Sio rahisi kwa nchi A mapinduzi ndani ya nchi B bila kupata uungwaji mkono wa baadhi ya watu ndani ya nchi B.Yes, Kiasili Mimi Ni mzanzibar ila Kwa sasa Ni miaka 38 Tangu Tutoke Zanzibar na kuamia Bara mwaka 1987 Baada ya Rais wetu wa Zanzibar Kuhamia Bara Kuwa Rais wa Muungano..(Rais Mwinyi)
Wengi walihama Kuja Tanga Ikiwemo Familia Yetu..
Japo Haifuti asili yangu Ya Uzanzibari..
Pili Umeangalia Hiyo Video ya Massacre (Revolution Massacre) niliyokutumia Hapo Juu?
Inaonyesha Kuwa Kulikuwa na Mashambulizi makali..Je Sehemu yenye Mashambulizi Huwa Kuna ruhusa Au ridhaaa
Hawa Asp na Umma party walioshiriki mapinduzi si wazanzibari?....mbona mnasema wazanzibari wote waliridhia serikali ya Shamte?
Hii ntaisoma baadaeMIAKA 20 BAADA YA KUFIKA PWANI YA KIPUMBWI: HISTORIA YA KAMBI YA KIPUMBWI KATIKA MAPINDUZI YA ZANZIBAR
Miaka 20 iliyopita tarehe kama ya leo 9 December, 2003 ndiyo siku Mohamed Omari Mkwawa alipotufikisha mimi na Dr. Harith Ghassany Kipumbwi.
Siku hii iliangukia kuwa siku Tanganyika ilipopata uhuru wake.
Kipumbwi ni kijiji kidogo cha wavuvi kilomita chache kutoka Tanga.
Hapa Kipumbwi ndipo ilipowekwa kambi ya askari mamluki wengi wao Wamakonde waliokuwa wanapewa mafunzo ili washiriki katika mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.
Historia hii si ngeni kwa sasa kwani Dr. Ghassany kaieleza kwa kirefu katika kitabu chake, "Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru," (2010).
Lakini kabla ya yeye kufika Kipumbwi na kushuhudia kwa macho yake yale aliyoelezwa na Mzee Mkwawa Tanga mjini kuwa alihusika katika kuwavusha Wamakonde kwa siri kuingia Zanzibar kushiriki katika mapinduzi hii ilikuwa siri kubwa sana.
Sikupata siku kumuona Dr. Ghassany kafurahi kama siku ile.
Kwa hakika kabisa alikuwa na haki ya kufurahi kwani alikuwa amekitegua kitendawili kikubwa; kwanza kuwa kuwa kulikuwa na kambi ya mamluki katika ardhi ya Tanganyika waliovushwa na kuingia Zanzibar kusaidia mapinduzi.
Kafika Kipumbwi na Mzee Mkwawa akatupitisha sehemu zote kuanzia pango la chini walikukuwa wanaficha majahazi yao hadi kutuonyesha mgahawa mdogo walipokuwa wakila usiku kabla ya kuingia katika vyombo na kuanza safari.
Pili Kipumbwi ilisaidia kueleza mauaji yaliyotokea mashamba ambako Waarabu wengi waliuliwa.
Leo naikumbuka siku hii miaka 20 iliyopita na naweka picha tulizopiga Kipumbwi.
PICHA: Picha ya mwisho ni Mzee Mohamed Omari Mkwawa na mkewe.
View attachment 2838139
Hanga alishiriki moja kwa moja mapinduzi ndio maana alikuwa makamu wa Rais wa Baraza la mapinduzi..Nyerere na Kambona walimtumia Kassim Hanga kufanikisha mapinduzi yale huku wakimuaminisha kuwa baada ya mapinduzi yeye ndie watakaempa uongozi, ila walimgeuka na kuchomeka watu kama akina Okello na wengine na akaishia kuwa powerless, na Karume akatangazwa kuwa raisi.
Na Ndiyo maana Kulilazimishwa Muungano wa Haraka sana..Sio rahisi kwa nchi A mapinduzi ndani ya nchi B bila kupata uungwaji mkono wa baadhi ya watu ndani ya nchi B.
Huo muungano uliwekwa haraka Ili kuilinda serikali mpya ya Zanzibar dhidi ya mapinduzi mengine kumbuka baada ya mapinduzi kulipelekwa Polisi 300 wa Tanganyika kulinda amani kule Zanzibar na kupuliza fujo.Na Ndiyo maana Kulilazimishwa Muungano wa Haraka sana..
Na Muungano huo Ukitaka Kuvunjika Utaleta Athari ikiwemo maswali kama Hayo uliyouliza Na Pengine Zanzibar wanaweza Kuishtaki Tz (Haya Ni maoni yangu Nisifungwe kwa Hayo)
Sasa Hilo ndo ulipaswa Ujiulize kwa Makini Sana 🤣🤣🤣Huo muungano uliwekwa haraka Ili kuilinda serikali mpya ya Zanzibar dhidi ya mapinduzi mengine kumbuka baada ya mapinduzi kulipelekwa Polisi 300 wa Tanganyika kulinda amani kule Zanzibar na kupuliza fujo.
Hanga alishiriki moja kwa moja mapinduzi ndio maana alikuwa makamu wa Rais wa Baraza la mapinduzi..