ni mwisho wa mwaka na nimeanza likizo nikaona bora niweke bandiko langu hapa jukwaani kuhusu mahusiano yangu yaliyodumu kwa miaka 12 na mwanamke aliyeitwa Renata lakini hatukufikia kwenye ndoa.
Unajua kilichotokea?
Turudi nyuma kidogo miaka ya mwanzoni ya 2000, tukiwa tu tumeanza kusahau mambo ya Y2K
Nikiwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) weekend moja nilirudi nyumbani maeneo fulani hapa hapa Dar es salaam. Nikiwa natembea mtaani nakutana na mama Renata, nikamsalimu na kwa uchangamfu akaniambia karibu nyumbani mdogo wako Renata amerudi kutoka shule, yupo likizo. Wakati huo Renata alikuwa kidato cha tano.
Jioni majira ya saa 12 hivi nikaona nipite kwa mama Renata ili kumsalimu huyu mdogo wangu, nikafika na kukaribishwa vizuri. Baada ya kupewa kiti na kuketi, Renata akaitwa ili aje kunisalimia. Kiufupi nilikuwa sijamuona Renata kwa miaka miwili maana muda mwingi alikuwa shule(watoto wa boarding schools).
Alipofika kwa kweli alikuwa ameshakuwa na kupendeza, ndio ule muda wa mabinti kutoka kwenye utoto na kuingia kwenye ukubwa.
Alifika kwa furaha, nikasimama ili kumsalimia nikapokelewa kwa kumbatio huku nikipewa shikamoo yangu. Mama Renata akaingia ndani akituacha ili tuzungumze, mazungumzo hayakuwa marefu sana, mengi yakiwa ni yeye kuniuliza masuala ya chuo na mimi kumuuliza maendeleo yake ya shuleni.
Nikaaga na kuondoka.
Miezi sita baadaye Renata akarudi tena likizo wakati huu alikuwa anaelekea kuingia kidato cha sita, alitumia likizo hii kwa jaili ya masomo ya ziada, nikapata tena nafasi ya kuonana naye. Wakati huu akanipa na namba ya simu kipindi akiwa likizo.
Baada ya siku kadhaa tukawa tunatumiana meseji na kujuliana hali, baadaye tukaanza kuwa na mazungumzo muda wa usiku.
Taratibu tukaanza kuchati na kuzungumza kama wapenzi, likizo ikaisha akarudi shule.
Aliporudi shule akiwa kidato cha sita ikawa ni utaratibu wetu kuzungumza kwa siku za jumamosi na jumapili, hapa ilikuwa inatumika simu ya Matroni akimdanganya kuwa anaongea na wazazi wake. Huku sasa ikawa kawaida kuitana wapenzi na kuzungumza kama wapenzi na kupeana ahadi mbalimbali japo hatukuwa tumewahi kukutana kimwili.
Hatimaye Renata akamaliza kidato cha sita na mimi nikiwa mwaka wa pili kwenda wa tatu.
Waakati huo mimi chuoni nilikuwa na mpenzi wangu mtoto mmoja shombe kutoka Tabora, hapa mwite Sakina. Sakina nilimpata mwaka wa kwanza, tulikuwa kozi tofauti, yeye alikuwa kwenye kozi ya miaka mitatu mimi nilikuwa kozi ya miaka minne.
Nilimpata vipi Sakina, acha nikuhadithie kidogo kisha tutarudi kwa Renata.
Siku moja nikiwa Cafteria nikiwa nimechelewa kwenda kula nikakutana na Sakina, tukakaa meza moja. Tukaanza mazungumzo ya hapa na pale ndipo akanieleza huzuni kuwa alifiwa na mama yake miezi mitatu iliyopita, nikampa pole na kumnunulia Soda. Tulizungumza pale kwa muda mrefu na baadaye akawa ananiaga hapo ndipo nikaomba namba. Miezi mitatu baadaye akawa mpenzi wangu kamili, hakuwa na usumbufu Mnyamwezi yule, mpole, mtulivu na kwa kweli alikuwa vizuri kwenye mambo yetu pendwa.
