Miaka 22 ya TICTS nchini yafika mwisho, mamlaka ya bandari kutosaini mkataba mpya

Hii akili ya kitoto na ya Kizamani. Guys 90% ya waTZ sio waaminifu kwenye ishu nyeti.
 
Nchi za Malawi, Rwanda, Burundi, Congo RD na Zambia pia wapewe na kuendesha magati yao maalum katika bandari ya Dar es Salaam ili kuvutia mizigo na meli nyingi bandarini Dar es Salaam
Mkuu Zambia wana ZamCargo

Malawi wana Malawi Cargo...

Lakini nao wamechemka big time
 
Tunawaza sawia katika hayo mawili uliyobainisha ktk paragraphs hizo mbili, ila ktk biashara mteja ni mfalme tusichukulie kwa kuwa hawana bandari basi tuwape nafasi ya unyonge na pia wao wakubali sisi ni wateja wao hivyo mikataba / treaties iwe katika muktadha huo.

Tukumbuke wakati wa dola kubwa ya Zanzibar kuwa Mashariki ya Congo DR , Rwanda, Burundi, Tanganyika zilikuwa chini ya dola kubwa ya Sultani wa Zanzibar. Pia baada ya 1884 Ruanda-Urundi na Tanganyika zilikuwa nchi moja. Free Congo ya mbelgiji walitwaa Kigoma Tabora hadi Morogoro kumpiga Jerumani na mbelgiji kuikalia Tanganyika hadi 1924 walipoondoa majeshi baada ya kukubaliwa kutumia bandari za Kigoma na DSM . Hivyo tuna uhusiano wa karibu mno na tunaweza kufanya biashara bila vikwazo vingi.

Tusiwe kama Bolivia na Chile kufikia kutaka kufanya choyo ya pwani ya Pacific

Chile is celebrating its National Independence day amid increasing tensions with neighbouring Bolivia. Bolivia has gone to the International Court of Justice, demanding Chile negotiates an outlet to the Pacific Ocean.
 
Mkuu Zambia wana ZamCargo

Malawi wana Malawi Cargo...

Lakini nao wamechemka big time

Hapo tujiulize mbelgiji na mwingereza wakiwa wakoloni walifanikiwa bandari za Kigoma, DSM na reli ya kati kutumia au kutumika na nchi za Free Congo (DR), Rwanda ,Burundi kupitia kampuni ya AMI kwa ufanisi vipi mataifa huru haya ya kiafrika tunashindwa na mbaya tunakata tamaa hatuwezi! Tatizo hili ya umoja ktk biashara, miundo-mbinu linawezekana

HISTORIA YA KAMPUNI YA AMI NA GATI LAKE BANDARI YA DSM

March 15, 1921​

On March 15, 1921, the Belgian and British governments signed a convention concerning " the free passage of persons, mail, goods, ships, vehicles and wagons from or to the Belgian Congo ", including the protectorate of the Rwanda - Urundi.

The last Belgian manager​

From January 1992 to December 1995, Guido Fallentheyn was the last Belgian manager of the Belbases in East Africa.


This agreement was signed 100 years ago, on March 15, 1921.

Belgium leased the concession for a symbolic Franc per year, where it could build docks and warehouses, first in perpetuity, from 1956 for 99 years.
Goods to and from the Belgian colonies in Central Africa could pass tax-free via the railway. The Belgian government entrusted the operation to a private company, the Belgian East African Agency, which later became the International Maritime Agency (AMI) ...

Source : Belbases - Une page oubliée du colonialisme Belge en Afrique
 
Bakhresa mara miambili yule ni mzarendo na anauwezo na pesa yake itabaki hapahapa wanashindwa nini kumshawishi mbona kiwanda cha sukari walimshawishi na kafanya vilevile
 
Siku hizi AMI imekuwa ICD kama vi ICD vingine tu.

Sijui nani alituroga
 
Wachina wako vizuri sana kwenye suala la kuoperate mizigo bandarani ndio wanaongoza kuwa na World's busiest ports duniani. Wahindi tumepigwa hapa
Wahindi ni wazembe balaa halafu hapo bandarini patageuka Mumbai kihindi kitupu hafu hawa kunguni wa mama ni kugeuka manamba .Bibie sijui anafanyia hii nchi kwa interest ya nani .
 
Bora wangewapa wachina..!

Mara 1000% maana kwanza nchi yao ina maendeleo kidunia inaikaribia America.

Kwa Hiyo hata uwezo wa kupata mtaji na mashine za kisasa ingekuwa Kwa urahisi.

Sasa hao Wahindi jamani duuh!

Huko TRC na ATC wame-add value kiasi gani ?
 
Viwango vya huduma bandarini ni vukubwa sana kiasi cha kupandisha bei za bidhaa kwa kiasi kikubwa kwa mlaji wa mwisho ambae ni mwananchi.
 

..mbona tayari kuna ISAKA DRY PORT ambayo ilijengwa mwaka 1982 maalum kwa mizigo ya Rwanda na Burundi?
 
..mbona tayari kuna ISAKA DRY PORT ambayo ilijengwa mwaka 1982 maalum kwa mizigo ya Rwanda na Burundi?
Inawezekana sijielezi vizuri na kueleweka.

Maana yangu ni "Bandari ukingoni mwa bahari."

Hizi nchi ziruhusiwe kujenga bandari zao na kuziendesha wao wenyewe bila ya kuingiliwa na TPA, au serikali; mradi tu wafanye kazi zao ndani ya makubaliano ya mikataba iliyokubalika kati yao na Tanzania.
 
Wahindi ni wazembe balaa halafu hapo bandarini patageuka Mumbai kihindi kitupu hafu hawa kunguni wa mama ni kugeuka manamba .Bibie sijui anafanyia hii nchi kwa interest ya nani .
Hili deal walilopewa hawa Wahindi lina harufu ya ufisadi. Tuuachie muda nafasi tu tutaona huo utendaji wao kazi
 
Mwizi utaongezeka mara elfu moja, wahindi wanapenda Rushwa na kulipa wanyakazi maslahi duni tunaenda kushuhudia ujambazi wa karne
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…