Miaka 22 ya TICTS nchini yafika mwisho, mamlaka ya bandari kutosaini mkataba mpya

Miaka 22 ya TICTS nchini yafika mwisho, mamlaka ya bandari kutosaini mkataba mpya

Ohooooo, si walisema watafanya wenyewe.

Serikalini kuna kitu huwa kinafurahisha sana, huwa maamuzi yanaanza halafu ndio wanagundua kuwa hata hata plan ya kutekeleza haipo.

Kwa pale TPA manpower na miundombinu ya kuziba pengo la TICS haipo.

Yaani hadi TPA waombe vibali vya ajira, waajiri watu wapya, wafanyiwe mafunzo kazini ndipo mambo yakae sawa, sio leo wala kesho.

Ni lazima tuache maamuzi ya kukurupuka haya, awamu nyingine hii.
TPA hawawez bora aje mhindi au mvimba macho

OVA
 
Bandari zinazoshindana na bandari ya Dar es Salaam zazidi kujizatiti

Serikali kutafutia bandari biashara


Serikali ya Kenya Kutafutia Bandari Biashara​

Na ANTHONY KITIMO
SERIKALI ya Kenya imepanga kutuma wajumbe kutafutia biashara bandari ya Lamu katika mataifa jirani kuanzia wiki hii.


Hii ni baada ya meli ya tano ya mizigo kutia nanga katika bandari hiyo Jumamosi, tangu ilipofunguliwa Mei 2021.

Meli ya Uholanzi inayofahamika kama Mv Seago inayomilikiwa na kampuni ya Maersk, ilitia nanga Lamu baada ya kutoka katika Bandari ya Salalah, Oman, kupakua makasha 100 ya mizigo iliyonuiwa kuelekea Zanzibar.

Meli hiyo iliyo na urefu wa mita 294 ni refu zaidi kuwahi kutia nanga katika bandari hiyo kufikia sasa, na ni ya pili kwa urefu zaidi kuwahi kutia nanga katika bandari za Kenya.

Waziri wa Fedha, Bw Ukur Yatani, alisema meli nyingine inatarajiwa kufika wiki mbili zijazo, ishara kuwa makampuni mengi yana imani na uwezo wa bandari hiyo kuendeleza biashara zao kimataifa.
“Tangu bandari ya Lamu ilipofunguliwa, tumepiga hatua na bandari hii imedhihirisha ina nafasi bora zaidi kwa usafirishaji mizigo kimataifa,” akasema.
Akiandamana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari za Kenya (KPA), Bw John Mwangemi, waziri alisema wajumbe watatumwa Ethiopia na Sudan Kusini kutafutia soko bandari hiyo.

Kamishna wa Forodha na Usimamizi wa Mipaka katika Mamlaka ya Ukusanyaji Ushuru nchini (KRA), Bi Lilian Nyawenda, alisema kwa sasa mamlaka hiyo inatilia maanani zaidi kuwapa imani wafanyabiashara kuhusu uwezo wa Kenya kuidhinisha bidhaa kupitia nchini kwa haraka.
“KRA imeongeza wafanyakazi na vifaa katika afisi zake mipakani ili uidhinishaji wa bidhaa ufanywe haraka. Wawekezaji wakiwa na imani kwetu, mapato yataongezeka kwa urahisi,” akaeleza.

Mkurugenzi Mkuu wa Maersk ukanda wa Afrika Mashariki, Bw Carl Lorenz, alihimiza kampuni nyingine kuungana kukuza sekta ya uchukuzi wa mizigo kwa manufaa ya uchumi.

Mradi wa bandari ya Lamu ulikuwa mojawapo ya ile ambayo Rais Uhuru Kenyatta alikusudia kukamilisha kabla aondoke mamlakani baada ya uchaguzi ujao wa urais.

Kufikia sasa, Zanzibar na nchi zilizo Mashariki ya Mbali zimeibuka kuwa soko kuu la bandari ya Lamu.

Mapema Julai, meli ya kwanza ya shirika la CMA CGM ilikuwa ya kwanza kutia nanga Lamu kutoka Soviet Union, ambapo ilibeba makasha 50 yaliyokuwa yametoka Zanzibar.

Bandari hiyo haijaanza kupokea mizigo kutoka kwa malori kwa sababu ujenzi wa barabara kuu zinazotegemewa haujakamilika.

Wakati huo huo, KPA ilisema iko tayari kuhudumia meli aina yoyote katika bandari hiyo baada ya kukamilisha kuweka mashine zote zinazohitajika kupakia na kupakua mizigo mikubwa.

Source : Serikali kutafutia bandari biashara – Taifa Leo
 
Mwisho wa TICS ni mwanzo wa TICS nyingine, kwa Tanzania tegemea yaleyale au zaidi ya yale, God father wa TICS hayupo sasa amelala Lupaso, shamba linawaniwa na wahuni wengine..
Wewe ndo uliongea la maana. TICTS nyingine imekuja, inaitwa DP World.
 
Ticts ilikuwa miaka 22
Na tuliona ni miaka mingi kupita kiasi sembuse hao DP wa milele?
 
Je ni kwa nini Kenya imewakataa DP World?

Kwa nini Djibouti imewafukuza DP World?

Kwa nini Zanzibar haipo ndani ya mkataba?
 
Tatizo huwa siyo TICTS wala DP World, bali tatizo liko kwenye management ya Bandari. Wakati Kakoko akiwa mkurugenzi wa Bandari, ucheleweshaji wa mizgo ulipungua sana baada ya Magufuli na Majaliwa kuwasimamia kwa ukaribu. Usimamizi ukipotea na uongozi kuzorota, madudu yanarudi pale pale.
 
Back
Top Bottom