Hivyo nikawa na wapenzi wawili Renata ambaye hatukuwahi kukutana kimwili na Sakina ambaye ndio ilikuwa pumziko langu nikiwa chuoni.
Turudi kwa Renata sasa baada ya kumaliza kidato cha sita.
Alipomaliza mtihani wa kidato cha sita na kurudi nyumbani, mama Renata akanitafuta tena wakati huu akaniuliza ni kitu anaweza akafanya wakati akisubiri majibu, nikamwambia hapo sasa asomee walau Introduction Course za Computer, miaka ile sehemu maarufu ilikuwa MOPAC pale Buguruni Rozana au UCC (University Computing Centre) Mlimani.
Kwa kuwa nilikuwa Mlimani binti akachagua kuja kusomea UCC ili walau tuwe tunapata muda wa kuonana.
Renata akaanza masomo UCC na kwa kweli tukawa tunapata muda wa kuonana mara kwa mara na penzi likashamiri vyema kabisa. Wakati huu akawa na simu yake mwenyewe hivyo kukawa hakuna kikwazo kwenye mawasiliano.
Baada ya muda ikabidi tu niombe tunda, Renata akaruka futi mia kuwa yeye hataki tufanye tuvute muda kidogo.
Nikakubaliana na msimamo wake na maisha yakaendelea, maana Sakina alikuwepo hivyo nikawa naona sio tatizo hata kidogo.
Miezi michache baadaye nikawa nimerudi home wakati wa likizo, jumapili moja ilikuwa na Vipaimara vingi sana mtaani kwetu, nikamwamuuliza kama tunmaweza kuonana. Akakubali na akaja nyumbani kwetu, hakukuwa na mtu nyumbani hivyo baada ya stori mbili tatu nikaomba mzigo.
Baada ya kutafakari sana Renata akakubali, alikuwa bado bikra baada ya kuhangaika sana hatimaye bikra ikatoka, hatukuendelea maana alikuwa analalamika maumivu. Rasmi tukavungua ukurasa mpya wa mapenzi.
Baada ya hapo tuliendelea kufanya kadri tulivyokuwa tunapata nafasi, ikawa ni mchezo wetu rasmi.
Sakina anagundua kuwa nina mpenzi mwingine!
Nikiwa mwaka wa tatu, kuna siku nikiwa na Sakina baada ya kumsindikiza mjini kununua nguo, tukiwa kwenye daladala za Kariakoo-Mwenge akawa ameomba simu ampigie mtu. Alipomaliza kupiga akaingia kwenye meseji, sikuwa na wasiwasi kwa sababu huwa nafuta meseji zote za Renata.
Pasipo kujua kumbe Renata alituma meseji ambayo sikuwa nimeifungua, Sakina alisoma na kisha kunipa simu huku akinionyesha meseji. Miaka mingi imepita lakini bado nakumbuka ile meseji “my darling, usije ukanisaliti hulo chuoni”. Tulibaki kimya mpaka tuliposhuka Mwenge kituoni. Sakina alishuka na kuomba mfuko uliokuwa na mizigo yake na kuniambia kwa upole, tafadhali kuanzia sasa tusijuane..
Wiki ikapita Sakina hajibu meseji wala kupokea simu yangu, tukikutana mahali hataki hata kuitikia salamu yangu, nikaona hapa mapenzi yamefikia tamati. Kwa kweli iliniuma sana, nilikuwa nimemzoea sana Sakina na alikuwa mwanamke mwema sana kwangu.
Nikaona sasa niwekeze kwa Renata maana Sakina ameshanipa mkono wa kwa heri.
Hatimaye matokeo yakatoka na Renata alikuwa amepata Division 1 baadaye akajiunga chuo hapa Dar.
