Miaka 20 Baada ya Kufika Pwani ya Kipumbwi: Historia ya Kipumbwi Katika Mapinduzi ya Zanzibar

Miaka 20 Baada ya Kufika Pwani ya Kipumbwi: Historia ya Kipumbwi Katika Mapinduzi ya Zanzibar

Yes, Kiasili Mimi Ni mzanzibar ila Kwa sasa Ni miaka 38 Tangu Tutoke Zanzibar na kuamia Bara mwaka 1987 Baada ya Rais wetu wa Zanzibar Kuhamia Bara Kuwa Rais wa Muungano..(Rais Mwinyi)

Wengi walihama Kuja Tanga Ikiwemo Familia Yetu..
Japo Haifuti asili yangu Ya Uzanzibari..

Pili Umeangalia Hiyo Video ya Massacre (Revolution Massacre) niliyokutumia Hapo Juu?
Inaonyesha Kuwa Kulikuwa na Mashambulizi makali..Je Sehemu yenye Mashambulizi Huwa Kuna ruhusa Au ridhaaa
Sio rahisi kwa nchi A mapinduzi ndani ya nchi B bila kupata uungwaji mkono wa baadhi ya watu ndani ya nchi B.
 
Hawa Asp na Umma party walioshiriki mapinduzi si wazanzibari?....mbona mnasema wazanzibari wote waliridhia serikali ya Shamte?

mkuu unaielewa dhana ya mapinduzi? siku zote dhana ya mapinduzi huwa haina mahusiano na wananchi wa kawaida. hata kama kuna baadhi ya wazanzibari ambao walishiriki kwenye zile harakati za mapinduzi hai translate kuwa ndio wananchi kiujumla.
 
MIAKA 20 BAADA YA KUFIKA PWANI YA KIPUMBWI: HISTORIA YA KAMBI YA KIPUMBWI KATIKA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

Miaka 20 iliyopita tarehe kama ya leo 9 December, 2003 ndiyo siku Mohamed Omari Mkwawa alipotufikisha mimi na Dr. Harith Ghassany Kipumbwi.

Siku hii iliangukia kuwa siku Tanganyika ilipopata uhuru wake.
Kipumbwi ni kijiji kidogo cha wavuvi kilomita chache kutoka Tanga.

Hapa Kipumbwi ndipo ilipowekwa kambi ya askari mamluki wengi wao Wamakonde waliokuwa wanapewa mafunzo ili washiriki katika mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.

Historia hii si ngeni kwa sasa kwani Dr. Ghassany kaieleza kwa kirefu katika kitabu chake, "Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru," (2010).

Lakini kabla ya yeye kufika Kipumbwi na kushuhudia kwa macho yake yale aliyoelezwa na Mzee Mkwawa Tanga mjini kuwa alihusika katika kuwavusha Wamakonde kwa siri kuingia Zanzibar kushiriki katika mapinduzi hii ilikuwa siri kubwa sana.

Sikupata siku kumuona Dr. Ghassany kafurahi kama siku ile.

Kwa hakika kabisa alikuwa na haki ya kufurahi kwani alikuwa amekitegua kitendawili kikubwa; kwanza kuwa kuwa kulikuwa na kambi ya mamluki katika ardhi ya Tanganyika waliovushwa na kuingia Zanzibar kusaidia mapinduzi.

Kafika Kipumbwi na Mzee Mkwawa akatupitisha sehemu zote kuanzia pango la chini walikukuwa wanaficha majahazi yao hadi kutuonyesha mgahawa mdogo walipokuwa wakila usiku kabla ya kuingia katika vyombo na kuanza safari.

Pili Kipumbwi ilisaidia kueleza mauaji yaliyotokea mashamba ambako Waarabu wengi waliuliwa.

Leo naikumbuka siku hii miaka 20 iliyopita na naweka picha tulizopiga Kipumbwi.

PICHA: Picha ya mwisho ni Mzee Mohamed Omari Mkwawa na mkewe.

View attachment 2838139
Hii ntaisoma baadae
 
Nyerere na Kambona walimtumia Kassim Hanga kufanikisha mapinduzi yale huku wakimuaminisha kuwa baada ya mapinduzi yeye ndie watakaempa uongozi, ila walimgeuka na kuchomeka watu kama akina Okello na wengine na akaishia kuwa powerless, na Karume akatangazwa kuwa raisi.
 
Hanga alishiriki moja kwa moja mapinduzi ndio maana alikuwa makamu wa Rais wa Baraza la mapinduzi..
 
Sio rahisi kwa nchi A mapinduzi ndani ya nchi B bila kupata uungwaji mkono wa baadhi ya watu ndani ya nchi B.
Na Ndiyo maana Kulilazimishwa Muungano wa Haraka sana..
Na Muungano huo Ukitaka Kuvunjika Utaleta Athari ikiwemo maswali kama Hayo uliyouliza Na Pengine Zanzibar wanaweza Kuishtaki Tz (Haya Ni maoni yangu Nisifungwe kwa Hayo)
 
Huo muungano uliwekwa haraka Ili kuilinda serikali mpya ya Zanzibar dhidi ya mapinduzi mengine kumbuka baada ya mapinduzi kulipelekwa Polisi 300 wa Tanganyika kulinda amani kule Zanzibar na kupuliza fujo.
 
Sasa Hilo ndo ulipaswa Ujiulize kwa Makini Sana 🤣🤣🤣
KWanini Walipelekwa polisi Na Jeshi haraka?
Kwani Zanzibar Lilikuwa Ni Koloni letu au Mkoa wetu??
Kwanini Hilo jeshi lisingepelekwa Kutoka Uganda au Kenya au Lisingepelekwa KutoKA UNO au OAU (kipindi hicho)..
Toka nje ys Box Halafu jiulize, Kwanini Jeshi Kilikuwa Kinafichwa Nini Kupeleka Jeshi na Kabla Hujaondoa Jeshi Ukataka Muungano wa Haraka?
Ambao mpaka Leo Mkataba Wake haujulikani?
 
kumbe ni nyerere ndio alimkamata okolle na kumfukuza

1736697628130.png
 
Hanga alishiriki moja kwa moja mapinduzi ndio maana alikuwa makamu wa Rais wa Baraza la mapinduzi..

kule kuwa makamo wa rais ndio kutulizwa kwenyewe mkuu, alidhibitiwa kwa njia hiyo. yeye ndie aletakiwa awe Raisi.
 
Back
Top Bottom