Miaka 27 ya MV Bukoba. Leo wachezaji wakae kimya kwa dakika moja kwa ajili ya kumbukumbu ya marehemu wa MV Bukoba.

Miaka 27 ya MV Bukoba. Leo wachezaji wakae kimya kwa dakika moja kwa ajili ya kumbukumbu ya marehemu wa MV Bukoba.

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
18,037
Reaction score
33,681
Tarehe 21 mwezi May mwaka 1996 ilitokea ajali mbaya ya meli kwenye Ziwa Victoria kilomita chache kabla ya kufika kwenye bandari ya jiji la Mwanza.

Meli ya MV Bukoba ilipinduka na kuchukua maisha ya watu takribani elfu moja.

Leo imetimia miaka 28 tangu kutokea tukio hilo ambalo ni miongoni mwa matukio mabaya kabisa kutokea tangu nchi yetu kupata uhuru.

Tunawaomba leo TFF kwenye mechi ya Simba kuwe na moment of silence kwa ajili ya kuwakumbuka marehemu wote walio poteza maisha yao kwenye ajali hiyo.

Mwenyezi Mungu aendelee kuzilaza mahala peponi roho za marehemu wote walio fariki kwenye ajali hiyo.

Ameen!
 
naomba na huyu robot pia kukaa kimya
Screenshot 2024-05-17 170100.png
 
Tarehe 21 mwezi May mwaka 1996 ilitokea ajali mbaya ya meli kwenye Ziwa Victoria kilomita chache kabla ya kufika kwenye bandari ya jiji la Mwanza.

Meli ya MV Bukoba ilipinduka na kuchukua maisha ya watu takribani elfu moja.

Leo imetimia miaka 27 tangu kutokea tukio hilo ambalo ni miongoni mwa matukio mabaya kabisa kutokea tangu nchi yetu kupata uhuru.

Tunawaomba leo TFF kwenye mechi ya Simba kuwe na moment of silence kwa ajili ya kuwakumbuka marehemu wote walio poteza maisha yao kwenye ajali hiyo.

Mwenyezi Mungu aendelee kuzilaza mahala peponi roho za marehemu wote walio fariki kwenye ajali hiyo.

Ameen!
RIP wote waliopoteza maisha katika ajali hii. RIP my Sister!
 
Tarehe zingine hizi ni balaa vipi walio zaliwa tarehe ya leo?
Kwahiyo kila tarehe ambayo itatokea ajali inakua hiyo ni tarehe mbaya?
Kuna tarehe zingine hua ni nzuri na hakuna uwezekano wa ajali kutokea kisa tarehe?

Mpaka sasa tunazo tarehe ngapi ambazo ni mbaya kisa tu tarehe hizo zilitokea ajali?
 
Kama huo mwaka ulioandika ni sahihi basi siyo miaka 27 ni 28, by the way kama watalifanyia kazi hili basi nitaamini viongozi wa hizi timu huwa wanapita humu, hivyo wanaweza kufanyia kazi na maoni mengine muhimu ya wadau kuhusiana na hizi timu
 
Aisee kweli ni 28.
 
Hakuna tatizo kabisa kwanza siku ya leo ndio siku ya kwanza ya mzunguko ya nyota ya Gemini, nyota kubwa kuliko zote duniani
Mkuu hii sasa kwa wali zaliwa inaishara gani kuhusu nyota je ni ya nuru au ya shari? Mana tarehe kama ya leo ndo siku yangu ya kuzaliwa
 
Back
Top Bottom