Miaka 20 Baada ya Kufika Pwani ya Kipumbwi: Historia ya Kipumbwi Katika Mapinduzi ya Zanzibar

Miaka 20 Baada ya Kufika Pwani ya Kipumbwi: Historia ya Kipumbwi Katika Mapinduzi ya Zanzibar

Mkuu Asilimia 2.ni negligible in science where the sample size is large than the Required value...
Kwa mfano wanaposema hakuna Dawa mahospitali wanamaanisha Dawa zilizopo hazikidhi Matakwa wa kiasi kinachotakuwa kuwepo...

Mfano mwingine...unaohudu Siasa..

Unapoambiwa kuwa Tanganyika haikuwa Huru kabla ya 1961,Haimaanishi kwamba waliishi kama hera ila walikuwa na uhuru ila haukutosha kusema walikuwa huru moja kwa moja...
Sawa nimekuelewa msingi wa hoja.
 
Ni kwamba Watanganyika ndo walishiriki mapinduzi ya Zanzibar kumuondoa mwarabu bila wazanzibar kupenda? Au sijaelewa
Chief mapinduzi hasa nyakati hizo za 1960 yalikuwa na mikono ya Mmarekani au Msoviet.

Zanzibar kwa sababu nyingi, ilikuwa inawindwa na Wakomunisti mf kina M.Babu na wamarekani. Kwa hesabu za CIA, sehemu pekee ya mapinduzi ni kutokea Tanganyika. So, ni makundi mengi yalikuwa yanaimendea zenji, Ila lilofanikiwa ni la Nyerere[CIA influenced]
 
Chief mapinduzi hasa nyakati hizo za 1960 yalikuwa na mikono ya Mmarekani au Msoviet.

Zanzibar kwa sababu nyingi, ilikuwa inawindwa na Wakomunisti mf kina M.Babu na wamarekani. Kwa hesabu za CIA, sehemu pekee ya mapinduzi ni kutokea Tanganyika. So, ni makundi mengi yalikuwa yanaimendea zenji, Ila lilofanikiwa ni la Nyerere[CIA influenced]
Hili la siasa za vita baridi kuchangia hilo limetajwa sana na wanazuoni/wasomi.

Kuna hadi nyaraka za CIA ambazo tayari ni 'declassified' zinaongelea hizo, hata humu JF kuna vipande viliwahi kuwekwa na wadau.

Hayo ya mapinduzi kuanzia kambi za Sakura huku Tanganyika na kuhamia kipumbwi Zanzibar nimezisoma kwenye maandiko ya Mohamed Said.
 
Sio rahisi kwa wamatumbi kutoka Pwani ya nchi A kwenda kuangusha serikali ya nchi B jirani kwa Siri, bila mkono wa serikali A.
objectivity ya mtu kama Mayala hunishangaza sometimes. Yaani watu watoke tu from nowhere waingie nchi nyingine? Bila kuwa mobilized? Bila kuwa organized? Bila kuwa na planning? Bila kuwa na Prior knowledge? Na serikali yao iwaache tu? Hiyo serikali haihofii mgogoro na nchi jirani? Ticha alihusika na Mapinduzi zanzibar.
 
Kipumbwi hapo watoto wa shule zaidi ya asilimia 80 wanavalishwa hirizi. Tulikuja kuhubiri hapo injili tukashangaa shuleni watoto wanalipuka mapepo ukitaja jina la Yesu Kristo.
Kwa jamii zetu nyingi hilo la hirizi kuvishwa watoto hata watu wazima sio la kushangaza.

Wengi huvaa ili kujilinda dhidi ya kudhuriwa na wachawi wenye nia mbaya.

Ushirikina umedumaza jamii hizi.
 
Je?! WaZanzibar nini maoni yao kuhusu utawala wa Sultan na baad ya Sultan mpaka sasa?
 
No sio serikali, ni Wamatumbi wa Bara kwenda kuwasaidia Wamatumbi wa Zanzibar!, serikali yetu had no hands!.
P
Wana bodi, japo tuko kwenye harakati za kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge, kuna swali linanitatiza kuhusu Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, ambapo majibu yake sahihi, pia yanaweza kuwa ni kiashiria tosha cha mshindi wa urais wa Zanzibar, iwapo uchaguzi utakuwa huru na wa haki.

