Namkubali sana huyu mzee sababubya sisi wabongo muislam kumuoa mkristo na mchaga kjmuoa msukuma bila shida ni huyu mzee.
Ni kawaida mtu kuhudhuria msiba wa mtu asiyemjua kwenye nzengo na kuchanga michango yote kiroho safi kabisa
Ni kawaida mbongo kumsaidia mttu mwingine hata kama hawajuani.
ni kazi ya huyu mzee kupitia sera yake ya ujamaa ambayo iliota mizizi na kuwa mbuyu mkubwa ambao bado unaishi ktk jamii hadi leo licha ya mfumo wa kiuchumi kubadilishwa ila misingi ya undungu bado inaishi.
Wengi huona ni kawaida bilavkujua kazi kubwa aliyoifanya huyu mzee. Baada ya kuona watu wanakaidi kutii sera ya ujamaa akaagiza jeshi liwaweke wachaga wasukuma wagogo wahaya n.k kijiji kimoja (wachanganyikane,) ktk maeneo tofauti nchini akilenga kujenga umoja na utamaduni wa psmoja huku kiswahili kikifundishwa kwa nguvu kubwa ili waweze kuwasiliana kwa lugha moja
Apumzike kwa amani.