Kwa sababu ya uhaba wa Hostel, Renata aliamua kupanga chumba mitaa fulani hapa wilaya ya Ilala, nilisaidia kufanikisha mpango huo kwa sababu niliona kabisa akiwa na chumba chake itakuwa fursa kwangu kwenda na kufaidi mema ya nchi.
Baada ya kuwa na chumba chake kwa kweli hapo sasa ikawa kama nyumbani kwangu maana nilikuwa nakaa chuoni mpaka ijumaa jioni namalizia weekend kwa Renata narudi chuoni Jumatatu asubuhi.
Hayo yakawa maisha yangu na Renata.
Hatimaye Sakina akamaliza chuo maana alikuwa na kozi ya miaka mitatu. Siku alipomaliza mtihani wa mwisho akiwa anajiandaa kuondoka hosteli akanipigia simu kuwa yupo Cafteria, nikaenda na kuzungumza naye na kuagana naye, nakumbuka maneno yake “I leave you in peace”.
Ukurasa wangu na Sakina ukafungwa rasmi. Mara ya mwisho nilikutana naye mwaka 2020 alikuwa ni afisa mkubwa kwenye taasisi moja ya elimu hapa DSM. Ameolewa na familia yake.
Mapenzi na Renata yakaendelea kwa kasi, wakati huu sasa hata baadhi ya wanafamilia wakaanza kuhisi kuwa sisi tuna mahusiano.
Hatimaye nawekwa kitimoto na mama Renata……
Siku moja nikiwa ndio namalizia Dissertation nikijiandaa kwa presentation ya mwisho nikapigiwa simu na mama Renata.
Baada ya kupokea akaniuliza swali ambalo hakuwahi kuniuliza “upo wapi?” nikasita kisha nikajibu kuwa nipo chuoni….akaniambia ukipata nafasi njoo nyumnbani jumamosi.
Nikaona hapa tayari kuna tatizo, nikampigia mrembo wangu Renata na kumuuliza kuna tatizo mbona mama yake amenipigia na kutaka kuonana na mimi? Renata akanijibu kuwa yeye hajui lakini pia ameambiwa awepo kwao jumamosi. Kufikia hapo nikajua hapa tayari kuna jambo.
Hiyo weekend sikwenda kulala kwa Renata maana machale yalinicheza hivyo nikabaki Hosteli.
Jumamosi ilipofika nikampitia Renata ili kuelekea nyumbani, tuliposhuka kila mtu akapita njia yake.
Nafika nyumbani kwetu mama yangu baada ya salamu ananiuliza una mahusiano na Renata? Nikabaki natoa macho na kujibu kuwa hapana. Mama akasema nyie watoto mna mambo ya ajabu kabisa mmekuwa hapa kama ndugu leo mmekuwa wapenzi? Hakuonyesha kushangazwa ila naona hakutarajia mahusiano kati yangu na Renata.
Jioni nikampigia mama Renata kuwa na kumwambia nipo nyumbani anataka tuonane saa ngapi, mama akajibu njoo sasa hivi.
Nikajipa nguvu na kwenda kwa akina Renata, nikamkuta Renata na mama yake wakiwa wamekaa na kiti kimoja kikiwa wazi. Nikawasalimu wote na kumuuliza Renata habari za siku nyingi, akaniangalia na kucheka huku mama yake akiguna.
Nilipokaa mama Renata akaniambia nilikuwa na maswali mengi lakini mwenzako ameshayajibu tayari. Nilitaka kujua una mahusiano na mwanangu? Renata ameshajibu kuwa ni kweli mna mahusiano, maana mimi nilikuwa nasikia tu. Nikatikisa kichwa bila kujua niseme nini.
Mama akaendelea kwa umri mlio nao siwezi kuwaambia msiendelee kwa sababu najua mtaendelea ila sasa nawaomba sana, mzingatie masuala ya afya na kuepeuka mimba....
Tutaendelea.........