Swali hili lahusu ukweli haswa kuhusu Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 12, 1964, baada ya kuibuka kwa kitabu kingine kiitwacho "Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru"
View attachment 2077603
kilichoandikwa na Mwanazouni wa Zanzibar, Dr. Harith Ghassany, kama kilivyofanyiwa mapitio na mwandishi Mohamed Said kwenye gazeti la Al-Nuur la leo.

Ghasanny anasema kumbe Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yalitekelezwa na askari mamluki wa Kimakonde (Wakata Mkonge) ambao waliongozwa na Mzee Mohamed Omar Mkwawa (Tindo) chini ya Amiri Jeshi wa jeshi la mamluki hao Victor Mkello (RIP). (kumbe amiri jeshi hakuwa Mganda John Okello pekee, bali pia Mkello yumo?!.

Mamluki hao walitumia zana zao za kukatia mkonge, zile sime za makali kuwili, walizisunda kwenye nguo zao za ndani na kusafirishwa kwa mitumbiwi usiku usiku kupitia Kipumbwi. Jee wale mashuhuda wa Mapinduzi yale Matukufu ya Zanzibar, wanayakubali haya?.

Pia mwandishi anamalizia kwa kusema hata mauaji ya Karume, hayakutekelezwa na wapinga Mapinduzi, bali ni miongoni mwa hao hao wanamapinduzi, baada ya kupishana kauli fulani fulani za uendeshaji wa Zanzibar baada ya Mapinduzi.

Nimesoma kitabu cha John Okello kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar,
View attachment 2077618
yeye anasema yake, vitabu kadhaa vya waandishi wazungu wanasema yao, historia tukuka ya Mapinduzi Matukufuya ya Zanzibar nayo nayo inasema kivyake, hivi hakuna any straight line yoyote kuhusu Mapinduzi hayo, ya Zanzibar?.
Jee yalipangwa na nani? Yalitekelezwaje?.
Nini haswa kilichotokea usiku ule wa Januari 11?.
Nani alifanya nini wapi?
Na mwisho tuzungumzie wafaidika wa Mapinduzi hayo Matukufu ya Zanzibar na bila kuwasahau wahanga wa Mapinduzi hayo ambao kwako yatakuwa sio Matukufu, ni kina nani haswa?, na kama kuleta amani na utangamano wa Zanzibar kuhusu Mapinduzi hayo kutahitajika kuundwa kwa Tume ya Ukweli na Upatanisho, "Truth and Reconciliation Commission" ili waliohasimiana kutokana na Mapinduzi hayo, wapatanishwe kwa maslahi mapana ya Zanzibar?.

Majibu ya maswali haya yatasaidia kujua mustakabali wa matokea ya uchaguzi wa Zanzibar kudhirihisha kuwa Wazanzibari ni wamoja, hakuna kundi la walishiriki Mapinduzi ndio wenye uhalali zaidi kuitawala Zanzibar kuliko wasioshiriki, after all kumbe Mapinduzi yenyewe, yametekelezwa na askari mamluki wa Kimakonde, toka mashamba ya mkonge Tanga!.

Pasco
Rejea za Mwandishi huyu kuhusu Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
  1. Miaka 50 Ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Bado Kuna Maswali Bila Majibu -1
  2. Neno "Matukufu" Katika Mapinduzi ya Zanzibar, Lilitoka Wapi, na Yana Utukufu Gani?!,
  3. Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar: Kumbe Waarabu Hawakufukuzwa! Walikimbia Wenyewe - Mzee Sukari
Tarehe kama ya leo 11/01/1964 miaka 60 iliyopita, ndio Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yalifanyika!. Alfajiri ya Tarehe 12 Januari, 1964 ilikuwa ni kutangazwa tuu!.

Nawatakia maadhimisho mema ya miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Paskali
 
Asante sana kwa kumbukumbu ya Maskani Kipumbwi.

Mimi ni muumini wa karma, what goes around, comes around.

