Miaka 13 Bila Albert Mangweah: Bongo Flavour Artists wamejipangaje kumuenzi 2026

Miaka 13 Bila Albert Mangweah: Bongo Flavour Artists wamejipangaje kumuenzi 2026

D

DeletedMember281674

Guest
28 Mei 2013 Msanii Maarufu enzi hizo wa Bongo Flavour alitutoka Duniani akiwa kwenye Matibabu huko nchini Afrika Kusini.

Wasanii wa Bongo Flavour wamejipangaje kumuenzi? Naona kimya sisikii watu wakimzungumzia namna ya kumuenzi mwaka huu wa 2026.

Kwangu Binafsi nitamkumbuka kwa nyimbo ya ni Ghetto langu Tu...huu wimbo aliutoa wakati ndiyo naanza Maisha nikiwa ndani ya chumba kimoja mitaa ya Sinza.
 
Mpaka sasa kwenye free style hakuna wa kumkuta Ngwear... alikua akiitwa hata usingizini anaingiza verse. Ilikua wewe mpe tittle ya nyimbo mengine muachie. Atakuua
Kweli kabisa, hili alishawahi kusema Fid Q kwenye Media Moja Kwamba walipokuwa wanarekodi wimbo wa CNN, ilibidi Mashauri ya awali ayafute, atunge upya...huku Producer Majani akiweka unyama mwingi sana kwenye Beat.

Ngwair aliitendea vyema Sana Beat ya Majani kwenye wimbo wa CNN
 
Ngwea hakua na mistari mikali kama jay mo. Sema jamaa alikua na flow kali yaani hata ukimpa biti la singeri anashuka nalo
 
Naona Media zote Bongo wapo kimya sana
Mkuu kwa hili wala usizipe media za bongo lawama, coz wamekufa celebrities wengi hapa bongo ila naona ngwea amekua na bahati ya kipekee sana kupewa heshima hiyo.

Nafkiri ungeanzishwa utamaduni na wasanii wa bongo fleva kuwa enzi wenzao ingeleta maana zaidi
 
Kweli kabisa. Naona hata Mawingu FM wapo kimya hata MC Chonde haijatoa file lake kwenye Seva. Yaani ni changamoto sana
 
Jambo ulifikirie wewe utekelezaji wafanye wengine?

Wewe umefanya nini kumuenzi tofauti na kufungua uzi?

Albert yeye alikua anawaenzi vipi Malegend wa muziki waliofariki zamani?
 
Back
Top Bottom