Wakaazi halisi wa Zanzibar kabla ya ujio wa Waarabu ni Wakwezi na Wahadimu ambao wote ni Wamatumbi. Wareno wakaivamia Zanzibar, Kiongozi wa Wamatumbi, Mwinyimkuu akaomba usaidizi wa Waarabu kuwapiga Wareno, wakakubali na baada ya kuwashinda Wareno, haijulikani hawa Waarabu walimfanya nini Mwinyimkuu, maana hakuna kukumbukumbu yoyote hata ya uongo uongo kuonyesha ilikuwa Sultan Seyyid Said akahamishia The Sultanate yako toka Oman kuja Zanzibar ile 1732. Kwa Tanganyika Karl Peters alisainisha mikataba kwa kina Chifu Mangungo, kwa Kilwa Hassan Bin Amiri, alikinunua kisiwa cha Kilwa kwa kitambaa kinachozunguka Kilwa yote, lakini kwa Zanzibar, Mwarabu aliipataje Zanzibar!, no one knows Udhalimu wa Waarabu Zanzibar na Pemba: Ndugu zetu waliteswa, hasiwa, bakwa, na kuuawa kinyama

Hivyo Sultan Seyyid Said wa Oman, alivivamia visiwa vya Zanzibar, akajimilikisha na kuvifanya mali yake, bila kubisha hodi!.

Hivyo hakuna ubaya wowote kwa Wamatumbi wa Zanzibar, kuomba msaada kwa Wamatumbi wenzao wa Tanganyika kuwasaidia kuvikomboa visiwa vyao dhidi ya uvamizi wa Sultan of Oman ambaye baada ya kuitwaa Zanzibar, akawa Sultan of Zanzibar.

Hivyo ile usiku wa January 11 kuamkia January 12, Wamatumbi wakafanikiwa kuvikomboa visiwa vyao, na Mwarabu, kama alivyokuja pasi hodi, aliondoka pasi kuaga! Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar: Kumbe Waarabu Hawakufukuzwa! Walikimbia Wenyewe - Mzee Sukari

Kama ikithibitika Kipumbwi ilitumika kuikomboa Zanzibar, inastahili kupewa hadhi na heshima yake katiba ukombozi wa Zanzibar.
P
Mwana JF, Paskali, anakutakia wewe na familia yako HERI YA SIKUKUU YA MAPINDUZI MATUKUFU
YA ZANZIBAR!
Paskali
 
MIAKA 20 BAADA YA KUFIKA PWANI YA KIPUMBWI: HISTORIA YA KAMBI YA KIPUMBWI KATIKA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

Miaka 20 iliyopita tarehe kama ya leo 9 December, 2003 ndiyo siku Mohamed Omari Mkwawa alipotufikisha mimi na Dr. Harith Ghassany Kipumbwi.

Siku hii iliangukia kuwa siku Tanganyika ilipopata uhuru wake.
Kipumbwi ni kijiji kidogo cha wavuvi kilomita chache kutoka Tanga.

Hapa Kipumbwi ndipo ilipowekwa kambi ya askari mamluki wengi wao Wamakonde waliokuwa wanapewa mafunzo ili washiriki katika mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.

Historia hii si ngeni kwa sasa kwani Dr. Ghassany kaieleza kwa kirefu katika kitabu chake, "Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru," (2010).

Lakini kabla ya yeye kufika Kipumbwi na kushuhudia kwa macho yake yale aliyoelezwa na Mzee Mkwawa Tanga mjini kuwa alihusika katika kuwavusha Wamakonde kwa siri kuingia Zanzibar kushiriki katika mapinduzi hii ilikuwa siri kubwa sana.

Sikupata siku kumuona Dr. Ghassany kafurahi kama siku ile.

Kwa hakika kabisa alikuwa na haki ya kufurahi kwani alikuwa amekitegua kitendawili kikubwa; kwanza kuwa kuwa kulikuwa na kambi ya mamluki katika ardhi ya Tanganyika waliovushwa na kuingia Zanzibar kusaidia mapinduzi.

Kafika Kipumbwi na Mzee Mkwawa akatupitisha sehemu zote kuanzia pango la chini walikukuwa wanaficha majahazi yao hadi kutuonyesha mgahawa mdogo walipokuwa wakila usiku kabla ya kuingia katika vyombo na kuanza safari.

Pili Kipumbwi ilisaidia kueleza mauaji yaliyotokea mashamba ambako Waarabu wengi waliuliwa.

Leo naikumbuka siku hii miaka 20 iliyopita na naweka picha tulizopiga Kipumbwi.

PICHA: Picha ya mwisho ni Mzee Mohamed Omari Mkwawa na mkewe.

View attachment 2838139
Kipumbwi na Sakura nimevisoma kwenye kitabu cha kwaheri ukoloni kwaheri uhuru.....hiki kitabu kina mengi mazuri ya kujifunza.
 
Huo ndo ukweli mchungu mkuu...
Wazanzibar walikuwa wameridhia na Utawala wao kwani waliishi kwa Raha..
Story kama hizi ukitaka kuzipata nenda zanzibar na Tanga...
Hawa Asp na Umma party walioshiriki mapinduzi si wazanzibari?....mbona mnasema wazanzibari wote waliridhia serikali ya Shamte?
 
Hawa Asp na Umma party walioshiriki mapinduzi si wazanzibari?....mbona mnasema wazanzibari wote waliridhia serikali ya Shamte?
Mapinduzi hayakufanywa na ASP wala Umma Party..
Mapinduzi yana Historia Ngumu sana Kuiweka kwenye Mitandao..
Hakuna Kiongozi wa Hivyo Vyama Ulivyotaja Alishiriki Mapinduzi..
WAlioshiriki Wengi walitesa Babu zetu..

Akiwemo Babu yangu aliuawa Vikali sana..
Mapinduzi yalifanywa na John Okelo et al na sio Wazanzibar..
Pitia Hapa..


View: https://youtu.be/Ss-lfLLzV-k?si=iK-ydwX4uzyaroe1


View: https://youtu.be/6rX5MHdXW7E?si=T0-LYPsJxvecdPu5

Mwisho kwa Masikitiko Makubwa Malizia Na hii..


View: https://youtu.be/NoRgEqtwAks?si=uT1EaXWufbjW26Mg
 
Kipumbwi na Sakura nimevisoma kwenye kitabu cha kwaheri ukoloni kwaheri uhuru.....hiki kitabu kina mengi mazuri ya kujifunza.
Kipumbwi na Sakura Ndo tulipofikia Baada kutoka Zanzibar Tulivyopanda Vidau kuja Bara..
Baadaye kuhamia Tanga Mjini mwaka 1980s
 
Mapinduzi hayakufanywa na ASP wala Umma Party..
Mapinduzi yana Historia Ngumu sana Kuiweka kwenye Mitandao..
Hakuna Kiongozi wa Hivyo Vyama Ulivyotaja Alishiriki Mapinduzi..
WAlioshiriki Wengi walitesa Babu zetu..

Akiwemo Babu yangu aliuawa Vikali sana..
Mapinduzi yalifanywa na John Okelo et al na sio Wazanzibar..
Pitia Hapa..


View: https://youtu.be/Ss-lfLLzV-k?si=iK-ydwX4uzyaroe1


View: https://youtu.be/6rX5MHdXW7E?si=T0-LYPsJxvecdPu5

Mwisho kwa Masikitiko Makubwa Malizia Na hii..


View: https://youtu.be/NoRgEqtwAks?si=uT1EaXWufbjW26Mg

Oooooh!...pole mkuu...wewe pia ni Mzanzibari?

Kwa maelezo yako ni kuwa mapinduzi yalipangwa na kufanywa na walio nje ya Zanzibar (Tanganyika), ila mkuu lazima tukubaliane kwamba hao waliofanya mapinduzi (Tanganyika) wasingeweza bila kupata ridhaa/ruhusa/ushirikiano kutoka baadhi ya wazanzibari (ASP).....
 
Oooooh!...pole mkuu...wewe pia ni Mzanzibari?

Kwa maelezo yako ni kuwa mapinduzi yalipangwa na kufanywa na walio nje ya Zanzibar (Tanganyika), ila mkuu lazima tukubaliane kwamba hao waliofanya mapinduzi (Tanganyika) wasingeweza bila kupata ridhaa/ruhusa/ushirikiano kutoka baadhi ya wazanzibari (ASP).....
Yes, Kiasili Mimi Ni mzanzibar ila Kwa sasa Ni miaka 38 Tangu Tutoke Zanzibar na kuamia Bara mwaka 1987 Baada ya Rais wetu wa Zanzibar Kuhamia Bara Kuwa Rais wa Muungano..(Rais Mwinyi)

Wengi walihama Kuja Tanga Ikiwemo Familia Yetu..
Japo Haifuti asili yangu Ya Uzanzibari..

Pili Umeangalia Hiyo Video ya Massacre (Revolution Massacre) niliyokutumia Hapo Juu?
Inaonyesha Kuwa Kulikuwa na Mashambulizi makali..Je Sehemu yenye Mashambulizi Huwa Kuna ruhusa Au ridhaaa
 
Back
Top Bottom